Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinatarajia kuwatambulisha kwa Wanachama Wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 katika maadhimisho ya miaka 48 ya Chama hicho February 05,2025, uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Taarifa ya kuelekea maadhimisho hayo iimetolewa na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa,Itikadi,Uenezi na Mafunzo CPA. Amos Makalla ambapo amesema sherehe hizo zitakuwa na matukio mbalimbali ikiwemo hilo la utambulisho.
Ikumbukwe hivi karibuni Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho wa January 18 na 19,2025 ulipitisha majina ya Dkt. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mgombea Urais na Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea mwenza kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Hussein Ally Mwinyi kuwa Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Soma, Pia: Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025