Makamba aja na kitabu "Cha kale Ni dhahabu"

Dr am 4 real PhD

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
11,640
Reaction score
24,066
Screenshot_20240524-203545.png

Screenshot_20240524-203641.png

"Niwakati tulipokuwa mafunzoni Monduli Machi, 1976 hadi Januari, 1977 ndipo nilipomfahamu vizuri Yusufu Rajabu Makamba na tukawa marafiki tangu wakati huo mpaka sasa. Nikatokea kuutambua vizuri uwezo wake wa uongozi. Nilivibaini vipaji vyake adimu vya kuhamasisha, kuunganisha watu, kujieleza na ubunifu. Pia moyo wake wa kujituma, kutokata tamaa na uhodari wa kazi. Ndiyo maana nilipokuwa Rais nilimteua kuwa Mkuu wa Mkoa na Mbunge na nilipokuwa Mwenyekiti wa CCM nilimteua kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.”

—Dkt. Jakaya M. Kikwete, Rais wa Awamu ya Nne wa Tanzania

Kuhusu Mwandishi:

Mwandishi wa kitabu hiki, Yussuf Rajabu Makamba, ni mkulima na mfugaji. Amewahi kuwa Mbunge, Katibu Mkuu wa CCM, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, na ni Afisa Mstaafu wa JWTZ. Amewahi pia kuwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kigoma na Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa.

Mwandishi ameandika vitabu vingi ikiwemo ‘Methali, Semi na Vitendawili vya Kisambaa

Wakuu kinapatikana mkuki na nyota @15,000/=

Wapenzi wa vitabu mkipata muda tusome kitabu Cha mzee wetu Yusuf makamba.

Wasalaam
 
Itakuwa vizuri sana kama atakuwa ameiombea msamaha ile kauli yake "tata" ya wazuri hawafi. Mizengo Pinda ilibidi ajitokeze hadharani na kuomba msamaha kwa kauli yake ya "wapigwe tu".

Kama hajafanya hivyo na hatafanya hivyo, sipati picha mitandaoni humu siku akikata moto. Yote kwa yote ni jambo jema kwamba viongozi wetu hawa nao wameanza kuandika uzoefu wao.

Screenshot_20240524_211507_Samsung Internet.jpg
 
Itakuwa vizuri sana kama atakuwa ameiombea msamaha ile kauli yake "tata" ya wazuri hawafi. Mizengo Pinda ilibidi ajitokeze hadharani na kuomba msamaha kwa kauli yake ya "wapigwe tu".

Kama hajafanya hivyo na hatafanya hivyo, sipati picha mitandaoni humu siku akikata moto. Yote kwa yote ni jambo jema kwamba viongozi wetu hawa nao wameanza kuandika uzoefu wao.

View attachment 2998486
Ulimi uliteleza pia itakua Ni hasira maana magufuli aliwakatia umeme hakua anawasikiliza Wala kushaurika so mzee Yusuf makamba akaamua kutema vapour
 
View attachment 2998460
View attachment 2998461

"Niwakati tulipokuwa mafunzoni Monduli Machi, 1976 hadi Januari, 1977 ndipo nilipomfahamu vizuri Yusufu Rajabu Makamba na tukawa marafiki tangu wakati huo mpaka sasa. Nikatokea kuutambua vizuri uwezo wake wa uongozi. Nilivibaini vipaji vyake adimu vya kuhamasisha, kuunganisha watu, kujieleza na ubunifu. Pia moyo wake wa kujituma, kutokata tamaa na uhodari wa kazi. Ndiyo maana nilipokuwa Rais nilimteua kuwa Mkuu wa Mkoa na Mbunge na nilipokuwa Mwenyekiti wa CCM nilimteua kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.”

—Dkt. Jakaya M. Kikwete, Rais wa Awamu ya Nne wa Tanzania

Kuhusu Mwandishi:

Mwandishi wa kitabu hiki, Yussuf Rajabu Makamba, ni mkulima na mfugaji. Amewahi kuwa Mbunge, Katibu Mkuu wa CCM, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, na ni Afisa Mstaafu wa JWTZ. Amewahi pia kuwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kigoma na Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa.

Mwandishi ameandika vitabu vingi ikiwemo ‘Methali, Semi na Vitendawili vya Kisambaa

Wakuu kinapatikana mkuki na nyota @15,000/=

Wapenzi wa vitabu mkipata muda tusome kitabu Cha mzee wetu Yusuf makamba.

Wasalaam
Tunakipata wapi?
 
Back
Top Bottom