MAKALA: Hili la Perfume, Diamond ataandika historia nyingine muhimu kwake

Maboso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
5,164
Reaction score
5,762
Kwanza nikiri kuwa, Diamond ana fursa nyingi za wazi wazi ambazo ameziacha tu zipite. Kwa umaarufu aliojikusanyia hadi sasa katika bara zima, alipaswa kuwa na miradi mingi chini ya jina lake ambayo ingekuwa inamuingizia mamilioni ya fedha, ukiacha zile anazopata kutokana na muziki wake.

Lakini bado hajachelewa na kwakuwa ukubwa wake unaanza kuizidi nguvu timu yake, mambo mengine yatakuja pole pole, na uzuri tayari tumeanza kuyaona. Nafahamu kuwa aliwahi kuonesha interest ya kuanzisha clothing line yake ya WCB ambayo hata hivyo aliishia kutoa bidhaa chache tu zilizovaliwa na watu wa karibu na hazikuwahi kuingia sokoni kwa ukubwa uliotarajiwa. Hicho ni kitu ambacho huenda akawa amekiweka pending kwa muda.

Leo nichukue fursa kumpongeza kwa kuonjesha mradi wake mkubwa wa perfume aliyoipa jina la utani, Chibu. Ni hatua kubwa sana, tena kutoka kwa msanii wa Tanzania. Sina idadi kamili ya celebrity wa Afrika wenye bidhaa ya aina hiyo, na kama wapo basi ni wachache sana. Tumezoea perfume kuwa ni kitu kinachofanywa na mastaa wakubwa duniani kama Nicki Minaj, Beyonce, Diddy, David Beckham na wengine, hivyo kwa msanii wa Tanzania kuja na kitu kama hicho na tena kinachoonekana kuwa si cha mzaha, si suala la kuchukulia poa.

Diamond anastahili pongezi kwa uthubutu huo na kuionesha Afrika kuwa, Mtanzania anaweza kufanya kitu kikubwa. Ujio wa perfume yake, ni udhihirisho tosha kuwa sasa muimbaji huyo anazidi kujitambua kuwa brand yake imekuwa kubwa na anaingia rasmi kwenye biashara ya muziki yenye matawi mengi. Katika daraja analoingia sasa, Diamond ataanza kuifaidi fedha wanayoifaidi mastaa wakubwa katika nchi zilizoendelea.

Ametambua kuwa kwa hatua aliyofikia, si muziki wake pekee unaouza, bali ni jina lake ndilo lenye thamani zaidi ya kitu chochote kwa sasa. Ametambua kuwa, amefika katika anga ambazo hamlazimu tena kutegemea muziki, endorsement na show peke yake, bali kwa mtaji wa jina lake na wafuasi wake, anaweza kutengeneza fedha kubwa zaidi.

Hatua hiyo inazidi kumweka katika ligi ya juu inayochezwa na wanamuziki wenzake nguli Afrika. Na kwakuwa si nguli wengi wa level yake wana mradi kama huo, inampa upekee zaidi na kuipa heshima Tanzania. Na pengine jambo kubwa zaidi, ni ari ya uthubutu anayoipandikiza kwa mastaa wengine wa Bongo na kuwatengenezea njia za kupita watakapo kufanya uwezekazaji wenye sura ya ukubwa kama huo anaoenda kuufanya punde.

Heko kwa Diamond na bila shaka perfume yake itapata mapokezi mazuri nje na ndani ya Afrika.

CREDIT TO: BONGO5
 

X
 
Ni kweli mkuu...hakika huku ndiko kukomaa katika sanaa..lazima uonyeshe utofauti..

Bongo hii mimi namkubali diamond na Jokate Mwegelo,hawa vijana wanajua kuutumia umaarufu wao kuingiza kipato
 
Ntakuwa mmoja wao wakaonunua hiyo Bidhaa, ila jina Chibu? mmh unaenda dukani unaomba parfme ya Chibu? bora angeita tu hata Bi Sandra.
 
Ntakuwa mmoja wao wakaonunua hiyo Bidhaa, ila jina Chibu? mmh unaenda dukani unaomba parfme ya Chibu? bora angeita tu hata Bi Sandra.
Hahhhahahah jamani nimecheka mie naona bora ya chibu! [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Safi.... hii sasa akili.
 
Hii biashara kibongo bongo hailipi kwasababu raia hawadhamini cha nyumbani alikuja na wazo la nguo sijui ilishia wapi? wabongo kma roho za Kwann


Rihana alitengeneza lipstick zake ndani ya siku moja bidhaa ikawa imeisha na alitengeneza hela ndefu sana

jamani tusupport cha nyumbani
 
Wema alitengeza Lipstick zake... Aliishia kukesha nazo
 
Kwa jina la chibu brand name haiko sawa kwa kuwavutia wateja na kama sadra kama ni ya kike ingekua imekaa sawa
 
Ntakuwa mmoja wao wakaonunua hiyo Bidhaa, ila jina Chibu? mmh unaenda dukani unaomba parfme ya Chibu? bora angeita tu hata Bi Sandra.
Hahaha nimecheka hii comment. Naisubiri kwa hamu mie ninukieee.
 
Hii ishu unajua imekaa kibongo bongo zaidi lakini kwa suala la branding ukweli ni kwamba hata diamond mwenyewe halijui na liko nyuma sana hapa nchini ni kitu ambacho kitaiua biashara yake hiyo mapema.

Kwanza diamond mwenyewe hajajua umuhimu wa kutengeneza brand ndio maana leo anajiita diamond,kesho bin laden,kesho kutwa Simba,mtondogoo anajiita chibu hapo anakuwa anapandisha brands nyingi kwa pamoja ambapo hakuna mtu mmoja anaeweza kuzipandisha zote zikafanya poa.hata instagram yake kajiandika Rolls Royce musician hilo jina la gari mara chibu dangote hilo dangote ni brand ya mtu na mwenye nayo kaiweka sehemu zote 2 a
Kama kampuni na pia jina lake mwenyewe.

Kwa upande wa hiyo pafyumu sijajua kwa upande wa bei lakini kama akiwalenga mashabiki wake itauza sana ila kama akiiweka ipambane na brands nyingine itafeli kwa sababu chibu sio brand iliyofanikiwa imebidi hadi kwenye kasha iandikwe from Diamond Platnumz na picha yake hiyo yote ni kuibust ili ionekane ni yake sasa,ikitoka nje ya mipaka ya Tz ambako hawayajui majina ya chibu dangote bin laden simba haiwezi kuuza sababu hawatanunua diomond platnumz ila watanunua chibu hapo ndio itakapofeli sasa.

Angeanza kwa kujielewa kwanz na kusimamish brand moja halafu biashara zake zingekuja kutoka kwa kujitegemea bila kumtegemea yeye ila nguvu ya brand yake ambapo ingekuwa ni hadhi yake ukisema nick minaj katoa pafyumu brand ni nick minaj so watu wanafatilia brand imetoa sub brand gani ila sasa chibu katoa pafyumu ya chibu,simba katoa pafyumu, Diamond katoa pafyumu,dangote katoa pafyumu .

Ishu iko deep sana kibiashara na ndio maana bidhaa nyingi zinafeli.

Brand ya mfano kwa watu maarufu wajaribu kumuiga Jokate na Kidoti anafanya poa sababu amesimama vizuri na kila kitu kinajitegemea daah nikiandika ni mengi sana ngoja niishie hapa.
 
Ntainunua pia ila wahuni wasije ichakachua
 
Atauza sana.
Na ndo maana ya kazi yake inapokuja apo.
Long term investment kama izo zafaa sana siku mziki unashuka bado unakamua kupitia bidhaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…