Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, amewahakikishia wazee na wananchi wa mkoa huo kuwa serikali imejipanga vizuri kuhakikisha kuwa siku ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, itafanyika katika mazingira ya amani, utulivu na usalama kwa kila mwananchi.
“Kupiga kura ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania. Wazee wangu, mtukumbushe na muwakumbushe vijana kuhusu umuhimu wa kuitunza amani, kutumia mitandao ya kijamii kwa busara, na kujitokeza kwa wingi kupiga kura. Niahidi, kila mmoja atapiga kura kwa amani, na atakayeshinda atatangazwa kwa haki,” amesema CPA Makalla.