Ili mtu apatikane na hatia ya kufanya ukahaba ni lazima awe kafanya nini? Na kuna vice squads ambazo huwa zina carry out sting operations?
Maana sehemu zingine ili mtu apatikane na hatia ya ukahaba kama hiyo sehemu ukahaba ni illegal basi ni lazima kuwe na mabadilishano angalau ya pesa in return for sex (oral or penetrative).
Umenikumbusha the famous case of
Smith v Hughes [1960] 2 All E.R. 859 on the mischief rule of statutory interpretation
The UK Street Offences Act 1959 made it a criminal offence for prostitutes to "loiter or solicit in the street for the purposes of prostitution".
The defendants were calling to men in the street from balconies and tapping on windows. They claimed they were not guilty as they were not in the "street."
The judge applied the mischief rule to come to the conclusion that they were guilty as the intention of the Act was to cover the mischief of harassment from prostitutes.:
http://en.wikipedia.org/wiki/Mischief_rule
Na "uzembe na uzururaji" unafasiliwaje na sheria?
I have got no clue Sir. Nafikiri hilo kosa liliwekwa kwenye vitabu vya sheria wakati wa utawala Nyerere na sera zake. Enzi za utawala wake watu wengi tuu walikamatwa na kushtakiwa under this offence.
Kwa siku hizi ambapo watu wengi hawana hata hela ya nauli anaweza kupiga mguu kutoka Buguruni kwenda Mbagala usiku halafu akakamatwa njiani na polisi kwa kosa za "usembe na uzururaji". Wapo ambao walishalalamikia kuwa kosa la "uzembe na uzururaji" ni la kibaguzi na liondolewe kwenye vitabu vya sheria.
========
Sheria hii ya kibaguzi iondolewe
".......Leo nami napendekeza baadhi ya sheria za ukandamizaji katika katiba zifutwe. Moja ya sheria hizo ni ile ya uzembe na uzururaji kwa sababu ni ya ubaguzi tena wa hali ya juu. Nitatoa mfano. Siku moja saa sita usiku nikiwa katika gari na rafiki yangu tulipita maeneo ya Buguruni. Nilishuhudia vijana na wazee, wake kwa waume wakiwa wamekusanywa na polisi.
Wanaume walikuwa wamefungwa mashati na wanawake wamepangwa msitari wakielekea Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar.
Alikuwepo baba mmoja ambaye alikuwa akijitahidi kuwaomba askari polisi kwamba aachiwe kwa kuwa alikuwa akitoka Kigamboni kwa miguu.
Alisema kwa kuwa hakuwa na nauli aliamua kutembea kutoka Ferry kwenda Vingunguti kumuona mgonjwa, hakusikilizwa. Alifungwa shati na safari ikaanza kuelekea kituoni. Kesho yake wote walipelekwa mahakamani wakishitakiwa kwa uzembe na uzururaji.
Ulikuwa ni ubaguzi kwa sababu sisi ambao tulikuwa kwenye gari licha ya kusimama na kusikiliza kile walichokamatiwa, polisi hawakutuuliza wala kututuhumu kwa uzururaji japokuwa kweli tulikuwa tunazurura. Kwa nini hawakututuhumu? Jibu ni rahisi. Tulikuwa kwenye gari ndiyo maana hatukukamatwa. Huu ni ubaguzi wa hali ya juu na ni kinyume na haki za binadamu.
Yule mzee ambaye alikuwa akienda kumuona mgonjwa alionekana ni mzururaji na sisi tuliokuwa tunazurura ndani ya gari tukaonekana ni waheshimiwa.
Naamini kabisa kwamba sheria hii itafutwa na haitaonekana katika katiba mpya ambayo imeanza mchakato wake. Naiomba tume inayofanya mchakato wa kupata katiba mpya chini ya Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Sinde Warioba iliangalie hili. Sheria za ukandamizaji zipo nyingi lakini kwa leo niwasilishe hili. Naomba kutoa hoja."
Chanzo:
Sheria hii ya kibaguzi iondolewe - Global Publishers