Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Mimi ni muumini wa kitu kinachoitwa "Karma", na nimekuwa nikikihubiri mara nyingi tuu humu jukwaani kuwa karma ndio the power pekee ambayo hutoa hukumu ya haki hapa duniani, kwenye karma, mtu unaadhibiwa au kuhukumiwa kwa mawazo, maneno na matendo yako, karma haina mswalie Mtume, wala haujui nani ni nani!, kwenye hukumu ya karma, inatembeza bakra za kutosha na adhabu kubwa ya mwisho ya karma huwa ni kula kichwa!. "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Leo kikao cha CC ya Chadema, kinakaa as usual, kama kawaida yao, kikao hiki huwa kinakaa as a Kangaroo court!, kama kilivyokuwa kinakaa huko nyuma na kutoa hukumu za kikangaroo za ajabu ajubu ikiwemo timua timua, ambazo karma za hukumu hizo, zinakuja kuigharimu Chadema mbele ya safari, tatizo, wakati wa karma payback time unapofika, when karma strikes back,
no one remembers, hakuna anayekumbuka kuwa kinachotokea ni hukumu ya Karma ya matendo yake ya nyuma!. Tatizo la karma, unaweza kufanya kitu kidogo, tuu, kwako ukakiona ni kidogo, it's nothing and insignificant, lakini when karma takes its toll, mapigo ya karma yanayokushukia ni mapigo makubwa in three folds, kulinganisha na ulichotenda, hadi huwezi kukumbuka ulifanya nini kustahili kinachokupata!. Ila pia, anayehukumiwa pasipo haki, karma pia huwa ina mtake care, na kumu elevate kwa kumuweka mahali pa juu palipoinuka, machoni pa watesi wake!.

Mifano michache ya baadhi ya Matendo ya Chadema, na Matokeo ya Karma Zake.
  1. Chadema walipo establish a torture chamber pale makao makuu yake na kumshughulikia ipasavyo Mlinzi wa Dr. Slaa, Kagenzi, nilionya kuhusu karma. Kwa vile hii ilikuwa ni internal operation, na mimi sio inside man wa Chadema, naombeni ndugu zangu wa Chadema, jifanyieni tathmini, nani alifanya nini, the roles walizo play, then angalia kilichokuja kuwakuta the players, na sasa Kagenzi yuko wapi na ana hali gani!. Bodigadi wa zamani wa Dr. Slaa, Khalid Kagenzi akanusha kutaka kumuua Dr. Slaa, Ya mke wa Slaa na Mlinzi binafsi wa Dk. Slaa, Tena tazameni karma ilivyo, aliyetuhumiwa kumpa sumu Kagenzi ili amtilie Dr. Slaa, na yeye alikuja kutiliwa sumu na ikamwingia na kumdhuri, tena alikuwa ni almanusura!, asingewahishwa saa hizi tungekuwa tunazungumza mengine!.
  2. Chadema mlipokuwa kwenye kikao chenu cha ndani, CC Arusha, kukatokea mtu miongoni mwenu aliyekuwa akivujisha jf, kilichokuwa kinajadiliwa ndani, mlimuita msaliti, kwa kuvujisha info humu JF, jiulizeni ni nani alimdakua mtu huyo, na mlimfanya nini!, then jikumbumbusheni kilichompata huyo kamanda shupavu aliyemshughulikia msaliti!. Kinachoendelea CHADEMA Mitandaoni: Je, ni Ushujaa wa Mhe. Lema au ni Udhaifu wa "Kule Juu"?
  3. Chadema mlipomtimua Juliana Shonza na masalia kwenye kangaroo court yenu, nililizungumzia hili, sasa leo angalieni waliomshughulikia Shonza, nini kiliwakuta, leo wako wapi, na mlinganishe na Juliana Shonza alipo!. Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!
  4. Mlipowatimua kina Kitila kwa hoja ya ule Waraka wa Mabadiliko, ambao nyinyi mliuita ni waraka wa mapinduzi, mimi nikawaambie ule ni waraka wa kui transform Chadema kutoka Chama cha kiharakati, kukigeuza Chama Tawala in waiting, hivyo waraka ule haukuwa wa mapinduzi, bali a "winning coalition" kuu revamp uongozi static na stagnant wa Chadema, na kuleta uongozi mpya vibrant na dynamic, angalieni makamanda wa timua timua hiyo nini kiliwakuta, linganisha na mahali alipo Prof. Kitila, tena anakuwa Waziri kwenye key ministry!. Ningekuwa CC ya CHADEMA ningemsamehe Kitila Mkumbo
  5. Mlipomtimua Zitto kwa kutumia CC kangaroo, niliwauliza humu, CC ya Chadema, inapata wapi mamlaka ya kumuadhibu NKM wakati mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu?!, hakuna aliyejibu, angalieni nini kiliwakuta waliomtimua Zitto, na angalieni Zitto ni nani, tena anakwenda kuteuliwa mbunge wa kuteuliwa kwenye zile nafasi 10 za uteuzi za JPM, linganisha makamanda waliosimamia kutimuliwa kwa Zitto!. Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!"

    Hii ni mifano michache tuu ya dhambi ya dhana ya usaliti inavyoendelea kuitafuna Chadema ndani kwa, ndani, hapo sijamtaja Dr. Slaa, hadi watu kumuita Dr. Mihogo!, leo angalia waliombeza Dr. Slaa wako wapi, ulinganishe na mahali Dr. Slaa alipo!, haiwezekani watu na makamanda wameipigania Chadema kwa kuigharimikia kwa Machozi, Jasho na Damu, halafu leo uje uwaite wasaliti na kuwatimua kama mbwa!, kamwe Karma haiwezi kuacha salama Chadema!.
Leo Kangaroo court ya Chadema inakutana kumhukumu Halima na wenzake, Halima Mdee ni Mwenyekiti wa Bawacha, mamlaka yake ya nidhamu sio CC ya Chadema, hii CC ya Chadema iliyokaa leo kumvua uanachama Mdee, imepata wapi mamlaka hayo?.

Ndani ya majina yale 19 ya wabunge wa viti maalum wa Chadema, walioapishwa, wabunge 5 ni 'vidumu' vya wajumbe wa CC ya Chadema ambao sio vile 'vidumu' vya 'mpango kando', no!, ni vidumu vya cohabitation, mnaishi nyumba moja, mnalala chumba kimoja, kitanda kimoja!, huku mkiishi katika dhana ya ndoa, na kila mtu anawatambua kama mke na mume!, haiwezekani mwenza wako, akaibukia kwenye majina ya viti maalum bila wewe kujua, kisha akaamkia Bungeni Dodoma kuapishwa bila wewe, kujua!, namhurumia sana KM. JJ. Nnyika ni mtu muadilifu sana, lakini hajui, the games people plays!.

Miaka mingi nyuma nililizungumzia Chadema kuwa na kirusi, CHADEMA Kuna Kirusi! Je, Unajua kirusi hiki ni Nani?! Na The Motive Behind?
Sasa miaka mingi imepita nikajua sasa Chadema ni safi, kumbe bado!, na sio kuna kirusi, Chadema ina virusi!. Kikulacho...ki nguoni mwako!.

Naomba kuwa mtu wa kwanza kukujulisha kuwa JPM, anaweza kila kitu!, Japo Tanzania hatuna serikali ya mseto, kama aliweza kumteua Anna Mngwira na Prof. Kitila, wakiwa ACT, kwenye baraza lake jipya la mawaziri, hawezi kushindwa kuwateua Mdee na Esta Bulaya, manaibu mawaziri katika serikali yake na sisi huku bara tukaunda serikali ya umoja wa kitaifa!.

I Wish Halima Mdee and her team, all the best, kama wataadhibiwa kwa kuukataa ujinga!, Karma itawashughulikia watesi wao, na wao kuwa elevate machoni pa watesi wao!.

Mungu Ibariki Chadema at least for once iweze kutenda haki, kuepuka adhabu ya karma, maana kiukweli Chadema hapo ilipo, ni almost dead kinachosubiri ni kukomelea tuu msumari wa mwisho kwenye naniliu la Chadema na kulishusha 6ft under!. The choice is theirs!

Mungu Ibariki Tanzania!.

Paskali
 
Mungu Ibariki CHADEMA at least for once iweze kutenda haki, kuepuka adhabu ya karma, maana kiukweli CHADEMA hapo ilipo, ni almost dead kinachosubiri ni kukomelea tuu msumari wa mwisho kwenye naniliu la CHADEMA na kulishusha 6ft under!. The choice is theirs!....mwisho wa kunukuu
 
Pascal Mayalla, Mambo ya CHADEMA waachie Chadema wenyewe.

Pascal Mayalla, karma is myth. Chama chenu kimeua watu Unguja na Pemba, kimeumiza wengi wasio na hatia, je wamedhurika nini?

Mlimuua kwa kumchinja shingo Mawazo, mlimtwanga Tundu Lissu marisasi,
Karma imemuadhibu Nani?

Anzory na Ben Saanane wamepotezwa jumla, karma imefanya Nini?
Tangu enzi za Mwalimu, Karume na kupotezwa Abdullah Kassim Hanga, hadi leo, karma imewaadhibu Nini? Au karma ipo kuwaadhibu CHADEMA tu pale wanapowatimua wasaliti?
 
CHADEMA Wako kwenye mitihani sana , ni wazi kuwa watesi wao wanafurahia UCHONGANISHI waliowafanyia ....na wanaona kabisa hawachomoki...., leo wanatakiwa watoe maamuzi ya busara kwakuwa uamuzi wa kuwafukuza utashangiliwa na wana CCM na uamuzi wa kuwabakiza pia utatumiwa kuchochea kuni na wana CCM ....

Kiukweli demokrasia nchini iko kwenye mtihani mkubwa sana ....hakuna shaka kuwa hawa wanamama ni wana chadema kwa moyo kabisa lakini bahati mbaya wamenasishwa kwenye mtego na watesi wao pamoja na chama chao
 
Mkuu mbona una 'hara' Sana siku hizi?
Wakuu nawasihi aliyechukua akili za huyu Mayala amrudishie.

Yani kwamba kweli unaamini wanapaswa kuachwa pamoja na kuvunja Katiba kwa kiwango kisichomithilika pamoja na kudhalilisha chama kwa kiwango hicho.

Najaribu kuwaza kama hili Jambo lingetokea CCM hakika sio kwamba wangeitwa na kamati kuu,bali wangeitwa na wasiojulikana,ingekuwa ni kuokota viroba baharini tu
 
Pascal Mayalla, karma is myth. Chama chenu kimeua watu Unguja na Pemba, kimeumiza wengi wasio na hatia, je wamedhurika nini?
Mlimuua kwa kumchinja shingo Mawazo, mlimtwanga Tundu Lissu marisasi,
Karma imemuadhibu Nani?
Anzory na Ben Saanane wamepotezwa jumla, karma imefanya Nini?
Tangu enzi za Mwalimu, Karume na kupotezwa Abdullah Kassim Hanga, hadi leo, karma imewaadhibu Nini? Au karma ipo kuwaadhibu CHADEMA tu pale wanapowatimua wasaliti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…