Sprian joseph
New Member
- Jul 28, 2022
- 2
- 0
Kilimo nchini Tanzania huleta tija kwa wanajamii waliopo pembezoni na wao wakifaidika.
Kilimo ni moja ya shughuli za kila siku kwenye maisha ya binadamu na hutegemeana na maeneo husika Kikilimo ili mkulima aweze kulima na kuvuna mazao yake huku akipata faida. Nchini kwetu Tanzania wakulima wengi hulima kutegemeana na maeneo walipo, asili yao kwenye masuala ya Kilimo au mbinu wezeshi walizopewa kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya kilimo waliyekutana nae.
Wakulima wengi nchini hutumia aina mbili za kilimo wakianza na kilimo cha asili huku wakimalizia na kilimo cha kisasa ambapo huwapa wao fursa ya kujifunza zaidi kuhusu kilimo.Wanajamii wengi walio nje ya miji nchini wanapoachana na shughuli zingine za kiutafutaji huwa wanajihusisha kilimo kama biashara yao ya kando huku baadhi yao wamekuwa na wasiwasi kwamba mbinu za kilimo zilizotumika katika kipindi cha miaka 30 hadi 40 zinaweza kuharibu mazingira na kupunguza ubora wa chakula.Takriban nchi zote Duniani zilianza na umaskini Kiuchumi na ni nchi chache tu ambazo zimefikia hali ya kipato cha juu hata hivyo, waliofanikisha hilo walianza na kilimo.
Jamii zetu za Kitanzania zitakapojihusisha na Kilimo ipasavyo zinaweza kupata faida za aina mbalimbali wakianzia na Kujipatia Kipato huku wakitunza Ardhi yao wanayoimiliki ipasavyo na wao kujipatia chakula cha kutosha kwa ajili ya jamii zao.
Kilimo pia kitawafanya wakulima wetu kutambuana au kujuana na wakulima wengine waliopo kwenye soko la kilimo huku wakibadilisha ujuzi wa namna ya kulima kwa kanuni za kisasa kiulimaji na kupitia fursa hiii ya kisoko wakulima wetu watajifunza au kupata mbinu mbadala kikilimo kwenye msimu mwingine wa kilimo.
Nchini kwetu wakulima wetu wamekuwa wakikumbana na changamoto za aina mbalimbali kikilimo mpaka kutofikia malengo yao waliyojiwekea kwenye shughuli zao za ulimaji.
Changamoto wanazokutana nazo wakulima wetu kwenye kilimo nchini Tanzania ni kama ifuatavyo
wadudu waharibifu kuharibu mazao kabla ya muda wa uvunaji
mvua zisizo tosha kiumwagiliaji hii husababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi na kwa kukosa soko lenye bei wezeshi kwa mkulima.
Changamoto hizi chache na nyingine huwafanya wanajamii au wakulima waliopo kukimbia kilimo nchini Tanzania au wao wenyewe kwa maamuzi ya kupumzika kilimo kwa baadhi ya misimu ya ulimaji. Wakulima wetu nchini Tanzania wanapaswa kufuata mbinu mpya za Kilimo ili waweze kupambana na changamoto zinazowakabili kama nilivyozitaja hapo juu.
Mbinu wanazopaswa kuzitumia ili walime kwa manufaa na mazao yao kutoharibiwa na wadudu ni wawe wanamwagiliaji madawa yanayouua wadudu waharibifu wa mazao,watumie mbegu za kisasa kukabiliana na changamoto ya mbegu za asili na walime kulingana na majira ya mvua wezeshi kwenye kilimo kwa kuchukua hatua hizi na zingine mahususi zitawawezesha kufurahia kilimo chao kama ilivyokuwa kwa wakulima wa awali au walionza kilimo kabla yao.
Mkulima atapowekeza kwenye kilimo ni mtaji wake kwenye jamii husika kwenye masuala ya kilimo kwani yeye mwenyewe ndiye atafaidika na hatua kilimo kwenye uvunaji mazao. Uwekezaji huu huwa mtaji wa kijamii kwani kilimo huchukua muda kidogo mpaka mazao yanapostawi.Ustawi ambao humfaisha mkulima kwa kupata idadi kubwa ya mazao shambani.Zaidi ya kuhifadhi ardhi zao, maendeleo yanayotokana kilimo yanakuza jamii zenye afya ambazo zinakuza maisha yenye afya timilifu kwa wakulima na familia zao kingine ni kujenga uhusiano thabiti kati ya watu wa jamii moja na nyingine na kuwa na hifadhi kubwa au yakutosha ya chakula chao na majirani zao.
Ukosefu au upatikanaji finyu wa chakula kwa afya na lishe huongeza hatari ya watoto wa wakulima husika kukumbana na baadhi ya magonjwa yatokanayo na ukosefu wa lishe timilifu.Jamii ambazo huwa hazipati chakula au lishe ya kutosha hukumbana na magonjwa kama Utapiamlo na Kwashakoho kwa watoto wanaoanzia miaka 0-5,Upungufu wa damu kwa watoto na hata vijana na Upungufu wa Protini mwilini.
Kuongeza kilimo wezeshi kwa jamii kutakuza elimu katika kilimo, uzalishaji wa chakula na uhifadhi wa ardhi katika wigo mpana. Hili huwezesha shule za msingi kujumuisha kilimo katika mtaala wao. Hii itatoa upana kwa warsha za Mkulima kwa Raia kufundisha jamii husika kujihusisha zaidi katika jamii yao na masuala yanayohusu kilimo. Hii pia inatoa jukwaa la mafunzo ya kizazi kijacho kufundisha na kufanya kilimo endelevu kwa siku zijazo.
Akiba ya mazao husaidia kuweka hifadhi ya chakula katika uchumi wa ndani na kusaidia wakulima wenyewe kuanza kufanya biashara ndogo ndogo ya kuuza mazao yao waliyoyavuna. Mashamba ya wakulima wa jamii husika yanaweza kutumika kama majukwaa ya bidhaa na huduma zinazokua kutoka shambani, kama vile bidhaa za chakula zilizoongezwa thamani, elimu ya bustani na huduma za usimamizi, programu na matukio shambani.
Tutakapokitumia Kilimo vizuri kwenye ardhi yetu ya Tanzania kitatufaidisha vya kutosha ukizingatia Tanzania ni nchi pendwa kimasoko ya chakula na majirani zake au wake anapakana nao kimpaka na hata nje ya nchi.Tutakuwa na fursa kubwa kama nchi na hata mkulima mmoja mmoja kulingana na mazao watakayokuwa wanayoyalima.
Kilimo pia husaidia mifugo inayofugwa na wakulima kupata chakula cha malisho bila ya kwenda umbali mrefu kimalisho huku kama mifugo kama ng`ombe ,mbuzi,kondoo na nk wakipata nafuu ya maliso.Kilimo pia husaidia mmony`oko wa udongo kupungua kwa kiasi ambao hutokana na ardhi kuwa pweke kishughuli za kimaendeleo au kiutafutaji.

Attachments
Upvote
2