Makamanda wa Hamas na Hizbullah waache kutumia simu za satellite za Ellon Musk

Makamanda wa Hamas na Hizbullah waache kutumia simu za satellite za Ellon Musk

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kufuatia minara yote ya simu na vinu vya umeme kubomolewa huko Gaza,Ellon Musk kwa kile kilichoonekana malengo ya kibiashara alisema ataunganisha jimbo hilo na mtandao wake wa mawasiliano wa star link.Israel ikamshutumu sana na yeye akarudi nyuma.

Hata hivyo watu wenye ndugu zao nje huko Gaza wameweza kuunganishwa na mfumo wa simu za satellite na ndio maana habari kutoka Gaza pamoja na uharibifu wote uliofanywa bado hazijasimama.

Kilichofanyiko ni simu zile zile za zamani walizonazo watu wa Gaza wanapokea line za simu za kielektronik na kuziingiza kwenye simu zao wanazozichaji kwa nguvu ya jua.Baada ya hapo wanapokea vifurushi kutoka kwa wahisani kwa njia hizo hizo za satellite.

Mfumo huo wa mawasiliano unaonekana umefadhiliwa na kwa watu muhimu wa Gaza wakiwemo viongozi na makamanda wakuu wa makundi hayo baada ya mfumo wa nyaya walizokuwa wakitumia bila kugundulika nao kuvunjwa katika vita hivyo.

Ellon Musk hivi karibuni alitembelea Israel na kujifakharisha kwamba yeye ana asili za kiyahudi.Kuna uwezekano mkubwa kuwa katika ziara yake hiyo ambapo alikutana na viongozi wa kiserikali alipokea jukumu la kufanikisha kuwatambua makamanda wa Hamas wapi walipo.

Watu wa Gaza wanapopokea line zinazolipiwa kwa crypto currency wengi wao hawajui kwa uhakika line hizo wamepatiwa na nani au ndugu yao aliyewapatia alishirikiana nani katika kufanikisha mawasiliano.

Katika siku za karibuni na tangu Ellon Musk atembelee Israel inaonekana kasi ya kuuliwa viongozi wa Hamas na makundi mengine ya wapiganaji imeongezeka sana.

Kwa mara ya mwanzo mfumo huo wa kupeleka laini za satellite Gaza ulifanikishwa na mwanaharakati wa kike ndani ya Misri.

Hivyo mbali na Ellon Musk na kwa Inavyojuliakana ilivyo Misri katika ushirika na Israel ni wazi kuwa itakuwa ni mlango wa pili mwepesi kwa Israel kunasa mawasiliano yote na makamanda walioko Gaza au Lebanon.
 
Basi wasitumie kabisa simu ili wage na njaa maana hawana Kila kitu kwa Sasa.
 
Hata wakitumia sasa wawasiliane vipi hamna mbadala acha kipigwe zayuni apate hata camera inayomuonesha kila kitu ila asahau hawa jamaa kurudi nyuma
Hiki kitanzi tayari kimeshanasa kwa yahudi
 
Hata wakitumia sasa wawasiliane vipi hamna mbadala acha kipigwe zayuni apate hata camera inayomuonesha kila kitu ila asahau hawa jamaa kurudi nyuma
Hiki kitanzi tayari kimeshanasa kwa yahudi
KIMENASA
 
IRAN NI WATU WABAYA SANA. WALIWADANGANYA HAMAS KUVAMIA ISRAEL OCTOBA 7 SASA GAZA YOTE IMEBAKI MAGOFU!.

NETANYAHAU KAZI IENDELEE!
 
IRAN NI WATU WABAYA SANA. WALIWADANGANYA HAMAS KUVAMIA ISRAEL OCTOBA 7 SASA GAZA YOTE IMEBAKI MAGOFU!.

NETANYAHAU KAZI IENDELEE!
Kasababisha mayahudi wote nao wanajificha ndani ya mahandaki na majumba yamehamwa kabla kugeuka magofu.Wengine wamejaa uwanja wa ndege wanakimbia nchi.
 
Back
Top Bottom