Makadirio ya tofali za uzio

sixlove

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
563
Reaction score
393
Habari wanajamvi.

Samahani nina kiwanja kina ukubwa wa 2430 square meter.

Nataka nijenge uzio ambao ni standard, namaanisha uwe na urefu toshelezi.

Msingi una urefu wa futi mbili kutoka ulipochomoza kwenye ardhi.

Je, yatahitajika matofali mangapi ya inch 5 kukamilisha ujenzi wote wa fence?

Natanguliza shukrani
 
Neno toshelevu ni subjective...
 
Ndio maana huwa najenga nyumba halafu ndio naweka uzio. Yaani roho inaniuma kuona matofali ya uzio yanazidi ya kujenga nyumba nzima.
 
54 ×45. Asante
Hapo zitaingia tofali 5660, msingi kozi 6 (kozi 4 chini ya ardhi, kozi 2 juu ya usawa wa ardhi), juu kozi 8 kwa fence yenye ukuta plain bila yale madirisha ya urembo/louvers

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kozi nane sio fupi sana?
 
Kozi nane sio fupi sana?
Kozi 8 ni sawa na urefu wa mita 2+ (ukijumlisha na kozi za msingi zilizotokeza juu ya usawa wa ardhi almost total inakuwa kama 2.4m+ (sawa na futi 8).

Average height ya watu wa sasa ni around 5ft-6ft (wachache wanaozidi 6ft, kwa hivyo mtu akitembea nje ya fence hawezi akaona ndani kupitia usawa wa fence mpaka apande juu ya fence)
 
Hapo zitaingia tofali 5660, msingi kozi 6 (kozi 4 chini ya ardhi, kozi 2 juu ya usawa wa ardhi), juu kozi 8 kwa fence yenye ukuta plain bila yale madirisha ya urembo/louvers

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Asante sana,,nimepata somo zuri sana. Lengo langu ni kujenga uzio ambao ukiwa kwa nje utaona paa lilipoanzia tu. Mzunguko wa hewa upo wa kutosha. Maana lengo langu kubwa ni ufugaji kwenye hilo eneo. Ubarikiwe ndugu
 
Pamoja na hoja zote zilizowtolewa na wadau, ni muhimu pia kuwa na michoro kwaajili ya uzio wako.

Hivi sasa fence sio tu ni suala la kuficha vilivyo ndani bali pia ni moja ya sehemu ya urembo wa kupendezesha muonekano wa jengo lako. Na hii hufanya idadi ya matofali kuwa kubwa au ndogo.

Kwa ukubwa wa eneo hilo hilo mnaweza kutumia tofali za idadi tofauti kabisa hata kama viwanja vyenu vinakaribiana. Hii ni kutokana na design husika ya fence.

Hivyo nashauri, ni bora ukatafuta mchoro madhubuti wa fence, na kutokea hapo utapata uhalisia wa ni matofali kiasigani, nondo, mchanga, cement, kokoto, marine n.k utakazo hitaji wakati wa ujenzi.

Hii itakusaidia Luanda bajeti itakayo maliza kazi mwanzo hadi mwisho.

Be blessed.

Cheers 🥂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…