Nimekuelewa.Ukishasajili kampuni yako, utatakiwa upate TIN ya kampuni, then Ukaombe leseni yako katika ofisi za halimashauri ya mji/jiji zilipo ofisi za shughuli zako, ila kabla ya kupewa itabidi TRA wakukadirie mapato, ulipe hilo kadirio kwa installment angalau moja, kisha watakupatia Tax Clearance.....itakayo kusaidia kupata hiyo leseni....makadirio huko TRA itategemea tu mtakavyohojiana na afisa wa TRA.
Ukitaka usaidizi kupitia hatua zote tangu kusajili kampuni hadi TRA twendelee kuwasiliana....
Zaidi sana huo mtaji wako unaangaliwa kwenye Business Licence. Huko TRA wanaangalia faida. Sasa makadirio ya Kodi ni vile utakavyotamka matarajio ya mapato yako.Asante.