Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu

Mkuu hii karma ni kwa ajili ya Chadema tu? Maana umetoa mifano yao mingi tu.

Hivyo vyama vingine huwa havikumbwi na karma? Au wenyewe huwa hawakosei?
 
Mdee amepata tabu sana miaka miwili au mitatu hii kwa ajili ya uchadema wake
Mdee amekaa mahabusu,mdee ana vimeo kibao mahakamani,mdee amefungiwa bungeni mwaka mzima yote kwa sababu ya misimamo ya kichadema,halafu eti sisimizi tu wanamuita mdee msaliti
Kuna watu walijifanya makamanda lakini wamekimbia nchi wanakula kuku kwa mrija na familia zao,Mdee hakuthubutu kukimbia,leo anatekeleza sheria mnamuita msaliti,laana ya Dr Slaa izidi kuwaangamiza
 

Ww ulivyopata kura moja ilikuwa karma ya wapi? Afrika ni masikini huku wakoloni wote wakiwa wametufanyia ukatili wote, mbona wao karma haiwakuti na bado ni matajiri kuliko sisi, mbona hiyo karma haiwakuti? Acha porojo za kiswahili, cdm fukuza hao wahuni ASAP, tuko tayari kwa hiyo karma.
 
Shetani akikutaza sana kufanya jambo.... ujue uko njia sahihi.

Tatizo unawaza kuhusu viongozi wa chama; unasahau kuhusu wanachama na wapenzi wa CHADEMA. Wooooote uliowasema waliondoka, na CHADEMA haikufa, mpaka mwaka huu imebidi dola nzima itumie nguvu kupindukia kuiangusha.

Ukweli ni kwamba wanachama na wapenzi wanataka kuona damu, nothing less. CHADEMA wachague, viongozi au wanachama.
 

Ni hivi, leo kikao ni kuwafukuza, ukishirikiana na shetani unapigwa chini, historia haina nafasi fullstop.
 
Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu lazima ujiulize mapenzi na upendo wa ccm kwa Chadema umeanza lini ?

Watu ambao tulithubutu kusema kuwa ni wasumbufu bungeni na wanakwamisha maendeleo leo hii tunawatetea kwa upendo hapana hapo kuna ulakini.

Mimi ni mwanachama lakini sehemu yeyote yenye chembe chembe ya usaliti sio kufumbia macho hata kidogo maana tabia hiyo itakomaa tu

Hivyo wakikutwa na makosa wachukuliwe hatua kali.

Kidumu chama tawala.
 

Leo hakuna kugeuka nyuma, ni kuwapiga chini, sisi wapiga kura bado tuna imani kubwa na cdm. Mtaji wa cdm ni watu sio njaa ya viongozi kadhaa.
 
Kama karma huja kingese hivyo basi inabidi ikaribishwe kwa mikono miwili lakini wakufukuzwa haki yao ni leo na si vingine
 
Hata Ibilisi kabla ya kuasi alikuwa hajalaaniwa.
Historia yake ya awali haimfanyi asiwe msaliti kwa kula njama za kujaribu kuharibu kazi ya Mungu.

Unapimwa kwa matendo yako, historia yako nzuri siyo excuse ya usaliti!

Hata Membe, Baba yake Lau Masha, Mzee Jumbe, Kassela Bantu, Abdallah Fundikira, Nassoro Moyo, Kassanga Tumbo, Bibi Titi, James Mapalala wote hao wamewahi kuwa wana CCM/TANU wazuri kabisa, ila walipokengeuka wakanyooshwa.
Kwenye harakati za kushika dola au kuikamatia dola hupaswi kucheka na wasaliti hata kama huko nyuma wamewahi kuwa makamanda wazuri. Usaliti ni kansa, ukiuruhusu tu inakula kwako!

Pia fahamu kuwa kila aliyefukuzwa Chadema amewahi kuifanyia kazi nzuri Chadema huko awali, lakini at the end of the day, nidhamu lazima itamalaki. Chama ni collective responsibility siyo kujiamkia tu na kufoji maamuzi ya vikao ili ushibishe tumbo lako, hilo halikubaliki
 
Nna uhakika leo hawafukuzwi.
Ila watasisitizwa kufuata katiba ya chama ya kuchangia asilimia ya posho kwenye chama..

Na Mwenyekiti kuendelea kujilipa madeni hewa

Imani pekee kwetu sisi wanacdm ni kuwapiga chini hao wahuni, ila wakiwaacha ndio wajue support yetu kwao itaanza kuondoka rasmi.
 
njaa mbaya sana hasa ikimpanda mtu kichwani
 

Peleka uduwanzi mbali, iwe Mbowe anajua ama hajui, leo ni kupiga chini hao wahuni. Unadhani utatupoteza kwenye utaratibu dhidi ya hawa wahuni wachache kurubuniwa na ccm?Hata Mbowe akizingua mwenyewe tunamzimia taa, itakuwa hao wahuni wachache?
 
Sikiliza paskali biblically ukishika amri tisa ukavunja moja tu basi inahesabiwa kwamba umevunja zote. kukipigania chama hakimpi mtu mandate ya kuvunja sheria au misimamo ya chama. Kama umesoma kweli Law school Basi ni rahisi sana kuelewa vitu vidogo kama hivi.
karma my foot
 
Unataka kusema Karma inatengenezwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…