Mimi nimejionea namna wapinzani na upinzani ulivyojikatia tamaa na kupoteza matumaini kabisa.viongozi wa upinzani wapo kama hawapo vile.hawana ushawishi wala sera wala ajenda wala hoja zenye kugusa Maisha ya watu.Maeneo mengi sana hawajaweka wagombea na wengi hawakuchukua Fomu kwa hofu na uoga wakukataliwa..
Ninyi hamuwezi mkajiuliza inakuwaje viongozi wa ngazi za juu wa upinzani kama Lissu wanakimbia kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura? Sasa hamuoni ni ile hali ya kukata tamaa? Sasa kama wao tu viongozi hawajajiandikisha wanataka nani ajiandikishe na kuwapigia kura? Kama wao tu hawapo kwenye daftari la mpiga kura wanataka nani awepo na awape kura?
Na hivyo naweza kusema kuwa CCM itapita na kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Nchi Nzima