Makalla: Asilimia 99.99 ya Malalamiko yaliyotolewa hawahusu utendaji wa Polisi

Makalla: Asilimia 99.99 ya Malalamiko yaliyotolewa hawahusu utendaji wa Polisi

Twilumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
12,576
Reaction score
14,522
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema asilimia 99.99 ya malalamiko yaliyowasilishwa kwake katika kipindi cha kusikiliza kero za wananchi jijini Dar es Salaam siku chache zilizopita hayakuwataja Polisi kama watu wanaosababisha kero jijini Dar es Sallam na hivyo kumshukuru Afande IGP Siro kwa utendaji mzuri wa jeshi analoliongoza.

Amesema hayo wakati wa ufungaji wa kozi Na. 1 ya maafisa wa polisi jijini Dar es salaam leo.

Hata hivyo wakati akihutubia Mh. Rais wa Jamhuri, Samia Suruhu amesema sio kweli kwamba Polisi wanafanya vema kwa asilimia 99.99 kama ambavyo Makalla amemwagia sifa jeshi hilo.

Samia amesema wapo askari ambao wamekuwa wakifanya mambo ya ovyo na kulishushia hadhi jeshi hilo la polisi.

Ametolea mfano yeye akiwa katika ngazi fulani ya uongozi huko nyuma aliwahi kukamatwa na Traffic barabarani kwa kuwa gari yake ilikuwa haiwaki taa moja jambo ambalo amesema lilitokea usiku hu8 na alipojaribu kumweleza traffic husika aligoma kumsikiliza na kueleza kuwa wakati mwingine polisi wanapaswa kutumia akili kwa maana kuwa kama wangemwelewa kuwa tatizo limetokea usiku na wangemsikiliza kuwa aterekebisha kesho yake wanegonekana ni waelewa na wenye weredi maana mambo mengine hutokea kwà dharura.

Akieleza kisa kingine ameeleza kuwa ipo siku alilazimishwa kwenda kituoni kwa kuwa alikutana na gari ya polisi ambayo yenyewe ndiyo iliiingia vibaya barabarani lkn badala yake walimlazimisha aende kituoni akatoe maelezo kwa nn alitaka kuligonga gari la polisi.

My Observations;
1. Makalla acha unafiki, ungeeleza ukweli juu ya malalamiko ya wananchi juu ya polisi khs uinezi, dhuruma etc usingeumbuka kama ambavyo umeonekana wa ovyo mbele ya mteuzi wako.

2. IGP Sirro hiyo ni warning light, kazi kubwa ya ku reform jeshi inatakiwa hasa kuondoa wale wote wenye kufanya jeshi kuonekana la ovyo, mfano kina Afande J4, Kigai, Mahita ambao wameongeza chuki juu ya jeshi hilo kwenye kesi ya mchongo ya ugaidi dhidi ya Mbowe.

3. Waziri Simbachawene, kauli kwamba jeshi halihitaji watu wenye weredi kwa sababu wanalinda benki imezikwa rasmi leo, jitokeze ukiri kuwa ulikengeuka kwa kauli yako kwenye kipindi cha Dak 45 cha ITV.

4. Mh. Rais ana nia njema kureform jeshi kuwa lenye weredi na ambalo litafabya kazi bila uonezi ila waziri na IGP ndio wana shingo ngumu kwendana na tune ya Mh. Rais. Mjitathimini Mh. Waziri na IGP naona bado mpo na dhana ya kumwaga sifa za kinafki Mama hapendi unafiki wenu huo
 
Makalla - alikuwepo Makonda; yupo Wapi ? Kama kuna mtu mzuri kumshauri Makalla ni Makonda!
 
Back
Top Bottom