Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kuwa mwalimu wa vyama vingine ili waendelee kujifunza kwao.
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, CPA Amos Makalla, ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Bukoba Mjini, mkoani Kagera, katika ziara yake ya siku saba aliyoianza ikihusisha pia, mikoa mingine ya Geita, Mwanza na Simiyu
"Nilisikia mtani wangu (John) Heche, Makamu Mwenyekiti CHADEMA amesimama hapa alivyopita na Shinyanga na kwingine kuwahadaa Watanzania wakishika nchi watamlipa kila Mtanzania pensheni.
"Nikajiuliza maswali mawili, huyu mtani wangu amechanganyikiwa, wewe si umesema huendi kwenye uchaguzi, utashikaje nchi, nahisi anaota"-Amos Makalla
Source: Nipashe