LGE2024 Makalla: Rais Samia ameleta hamasa kubwa kwa wananchi kujiandikisha kwa wingi uchaguzi wa Serikali za mitaa

LGE2024 Makalla: Rais Samia ameleta hamasa kubwa kwa wananchi kujiandikisha kwa wingi uchaguzi wa Serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Imeelezwa kuwa kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan, na viongozi wengine wa CCM wa ngazi mbalimbali kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la mkazi kimekuwa chachu ya wananchi kushiriki kwa wingi kwenye zoezi hilo

Mlezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Makala ameeleza hayo wakati wa hafla ya kupokea taarifa ya zoezi la uandikishaji wa daftari la mkazi la uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mkoa wa Dar es Salaam, taarifa aliyoipokea kutoka kwa viongozi wa CCM wa mkoa huo leo, Jumanne Oktoba 22.2024

Soma Pia: Makalla: Inashangaza kuona viongozi waandamizi wa vyama vya siasa hawajajiandikisha uchaguzi wa Serikali za mitaa

Amesema viongozi mbalimbali wa CCM kuanzia kwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Katibu Mkuu Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Wajumbe wa Kamati Kuu, Wajumbe wa sekretarieti, Wajumbe wa Halmashauri Mkuu, Viongozi wa mikoa, wilaya nk wote kwa namna moja au nyingine wameshiriki kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi hilo, sambamba na wao wenyewe kuwa mstari wa mbele kujiandikisha jambo ambalo limetengeneza hamasa kubwa kwa wananchi nao kushiriki kwa wingi wao
 
Back
Top Bottom