PreGE2025 Makalla: CHADEMA wameogopa kuingiza timu uwanjani uchaguzi mkuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Katibu wa NEC anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla, ameielezea CHADEMA kuwa haina dira ya kisera inayoweza kuwasaidia wananchi, zaidi ya kutegemea maneno na misaada ya kifedha kutoka kwa wanachama wake.

Akihutubia mkutano wa hadhara Aprili 13, 2025, huko Lindi Mjini, Makalla aliwataka wananchi waendelee kuiamini CCM, akisisitiza kuwa ndicho chama chenye mwelekeo wa maendeleo ya kweli kwa Watanzania.

Alieleza kuwa vyama vya upinzani vimepoteza dira, akivitaja CUF na ACT Wazalendo kuwa katika hali ya kusuasua, huku akidai CHADEMA wameamua kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu 2025 kwa kile alichokieleza kuwa ni kushindwa kuhimili kasi ya utekelezaji wa serikali ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Makalla alisisitiza kuwa CHADEMA walijiridhisha kuwa hawana nafasi ya kushinda kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na serikali, hivyo wakaamua kutoshiriki uchaguzi huo.

“CHADEMA wamepimaa, wamechungulia, wameona kazi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, wakatambua hawana ushindi, wakaamua kupumzika. Hawatakuwepo kwenye uchaguzi. CCM oyee!”
 
Kauli ya CPA Amos Makalla siyo tu ya kipropaganda, bali pia ni ushahidi wa wazi wa hofu inayozidi kuenea ndani ya CCM dhidi ya nguvu ya kisiasa inayozidi kukua kwa kasi: CHADEMA.

Kwanza kabisa, kusema kwamba CHADEMA “haina dira ya kisera” ni utani wa kisiasa usio na msingi. Mwaka 2020, CHADEMA iliwasilisha ilani ya uchaguzi iliyojikita kwenye ajenda za kitaifa: uchumi shirikishi, uhuru wa vyombo vya habari, haki za binadamu, mapambano dhidi ya rushwa kwa vitendo (siyo maneno), na elimu bora isiyobagua. Kama Makalla hajui hilo, basi labda hakuisoma. Kama aliisoma na bado anasema hakuna dira, basi anadhani Watanzania wote hawasomi. Lakini kizazi hiki kimeamka.

Pili, hoja kwamba CHADEMA inategemea "misaada ya wanachama wake" ni hoja ya kushangaza. Je, si hiyo ndiyo demokrasia ya kweli? Chama kinachotegemea nguvu ya watu — si fedha za serikali wala makampuni ya kivuli — ni chama kilicho huru. Kinachotegemea “misaada ya wanachama” kinajenga uaminifu. Kwa kifupi: CHADEMA haitegemei mafungu ya Ikulu — inategemea sauti ya wananchi.

Tatu, madai kwamba CHADEMA imesusa uchaguzi kwa sababu “imeona haitashinda” ni kejeli ya kifisadi. CHADEMA haijawahi kuogopa kushindana — inaogopa kushiriki mchezo wa maigizo. Uchaguzi usio huru na wa haki si uchaguzi, ni sarakasi. CHADEMA haijasusia uchaguzi, imekataa kuhalalisha uozo. Ni ujasiri, siyo uoga. Na kama CCM ina uhakika inaungwa mkono kweli, ifanye kazi moja rahisin sana: Bunge la sasa liofanye minimum reform under certificate of urgency na iruhusu tume huru ya uchaguzi. Period.

Alichosema Makalla kuhusu vyama vya upinzani “kusuasua” ni zaidi ya kejeli — ni dalili ya mfumo wa vyama vingi kuvunjwa kwa makusudi na chama tawala. Huwezi kupora haki, kunyima usajili wa mikutano, kuwatia viongozi rumande, halafu useme chama kimesuasua. Hiyo siyo siasa — hiyo ni hujuma.

Mwisho, kama kazi za Rais Samia ni nzuri kiasi hicho hadi “CHADEMA wakaamua kupumzika”, basi kwa nini CCM inaogopa kushindana nao katika uchaguzi huru? Huwezi kuwa bingwa wa mbio za mita 100 huku umefungia washindani miguu.

Kwa kifupi:

➡ CHADEMA ina dira — na ni tishio kwa mfumo wa kifisadi.
➡ Kusema wanategemea misaada ni ushahidi wa chama kinachojengwa na wananchi, si dola.
➡Kutoruhusu uchaguzi huru si ushindi wa CCM — ni udhaifu uliofungwa kwa bendera ya propaganda.
➡ Kauli ya Makalla ni sawa na kuku kujisifu mbele ya mbuni aliyezibwa macho — ni kelele zisizo na ushindi wa kweli.

Watanzania hawadanganyiki tena. Mabadiliko hayazuiliki kwa propaganda — yanaahirishwa kwa gharama.
 
So alitaka wasign kukubali haramu? Si wamepata ushindi wa mama kupita bila kupingwa why wanamtajataja huyu mwanaume wandugu? Yupo jela lakini watu wanateseka uraiani!
 
Yani referee wa mechi mumchague nyie utegemee fair result kweli,CHADEMA wapo sahihi.
 
Yani Chadema bado mnaiongelea pamoja na kutokushiriki..!!

Kweli Chadema wamewashika pabaya, mnaacha kuwaonyesha wananchi mlichofanya mnawashwa washwa na mwanaume aliyeawaacha..!! Hebu mjitahidi kumove on basii km mmedoda si muende kwa chauma..!! 😹😹😹
 
Kauli ya CPA Amos Makalla siyo tu ya kipropaganda, bali pia ni ushahidi wa wazi wa hofu inayozidi kuenea ndani ya CCM dhidi ya nguvu ya kisiasa inayozidi kukua kwa kasi: CHADEMA.

Kwanza kabisa, kusema kwamba CHADEMA “haina dira ya kisera” ni utani wa kisiasa usio na msingi. Mwaka 2020, CHADEMA iliwasilisha ilani ya uchaguzi iliyojikita kwenye ajenda za kitaifa: uchumi shirikishi, uhuru wa vyombo vya habari, haki za binadamu, mapambano dhidi ya rushwa kwa vitendo (siyo maneno), na elimu bora isiyobagua. Kama Makalla hajui hilo, basi labda hakuisoma. Kama aliisoma na bado anasema hakuna dira, basi anadhani Watanzania wote hawasomi. Lakini kizazi hiki kimeamka.

Pili, hoja kwamba CHADEMA inategemea "misaada ya wanachama wake" ni hoja ya kushangaza. Je, si hiyo ndiyo demokrasia ya kweli? Chama kinachotegemea nguvu ya watu — si fedha za serikali wala makampuni ya kivuli — ni chama kilicho huru. Kinachotegemea “misaada ya wanachama” kinajenga uaminifu. Kwa kifupi: CHADEMA haitegemei mafungu ya Ikulu — inategemea sauti ya wananchi.

Tatu, madai kwamba CHADEMA imesusa uchaguzi kwa sababu “imeona haitashinda” ni kejeli ya kifisadi. CHADEMA haijawahi kuogopa kushindana — inaogopa kushiriki mchezo wa maigizo. Uchaguzi usio huru na wa haki si uchaguzi, ni sarakasi. CHADEMA haijasusia uchaguzi, imekataa kuhalalisha uozo. Ni ujasiri, siyo uoga. Na kama CCM ina uhakika inaungwa mkono kweli, ifanye kazi moja rahisin sana: Bunge la sasa liofanye minimum reform under certificate of urgency na iruhusu tume huru ya uchaguzi. Period.

Alichosema Makalla kuhusu vyama vya upinzani “kusuasua” ni zaidi ya kejeli — ni dalili ya mfumo wa vyama vingi kuvunjwa kwa makusudi na chama tawala. Huwezi kupora haki, kunyima usajili wa mikutano, kuwatia viongozi rumande, halafu useme chama kimesuasua. Hiyo siyo siasa — hiyo ni hujuma.

Mwisho, kama kazi za Rais Samia ni nzuri kiasi hicho hadi “CHADEMA wakaamua kupumzika”, basi kwa nini CCM inaogopa kushindana nao katika uchaguzi huru? Huwezi kuwa bingwa wa mbio za mita 100 huku umefungia washindani miguu.

Kwa kifupi:

➡ CHADEMA ina dira — na ni tishio kwa mfumo wa kifisadi.
➡ Kusema wanategemea misaada ni ushahidi wa chama kinachojengwa na wananchi, si dola.
➡Kutoruhusu uchaguzi huru si ushindi wa CCM — ni udhaifu uliofungwa kwa bendera ya propaganda.
➡ Kauli ya Makalla ni sawa na kuku kujisifu mbele ya mbuni aliyezibwa macho — ni kelele zisizo na ushindi wa kweli.

Watanzania hawadanganyiki tena. Mabadiliko hayazuiliki kwa propaganda — yanaahirishwa kwa gharama.
Yaani wananchi wanaotakiwa wao ndio wapelekewe misaada na vyama vya siasa, inakuwa vise versa halafu unasema wanajenga uaminifu kwa njia hii? Tuwaonee huruma jamani.
 
Katibu wa NEC anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla, ameielezea CHADEMA kuwa haina dira ya kisera inayoweza kuwasaidia wananchi, zaidi ya kutegemea maneno na misaada ya kifedha kutoka kwa wanachama wake.

Akihutubia mkutano wa hadhara Aprili 13, 2025, huko Lindi Mjini, Makalla aliwataka wananchi waendelee kuiamini CCM, akisisitiza kuwa ndicho chama chenye mwelekeo wa maendeleo ya kweli kwa Watanzania.

Alieleza kuwa vyama vya upinzani vimepoteza dira, akivitaja CUF na ACT Wazalendo kuwa katika hali ya kusuasua, huku akidai CHADEMA wameamua kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu 2025 kwa kile alichokieleza kuwa ni kushindwa kuhimili kasi ya utekelezaji wa serikali ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Makalla alisisitiza kuwa CHADEMA walijiridhisha kuwa hawana nafasi ya kushinda kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na serikali, hivyo wakaamua kutoshiriki uchaguzi huo.

“CHADEMA wamepimaa, wamechungulia, wameona kazi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, wakatambua hawana ushindi, wakaamua kupumzika. Hawatakuwepo kwenye uchaguzi. CCM oyee!”
Muulize vile virusi vya EBOLA na MPOX Vinauzwa duka gani na je chadema bado wanampqngo wa kuviingiza ?
Jamaa mjinga huyu malkala
 
Kila mara chadema chadema kama hana cha kusema si akae kimya maana wanadai imekufa sasa kinachowa washa ni nini na wamepewa ushindi bure
 
So alitaka wasign kukubali haramu? Si wamepata ushindi wa mama kupita bila kupingwa why wanamtajataja huyu mwanaume wandugu? Yupo jela lakini watu wanateseka uraiani!
Ndiyo maana tunasema: ukinyamazisha sauti ya haki gerezani, usitarajie amani uraiani.

Unasema “alitaka wasign kukubali haramu” — lakini hukusema ni nani aliyefanya hiyo haramu. Na kwa nini haramu ikalindwa kwa wino badala ya kuanikwa hadharani? Kama kulikuwa na haramu, basi walioiandaa, kuisimamia, na kuilazimisha wapinzani waikubali ndio wa kulaumiwa — si aliyeikataa kwa ujasiri.

Na kuhusu mama “kupita bila kupingwa” — hiyo siyo sifa, ni aibu ya kisiasa kwa taifa linalojiita la kidemokrasia. Rais wa nchi kupita bila kupingwa si kwa sababu wananchi hawakuwa na chaguo jingine, bali kwa sababu chaguzi zimegeuzwa maonyesho ya upande mmoja. Huo si ushindi, ni ushindwa wa mfumo wa haki.

Halafu mnasema “mtu yupo jela lakini watu wanateseka uraiani” — ni kweli. Lakini swali ni hili: je, mateso haya yamesababishwa na Lissu akiwa jela, au na mfumo mnaouhifadhi kwa nguvu ya matusi na kejeli badala ya hoja? Unapomfungia mpinzani kwa sababu ya sauti yake, alafu taifa likaendelea kutaabika — hiyo ni ishara kwamba shida si mpinzani, bali mfumo mzima.

Kama kweli Lissu hana maana yoyote, mbona kila siku wanamtaja? Kama amesahaulika, kwa nini bado anawatesa kwenye majukwaa bila hata kuwepo? Jibu ni moja: kweli ina nguvu, hata ikifungiwa. Na hofu ya mnyanyasaji huwa kubwa kuliko ukimya wa mnyanyaswaji.

Kwa hiyo, badala ya kuwashangaa wanaoteseka uraiani huku Lissu yupo gerezani, jiulize ni kwa nini watawala walio huru ndio chanzo cha mateso hayo.

Na mwisho, mtu mwenye kosa haogopi uchaguzi — anaogopa haki. Kwa nini serikali ya ccm inaogopa kutenda haki ktk uchaguzi?
 
Yanini kupoteza muda kushiriki uchaguzi haramu kama chaguzi za hapa nchini zilizojaa wizi wa kura na upangaji wa matokeo, ni upotezaji wa muda na rasilimali na ni mwendawazimu pekee anayeweza kushiriki uchaguzi huu
 
Katibu wa NEC anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla, ameielezea CHADEMA kuwa haina dira ya kisera inayoweza kuwasaidia wananchi, zaidi ya kutegemea maneno na misaada ya kifedha kutoka kwa wanachama wake.

Akihutubia mkutano wa hadhara Aprili 13, 2025, huko Lindi Mjini, Makalla aliwataka wananchi waendelee kuiamini CCM, akisisitiza kuwa ndicho chama chenye mwelekeo wa maendeleo ya kweli kwa Watanzania.

Alieleza kuwa vyama vya upinzani vimepoteza dira, akivitaja CUF na ACT Wazalendo kuwa katika hali ya kusuasua, huku akidai CHADEMA wameamua kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu 2025 kwa kile alichokieleza kuwa ni kushindwa kuhimili kasi ya utekelezaji wa serikali ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Makalla alisisitiza kuwa CHADEMA walijiridhisha kuwa hawana nafasi ya kushinda kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na serikali, hivyo wakaamua kutoshiriki uchaguzi huo.

“CHADEMA wamepimaa, wamechungulia, wameona kazi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, wakatambua hawana ushindi, wakaamua kupumzika. Hawatakuwepo kwenye uchaguzi. CCM oyee!”
 
Attachments

  • cf0ea736521de32f5d65e1a6b7fd56a4_1743187151179.mp4
    579.6 KB
Back
Top Bottom