PreGE2025 Makalla: Kukamilika kwa SGR ni matokeo ya Utawala bora wa CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla, amesema kukamilika kwa miradi mikubwa ya kimkakati nchini, ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR), ni matokeo ya sera madhubuti na mipango thabiti ya CCM inayolenga kuwaletea maendeleo Watanzania.

​
CPA Makalla ametoa kauli hiyo mara baada ya kuwasili mkoani Morogoro leo kwa kutumia usafiri wa Treni ya SGR, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku saba mkoani humo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Katika ziara hiyo, CPA Makalla anatarajiwa kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kukutana na wanachama, viongozi wa chama, pamoja na kushiriki mikutano ya hadhara. Aidha, ataangazia namna chama kinavyotekeleza miradi ya maendeleo kwa vitendo kwa kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Makalla amewataka Watanzania kuendelea kuiamini CCM, akisisitiza kuwa maendeleo yanayoonekana nchini hivi sasa ni uthibitisho wa uongozi bora na utekelezaji wa ahadi kwa wananchi.
 
Mwambieni tunasubiri majibu . Vile viruses vya ebola na mpox vimeshaletwa????
 
Ni aibu kwa ccm yenye umri zaidi ya miaka 48 kuogopa uchaguzi wa huru, haki na kweli.
 
Ni aibu kwa ccm yenye umri zaidi ya miaka 48 kuogopa uchaguzi wa huru, haki na kweli.
Hawawezi hawajiamini . Ukiwatajia uchaguzi huru na wa haki wanakimbilia kwa wauaji kina TISS na MURILO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…