Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Wakati uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa wanaotaka kugombea ubunge na udiwani, ukianza leo Jumamosi, Juni 28, 2025 kwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), harufu ya mchezo mchafu imeanza kusikika.
Imeelezwa kuwa baadhi ya wagombea wanaokwenda kwenye ofisi za CCM kwa ajili ya kuchukua fomu wamekuwa wakitozwa zaidi ya viwango vilivyowekwa na chama hicho.
Viwango vya fomu vilivyopangwa ni Sh500,000 kwa nafasi ya ubunge na Sh50,000 kwa madiwani, lakini tayari yamesikika malalamiko ya baadhi ya wagombea kutozwa zaidi.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla leo Jumamosi, Juni 28, 2025 amewaonya watendaji wenye tabia hiyo kuacha mara moja. Amesema kuna taarifa za baadhi ya watendaji kuwatoza wanachama fedha zaidi ya kiwango kilichoweka cha ada ya fomu.