LGE2024 Makalla: CCM tumeweka mapingamizi, tunaamini haki itatendeka

LGE2024 Makalla: CCM tumeweka mapingamizi, tunaamini haki itatendeka

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Ni mwendo wa maigizo tu mpaka kieleweke.

=====

Screenshot_20241111_193035_Instagram.jpg


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, amewaomba wanachama katika maeneo ambayo wagombea wa CCM wamewekewa mapingamizi, kuwa watulivu kwani Chama kinaamini haki itatendeka kwa vyama vyote.

CPA Makalla aliyasema hayo leo wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, ambapo amesisitiza CCM kitaibuka na ushindi wa haki katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

“Niwaombe wanaCCM, tupo katika hatua za mapingamizi. Sasa hivi kinachoendelea mitandaoni ni malalamiko ya vyama vya upinzani kuonyesha kama vile pekee ndiyo waliowekewa mapingamizi.

Screenshot_20241111_193022_Instagram.jpg


“Wanafanya hadaa, upotoshaji wa takwimu feki na kujisahaulisha kwamba hata wagombea wa CCM wamewekewa mapingamizi. Juzi nilisema tunaamini TAMISEMI itatenda haki kwa vyama vyote kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki na atakayeshinda atangazwe kwa haki,” alisema Makalla na kusisitiza:

“Kwa hesabu zetu na wagombea tuliowaweka, tunaamini CCM tutashinda kwa haki. Kwa hiyo rufaa zinaendelea, baada ya uteuzi wa wagombea CCM kitatoa taarifa baadaye.”

CPA Makalla alikemea tabia hiyo ya baadhi ya vyama vya upinzani kupotosha umma kwamba wagombea wa vyama hivyo pekee, ndiyo wamewekewa mapingamizi, wakati si kweli.

Alisema kuwa vyama vyote, kikiwemo CCM, ambavyo wagombea wake wamewekewa mapingamizi ya kuteuliwa, vinaendelea kukata rufaa, kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa.

“Niwaombe wanaCCM katika maeneo ambayo tumewekewa mapingamizi, tuwe watulivu tukiamini haki itatendeka kwa vyama vyote,” alisisitiza CPA Makalla.
 
Ni muhimu sana haki ikatendeka kwa wasiostahili kuenguliwa na wanaostahili wakapewa nafasi 🐒
 
Mimi nashauri haki itendeke, tunakoenda baada ya kufa ni kuzito sana , na kila mmoja atamlaumu mwenziwe kwa wenye kudhulumu
 
Ipo siku si mbali tutaelewana....furahieni ukaburu wenu kwa sasa
 
Wenzake wanalalamika Kwa takwimu, yeye porojo, je nani aaminiwe?
Je kuna sehemu wagombea wake karibia wote wameenguliwa?
 
Huo siyo ushindi bali ni ubakaji na punyeto ya kisiasa,kama nyie wanaume kweli wekeni uwanja sawa wapiga kura ndiyo watoe hukumu.

Ila huu ushenzi mnaofanya utakuja kula kwenu,siku kikinuka hadi vijukuu vyenu havitabaki salama kwani ndiyo aina ya siasa mliyoichagua. Lazima tutakuja kulipa kisasi tu.
 
..mapingamizi ya nini tena?

..tunajenga utamaduni wa kutaka kushinda uchaguzi kwa njia za hila.
 
Hayo ndio maneno yako?Sasa na utuambie hivyo vikapu ndio vya kwenda kubebea nini?
kuzingatia kanuni, taratibu na sheria ndilo muhimu zaidi kulikoni mihemko na makasiriko kwa wagombea na vyama vyao gentleman 🐒
 
Back
Top Bottom