PreGE2025 Makalla: Tumepokea ushauri lakini CCM hatuna mgogoro na CHADEMA, Jaji Warioba akasuluhishe mgogoro wa CHADEMA

PreGE2025 Makalla: Tumepokea ushauri lakini CCM hatuna mgogoro na CHADEMA, Jaji Warioba akasuluhishe mgogoro wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Askari wasiishie kupima ulevi kwa madereva barabarani,

Wanasiasa pia wapimwe ulevi wapandapo na washukapo majukwaa ya kisiasa.
Maaskari wenyewe wanastahiki kupimwa!
Kifupi Makalla hana busara! Anachochea uovu, dhuluma na ukiukaji mkubwa wa HAKI!
 
CCM mwambieni Makala Mzee Warioba sio level yake kabisaa...
Ni bora akaacha haya mambo yampite....
Wenye hekima naamini wapo wataangalia namna ya kudeal na haya mambo...
Ni hivi atulie tuliii hana hiyo IQ na reputation ya kubishana na huyu Mzee...
CCM ni kubwa sana!
ccm haijawahi kuwaheshimu wazee.
 
Kwani warioba alishauri serikali ikae na CHADEMA au ccm ndio ikae na CHEDEMA?
 
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakina mgogoro na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kumwomba Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba kuwa msuluhishi wa yanayoendelea ndani ya chama hicho cha upinzani.


Amesema Mzee Warioba anao uwezo wa kumaliza mgogoro ndani ya CHADEMA na kwamba, CCM ikisikia kama kuna mchango unahitajika watasaidia ili chama hicho warudi kuwa wamoja kwa sababu kwa sasa inasikitisha.

Mwishoni mwa wiki, Jaji Warioba alishauri serikali na CHADEMA kukaa meza ya moja ha mazungumzo ili kupata muafaka wa amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Akizungumza leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mikese, mkoani humo ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara yake ya siku saba, Makalla amesema CCM inaheshimu ushauri wa Jaji Warioba aliotoa mwishoni mwa wiki, na kueleza kuwa CCM ina uhusiano mzuri na CHADEMA.

Makalla amesema juzi amemsikiliza Jaji Warioba ambaye wanamheshimu amekuwa Waziri Mkuu na mbobezi wa mambo ya uongozi na mwanasheria nguli na mwenye mchango katika taifa.

"Anaheshimika ni miongoni mwa wazee ambao tuko nao na wakati wote tutaendelea kuheshimu michango yao, nimemsikia akieleza, akitoa ushauri kwamba CCM wakae CHADEMA wamalize mgogoro kisiasa.

"Kama nilivyosema tunamheshimu, ametoa ushauri mzuri wa sisi kukaa na CHADEMA kuongelea mgogoro wa kisiasa.

Chanzo: Nipashe
Vinakula mpaka nywele zinanenepa!
 
Maaskari wenyewe wanastahiki kupimwa!
Kifupi Makalla hana busara! Anachochea uovu, dhuluma na ukiukaji mkubwa wa HAKI!


Makalla ni miongoni mwa watu walioenda shuleni kukariri, LAKINI kiuhalisia huyu Makalla hana akili yenye uwezo wa kufanya tafakuri. Huyu ni wa kumpuuza kama tunavyowapuuza wendawazimu wengine.
 
Back
Top Bottom