Septem
JF-Expert Member
- Feb 14, 2018
- 313
- 404
'Ni wajibu wa asili wa wale waliobahatika kupata elimu kutumia elimu zao kuwaelimisha wale wasiokua na elimu'-Mwalimu. Mimi ni muumini wa mtazamo huu Mwalimu juu ya elimu. elimu hii maanaishi 'kutokwenda shule' bali ni msingi kuwa watu tuna maeneo tofauti ya utaalamu na ujuzi. hivyo ni muhimu kushare ujuzi.
Kwa kuzingatia mapenzi yangu katika kujisomea na kuandika sambamba na taaluma yangu katika fani ya Sheria, huu utakua ni mfululizo wa makala zangu juu ya masuala mbalimbali ya kisheria. Nitaanza na makala hii ya kwanza ikizungumzia ni jinsi gani unavyoweza kujiepusha na 'kunasa katika mtego wa jinai' katika maisha yetu ya kila siku pasi na wewe mwenyewe binafsi 'kushiriki katika jinai'.
Nitaeleza kwa kifupi kwanza ni nini jinai na masuala kadhaa yanayoitengeneza jinai. katika mfumo wa kisheria kuna makosa ya namna mbili, JINAI na MADAI.
Katika mahusiano katika ya nchi(state) na raia wake upo utaratibu uliowekwa na sheria ili kusimamia mahusiano haya-i.e ni vipi raia hawa waishi, hivyo matendo yoyote yanayofanywa na raia ambayo yanaathiri/kuimiza nchi-jamii nzima-(JAMHURI kwetu Tanzania) haya yanaitwa MAKOSA YA JINAI. Yapo makosa dhidi ya Mamlaka kama vile uhaini, kuchochea vita; makosa yanayoathiri mahusiano ya nchi moja na nchi nyingine mfn uharamia, yapo makosa dhidi ya maadili kama vile kubaka, ulawiti, mapenzi kinyume na maumbile n.k. makosa haya yanaainishwa na sheria za nchi mfn kwa Tanzania makosa haya yanaainishwa na sheria mbalimbali za nchi mathalani KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,1977 (katika makala hizi nitaaita KATIBA), na SHERIA YA KANUNI ZA ADHABU SURA NA 16 YA 2002(PENAL CODE; Katika makala hizi nitaiita CODE) n.k. Makosa ya JINAI yote muathirika ni JAMHURI na ndio mshitaki huku vyombo vya dola kama POLISI wakihusika na mwenendo mzima.
Sambamba na hilo yapo makosa yanayohusiana na mahusiano kati ya mtu na mtu (ambapo Jamhuri haithiriki moja kwa moja). Haya ni makosa ya MADAI.makosa ya namna hii ni kama kutolipa madai kama mshahara, makubaliano mbalimbali-ingawa yapo mazingira ambayo madai hugeuka jinai (hii ni mada nyingine).
Hapa nitajikita katika jinai. Kisheria jinai inatazamwa kwa kuangalia mambo mawili-KITENDO (lugha ya kisheria inaitwa Actus reus) na NIA OVU (ikiitwa Mens rea). haya kwa pamoja yakitokea ndio yanatengeneza jinai.Mathalani. Mathalani, Mary alimtusi John, John kwa ghadhabu akachukua mpira na kumpiga nao kichwani Mary, haikupita saa 1 Mary alipoteza Maisha. hapa kuna masharti yote mawili (Kitendo na Nia ovu) hivyo Jinai ya Mauaji imetimia. Chukua mfano huu pia, John akiwa anacheza mpira, alipiga shuti kali kuelekea golini, mpira ule ulitoka nje ya uwanja na kumpiga kichwani mpita njia na kufariki papo hapo. Hapa pamoja na kua Mary amefariki, lakini Jinai ya Mauji haikutimia sababu pamoja na kua kitendo kipo lakini hakukua na NIA OVU. Hivyo Nia ovu inapimwa kwa kuangalia mtenda jinai alijua matokea ya kitendo chake-kama mtu mwenye akili timamu- na pia kusudio lilikuwepo. Nia ovu (intentiion) ni tofauti na sababu ya kufanya hicho kitendo(motive). sababu yaweza kuonekana nzuri machoni pa watu lakini hailalishi kosa. mfano, kuiba maji katika ghala la Bonite na kuwagawia watoto yatima hakufanyi jinai isiwepo.
Katika utendaji wa jinai kwa sheria za tanzania kuna makundi mawili ya wahusika katika jinai moja. wapo washiriki wa moja kwa moja/washiriki wakuu(Principal offenders) na washiriki baada ya kitendo kikuu/washiriki baada(accessory after the fact). Tuchukulie mfano wa kosa la ujambazi (armed robbery). Tukio la ujambazi ni tukio lenye kuhitaji maandalizi, utekelezaji na ukimbiaji baada ya kosa. hivyo maandalizi na utelekelezaji(kwetu tunaaita Principal offending) na ukimbiaji (accessory after the fact). hivyo kosa lote kwa mtiririko wake wa ushiriki wote ni jinai ya ujambazi. Hivyo katika muktadha huu wanadamu tunajikuta tumenasa katika makosa haya ya jinai hata kama hatukua na nia hasa ya ushiriki. bahati mbaya zaidi Upelelezi wa jinai unaofanywa na polisi unajikuta unawakumba na kuwaathiri watu wengi hii kuwapotezea muda, fedha, na kupata maradhi mbalimbali. Hivyo katika maisha yetu ya kila siku ni vyema kuchukua tahadhari mbalimbali zinazoweza kukuepusha na matatizo ambayo hukuiategemea au kushiriki nayo.
1. MAWASILIANO.
Kama tunavyojua kuwa mipango mbalimbali ya kimaisha inapagwa kwa kutumia mawasiliano siku hizi. iwe ni simu, emails au mitandao ya kijamii kwa ujumla. hivyo hata wahalifu nao hutumia mawasiliano ili kupanga uhalifu. hivyo ni vyema kuchukua tahadhari kubwa katika mawasiliano na vifaa vyako vya mawasiliano. kama ifuatavyo.
a) hakikisha unasajiri vifaa vyako kwa taarifa zako mwenyewe.
Usitumie taarifa za mtu mwingine hata mkeo au mumeo. Unaweza tumia taarifaza mtu mwingine bahati mbaya uliyetumia ID zake akawa ni mshiriki au muhusiwa kwa namna moja au nyingine wa ushiriki katika uharifu. pindi inapotokea upelelezi u7nafanyika yaweza jikuta umenasa humo na kukupotezea muda wako kukaa lockups au fedha ili kujinasua. hivyo hata wewe usitoe ID zako kumpa mtu mwingine kusajiria vitu mbalimbali.
b) epuka tabia ya kutumia/kuazimisha simu vifaa vya mawasiliano.
kama ilivyo kanuni ya maisha 'be independent always', ndivyo hata katika jinai inavyoweza kukusaidia. ni nini ninachokisema hapa. unaweza muazimisha mtu simu yako apige au aweke line yake. hapa anaweza mpigia mtu katika mpango wa uhalifu, au ni mtuhumiwa wa uhalifu amabaye polisi wanamtafuta. yaweza kuwa anawasiliana na mtu ambaye atakuja kuuawa au kufanyiwa kosa lolote hii inaweza kukuigiza katika kosa. Yupo diwani mmoja ameuawa kwa kunyweshwa sumu. hivyo upepelezi wako ulihusisha pia watu wote waliopimgia simu week kadhaa kabla, nao hao waliopmpigia waliwasiliana na nani. hii yaweza kukughalimu. ndio maana zikaweza simu za jumuiya. hata ukiwa safarini ni vyema uutumie simu ya kondakta wa basi. hii inaweza kukupa utetezi unaowezakukunasua.
2) MIAMALA YA KIFEDHA.
uhalifu pia unahusisha matumizi ya fedha, mfano ujambazi au mauiji unahusisha manunuzi ya vifaa vya utekelezaji wa matukio hayo. mara nyingi waharifu makini wanaepuka kutumia mawasiliano yataklayo watambulisha. hivyo epuka kuktumia mawasiliano yako katika mialmala ya kifedha ya watu usiowafahamu. zipo tabia mtu anakuomba atumiwe pesa kupitia bank akaunti yako au namba yako ya mpesa-hii yaweza kukugharimu. yupo bwana mdogo mmoja aliingizwa kwenye jinai ya ujambazi, baada ya mtu kufika duka la mpesa na kumuomba huyo dogo amuwekee pesa kwenye namba yake ili atume kwa 'mkewe' kwa kisingizio kuwa yeye hana namba ya Airtel. kumbe mtu aliyemtumia alikuwa ni mpiga katika tukio la ujambazi na lilisababisha mauji. hivyo bwana mdogo alihisiwa yeye ni financer au medium of financing ya mtandao huo. Trust nobody,suspect everybody.
3) NYUMBA ZA WAGENI
wahalifu wengi hutumia nyumba za kulala wageni. wapo matapeli wanaoishi nyumba za wageni kwa muda fulani na kisha kuondoka. sasa hapa huwa kuna mazingira ambayo yanaweza kukuingiza katika matatizo makubwa.
a) Epuka 'guest bubu'.
Mara nyingi wahalifu wanaoperate kificho (anonymously), hivyo hata malazi anatumia yasiyoeleweka. hivyo epuka sana kulala nyumba za wageni zisizoelewa. pia epuka nyumba za wageni zenye sifa zisizo eleweka, za mafichoni, na zenye historia ya uhalifu. ukiwa mgeni eneo fulani jitahidi utumie nyumba za wageni zilizo katika maneno yaliyokaribu na taasis za umma kwani mara nyingi hazitumiwi na waharifu na hazina police-attention.
b) kagua chumba kabla ya kuanza kukitumia.
hili ni jambo la msingi sana. unaweza kuingia chumba ambacho mtu ametoka au hujui nani aliyelala humo au hata mfanya usafi ameacha nini. ni vyema ujenge tabia ya kukagua chumba hasa maeneo ya maficho mfano chini ya uvungu, chini ya godolo., ndani ya fridge, ndani ya kabati na ndani ya bafu. huwezi jua yawezekana kuna kitu kimeachwa humo weweukaitwa muhusika.. zingatia unapofanya ukaguzi huu uwe na muhusika wa vyumba kabla hajakukabidhi. 'mshikwa na ngozi ndio mla nyama'
c) Jisajili kwa 'usahihi'.
hakikisha unajaza taarifa zako pasi na udanganyifu kwenye kitabu cha wageni, kutokujaza kwa ushaihi kunaleta mashaka pindi upelelezi unapofanyika na kubaiinika ulilala hapo na ulidanganya taarifa. Kuna kesi moja ambapo wezi wa magari walilala katika lodge moja huko kahama. bahati mbaya 'bwana mmoja' nae alila lodge hapo na 'mchepuko' a night before na alijaza taarifa za uongo. polisi walipofanya upelelzi wao waligundua ni yeye alyelala pale. hii ilimpa shida hadi kugundulika hausiki kwani kujaza kwake taarifa za uongo kuliwatia mashaka wapelelezi. yawezekana kuwa umeenda na 'mwenza' na usingependa kujulikana basi huyo mwenza ndio ajaze taarifa zake.
4) Sehemu za starehe.
kuwa makini na mazingira haya. nani unakunywa nao, kina nani unanunuliana nao vinywaji. jitahidi kuepuka strangers na kugawa mawasiliano yako pasi na sababu ya msingi.
5) maoni/kauli binafsi.
kauli unayoitamka leo inaweza kutumiwa kama ndio Motive na kuthibitisha Intention yako katika tukio la kesho la jinai. epuka kutoa kauli za vitisho au matamaniko fulani katika hadhari, vijiwe au kwa watu usiowafahamu. inapotokea mikwaruzano jitahidi sana kuepuka kutoa kauli za vitisho,kwani unayemtishia pindi akidhurika wewe ndiye mtuhumiwa namba moja.
6) Jaribu kuwa mdadisi na makini muda wote.
muda wote jihesabu kuwa uko hatarini hivyo jaribu kuwa makini sana na watu wanaokuzunguka. pindi ukihisi kuwa uko karibu na waharifu ondoka katika mazingira hayo. mfn unakuta tukio la ujambazi au mauji ni vyema ukajieupusha kusogelea eneo hilo ikiwa ndio punde limetokea. jipe muda wa 'kutosha' ndio uingie eneo hilo.
Hitimisho. Nimejaribu kueleza mambo haya kwa lengo la kukufanya uishi kwa umakini, kwani hata Inspekta aliimba wanaokwenda jela si wote wana hatia. bahati mbaya sana, mfumo wa utoaji haki, unahususha upelelezi na ushahdidi mahakamani, hivyo inaweza kukugharimu kutokana na ushahdidi wa kimazingira. So be smart and stay free from criminal liability.