Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka watanzania kusimama na Rais Samia Suluhu Hassan katika kulinda amani iliyopo nchini kwani Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine.
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla alieleza hayo wakati akizungumza na wananchi katika Wilaya ya Ubungo Dar es salaam akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani humo.
Aidha, Makalla amesisitiza hakuna Tanzania nyingine mbadala na kwa kulitambua hilo kuelekea katika kipindi cha uchaguzi na wakati uchaguzi ukiendelea wanasiasa watapishana kwa itikada lakini wakiendela kulinda amani.
Ameongeza wanasiasa wanatakiwa kuja na hoja watakazoziwasilisha na kuzinadi kwa wananchi na katika wakati wa uchaguzi wananchi ndo wataamua chama gani wakichague na baada ya uchaguzi atakayeshinda atatangazwa kuwa mshindi na kupewa ridhaa ya kuongoza.
Pia Makalla amesema amefurahishwa na hotuba ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi wa dini zote kwa kuhubiri amani wakionesha imani yao juu ya uchaguzi, kwani upo kwa mujibu wa katiba na CCM watafanya kama walivyoeleza ili kulinda amani.