'Makahaba' walalamikia polisi

Soma kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Kujamiiana hapa: http://www.hsph.harvard.edu/population/trafficking/tanzania.sexoffenses.98.pdf

Unataka kuniambia kuwa sheria imebadilika na kuhalalisha prostitution?

Mkuu EMT, my worry is, kila nikisoma kifungu unachokisema sioni actus reus ya offence ya prostitution katika hiki kifungu na kama hakuna actus reus basi ina maana hakuna kosa kama hilo. The provision was badly drafted I mont sure if it was by default or by design!!!!!!!!! Maneno procure na prostitution peke yake kamwe hawezi kuleta actus reus
 
Ngambo Ngali & EMT

Huu mjadala japo mmeuchukua ninyi lakini nadhani unaathiri jamii kubwa ya hawahakina mama wanaoitwa "makahaba"...! Endeleeni ku-brain-storm maana mnaweza kusaidia hii jamii iliyotengwa na kudharirishwa...!
 
Last edited by a moderator:
Huyu kamanda anatakiwa akajifunze kwa mwenzake wa Temeke,nadhani hajui sheria za nchi
 

Kifungu kimetumia "procure" or "attempt".

Actus reus ya "attempt" ni nini?
 

Ili mtu apatikane na hatia ya kufanya ukahaba ni lazima awe kafanya nini? Na kuna vice squads ambazo huwa zina carry out sting operations?

Maana sehemu zingine ili mtu apatikane na hatia ya ukahaba kama hiyo sehemu ukahaba ni illegal basi ni lazima kuwe na mabadilishano angalau ya pesa in return for sex (oral or penetrative).

Matokeo yake wanashusha kosa na kuwashtaki kwa kosa la "uzembe na uzururaji".

Na "uzembe na uzururaji" unafasiliwaje na sheria?
 

Umenikumbusha the famous case of Smith v Hughes [1960] 2 All E.R. 859 on the mischief rule of statutory interpretation

The UK Street Offences Act 1959 made it a criminal offence for prostitutes to "loiter or solicit in the street for the purposes of prostitution".

The defendants were calling to men in the street from balconies and tapping on windows. They claimed they were not guilty as they were not in the "street."

The judge applied the mischief rule to come to the conclusion that they were guilty as the intention of the Act was to cover the mischief of harassment from prostitutes.: http://en.wikipedia.org/wiki/Mischief_rule

Na "uzembe na uzururaji" unafasiliwaje na sheria?

I have got no clue Sir. Nafikiri hilo kosa liliwekwa kwenye vitabu vya sheria wakati wa utawala Nyerere na sera zake. Enzi za utawala wake watu wengi tuu walikamatwa na kushtakiwa under this offence.

Kwa siku hizi ambapo watu wengi hawana hata hela ya nauli anaweza kupiga mguu kutoka Buguruni kwenda Mbagala usiku halafu akakamatwa njiani na polisi kwa kosa za "usembe na uzururaji". Wapo ambao walishalalamikia kuwa kosa la "uzembe na uzururaji" ni la kibaguzi na liondolewe kwenye vitabu vya sheria.

========

Sheria hii ya kibaguzi iondolewe

".......Leo nami napendekeza baadhi ya sheria za ukandamizaji katika katiba zifutwe. Moja ya sheria hizo ni ile ya uzembe na uzururaji kwa sababu ni ya ubaguzi tena wa hali ya juu. Nitatoa mfano. Siku moja saa sita usiku nikiwa katika gari na rafiki yangu tulipita maeneo ya Buguruni. Nilishuhudia vijana na wazee, wake kwa waume wakiwa wamekusanywa na polisi.

Wanaume walikuwa wamefungwa mashati na wanawake wamepangwa msitari wakielekea Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar.
Alikuwepo baba mmoja ambaye alikuwa akijitahidi kuwaomba askari polisi kwamba aachiwe kwa kuwa alikuwa akitoka Kigamboni kwa miguu.

Alisema kwa kuwa hakuwa na nauli aliamua kutembea kutoka Ferry kwenda Vingunguti kumuona mgonjwa, hakusikilizwa. Alifungwa shati na safari ikaanza kuelekea kituoni. Kesho yake wote walipelekwa mahakamani wakishitakiwa kwa uzembe na uzururaji.

Ulikuwa ni ubaguzi kwa sababu sisi ambao tulikuwa kwenye gari licha ya kusimama na kusikiliza kile walichokamatiwa, polisi hawakutuuliza wala kututuhumu kwa uzururaji japokuwa kweli tulikuwa tunazurura. Kwa nini hawakututuhumu? Jibu ni rahisi. Tulikuwa kwenye gari ndiyo maana hatukukamatwa. Huu ni ubaguzi wa hali ya juu na ni kinyume na haki za binadamu.

Yule mzee ambaye alikuwa akienda kumuona mgonjwa alionekana ni mzururaji na sisi tuliokuwa tunazurura ndani ya gari tukaonekana ni waheshimiwa.

Naamini kabisa kwamba sheria hii itafutwa na haitaonekana katika katiba mpya ambayo imeanza mchakato wake. Naiomba tume inayofanya mchakato wa kupata katiba mpya chini ya Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Sinde Warioba iliangalie hili. Sheria za ukandamizaji zipo nyingi lakini kwa leo niwasilishe hili. Naomba kutoa hoja."

Chanzo: Sheria hii ya kibaguzi iondolewe - Global Publishers
 
Actus reus ya "attempt" ni nini?

Attempt haina actus reus kwani offence inakuwa haijafanyika, kunakuwa na mens rea however actus reus inakuwa haipo, the moment the mens rea is implemented then the offence will have been committed and as such there cannot be an attempt to commit the offence.
 

NN hapo ndipo mapungufu ya kisheria yalipo, watunga sheria walikuwa na haraka sana wakasahau kuweka elements za offence ya prostitution wakaishia kuidefine tu
 
Iwapo wakabadilisha wakawa wanatoa bure kama kuwaondolea stress watu wenye mtindio wa kutongoza! Je, napo watakuwa wametenda kosa kutoa free service!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…