PreGE2025 Makalla amtaka Waziri Ulega kusimamia ujenzi wa madaraja kwa ubora

PreGE2025 Makalla amtaka Waziri Ulega kusimamia ujenzi wa madaraja kwa ubora

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi and Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amewasili mkoani Lindi Aprili 10,2025 kwa ajili ya ziara yake katika mikoa miwili ya Lindi na Mtwara.

Awali baada ya kuwasili mkoani humo alipita katika Kata ya Somanga, Mtama iliyopo katika Jimbo la Kilwa Kaskazini mkoani Lindi kwa ajili ya kusalimia wananchi wa eneo hilo.

Aidha, alitembelea Daraja la Somanga Mtama ambalo lilikatika na kupelekea kupotea kwa mawasiliano katika barabara ya Dar es Salaam-Lindi na kuangalia hali inavyoendelea katika daraja hilo.

Akizungumza katika eneo hilo baada ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega kutoa ufafanuzi mfupi Makalla alimpongeza kwa weledi mkubwa aliouonesha kwa kuweza kurudisha mawasiliano hayo kwa muda mfupi na kumtaka aendelee kuwa mkali pale uzembe unapotendeka kwani kile anachokifanya ni kwa maslahi ya CCM kwa sababu wana dhamana kwa wananchi.

Zaidi ya Shilingi bilioni 100 zimetolewa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madaraja hayo, hivyo amemsisitiza Waziri Ulega kuhakikisha anasimamia wakandarasi ili madaraja hayo yajengwe kwa ubora na kwa hadhi inayostahili kwani fedha zipo za kutosha.

 
Back
Top Bottom