Elections 2010 Makamba atinga jimboni Bumbuli leo na ufanya vikao vya siri.....

Elections 2010 Makamba atinga jimboni Bumbuli leo na ufanya vikao vya siri.....

Hamna kitu kamjamaa kametumia State House Resources kujijenga huko Bumbuli na kulaghai wananchi kuwa ana baraka za Ikulu kugombea hilo jimbo siku nyingi tu. Na ukweli usiokua na shaka haka kamjamaa si ndio kalituandikia hutoba ya mbayuwayu? :A S-eek: hakuna jipya
 
Mi nakubaliana na Gembe 100%...si lazima mtu uwe mbunge ndo uweze kusaidia wananchi jamani!!!
Kwanza hili suala la watoto wa viongozi (watawala?) kuanza kuandaliwa kuja kuwa viongozi (watawala?) naona linaelekea pabaya sana...tunarudi ktk masuala yale yale ya wafalme,machifu, etc kuwarithisha uongozi (utawala?) watoto wao hata kama hawana vipaji vya uongozi. Ila naamini ipo siku watu watakataa kufanywa watawaliwa milele...that day is coming!!
 
Hamna kitu kamjamaa kametumia State House Resources kujijenga huko Bumbuli na kulaghai wananchi kuwa ana baraka za Ikulu kugombea hilo jimbo siku nyingi tu. Na ukweli usiokua na shaka haka kamjamaa si ndio kalituandikia hutoba ya mbayuwayu? :A S-eek: hakuna jipya


Hotuba ya Mbayuwayu wa the worst speech ever..

Sijawahi kuona hotuba nzuri ambayo imetoka magogoni kuanzia 2005,kama ipo naomba mnipe..
 
as per in red above, sehemu nzuri ya kuleta mabadiliko ya ukwei katika nchi yeyote hasa Tanzania ni Bungeni maana ndiyo watunga sera na sheria zinazoendesha nchi na kwingineko

Naomba unitajie mabadiliko ya ukweli ambayo umewahi kuyasikia Bungeni?

wapo wanaosema Richmond..or bla blah..what is the outcome of RDC?usanii at large..

wengine watakwambia EPA..what is the outcome?Wananchi wanataka maendeleo na siku zote mipango mizuri ya maendeleo inapangwa na watendaji makini ambao wanajua nini cha kufanya.Wabunge kazi ya ni kupitia Bajeti za wizara tu..Tena wanaozisoma kwa umakini ni wachache na wanajulikana..

Lete Hoja kama za mdudu Nyuki
 
Naomba unitajie mabadiliko ya ukweli ambayo umewahi kuyasikia Bungeni?

wapo wanaosema Richmond..or bla blah..what is the outcome of RDC?usanii at large..

wengine watakwambia EPA..what is the outcome?Wananchi wanataka maendeleo na siku zote mipango mizuri ya maendeleo inapangwa na watendaji makini ambao wanajua nini cha kufanya.Wabunge kazi ya ni kupitia Bajeti za wizara tu..Tena wanaozisoma kwa umakini ni wachache na wanajulikana..

Lete Hoja kama za mdudu Nyuki

Bunge ni maigizo tuuuuuuuuu. its funny how much time, space and money is wasted on this white elephant kuanzia 'kuonesha nia' , nomination, maigizo kwene bunge sessions mpaka uchaguzi mwingine unapowadia.
 
as per in red above, sehemu nzuri ya kuleta mabadiliko ya ukwei katika nchi yeyote hasa Tanzania ni Bungeni maana ndiyo watunga sera na sheria zinazoendesha nchi na kwingineko
Kama hawa waliopo wameshindwa kutunga sheria huko bungeni ya kubadilisha maisha yetu zaidi ya kuongeza tu maslahi yao, yeye atabadilisha kwa vipi? kwa maneno matamu anayotuambia leo?
Huyu mwandishi wa hotuba tu ni tapeli wa kisiasa kama bosi wake tu, hamna lolote! Wakimchagua wameliwa kama tulivyoliwa wadanganyika tulipoahidiwa maisha bora kwa kila mdanganyika kisha baadaye tukaambiwa tutafute namna ya kuyapata wenyewe. Na maneno mengine mengi ya kejeli.
:frusty:
 
Kazi za mbunge hazifahamu! Yeye aendelee na kufanya kazi huko ikulu tu! Kwani mbunge kazi yake ni kujenga barabara? Au kutatua matatizo ya wananchi moja kwa moja au ni serikali?
 
Inasikitisha watu watanunua ulaghai wake, japo navutiwa na umri wake na alikuwa mtu poa kule Galanos lakini kwamba yeye kuwa mbunge wangu nahitaji kushawishiwa zaidi kwani ni kweli haelewi anakwenda bungeni kufanya nini na si ajabu kaahidiwa uwaziri mdogo na kona ya Magogoni na Lithuli.
 


In my own personal opinion this guy is a fraud! Kumuamini na kumkubali eti tu kwa sababu ni kijana ni sawa na doing the same kwa mgombea simply kwa sababu ni kabila lako au dini yako!

Mmemsahau Lau Masha nini?
mi nimewasoma watu hapa, sijaamini macho yangu!!
simple minds tu hakuna lolote!!
kama ni kijana mwenye akili, kwa nnini anakimbilia siasa? Tutamtenganisha vipi na bab yake na wote wanaomzunguka kwenye meza wakati wa chakula cha jioni?

kwa kijana yeyote mwenye akili, nategemea nione anaanzisha kampuni, ambayo siyo ya kifisadi, innovative business, then anatoa ajira kwa growing brains (vijana)........at the same time, biashara hiyo, inatoa huduma kwa jamii!! (sio biashara ya kukusanya ushuru Ubungo lakini - coz, that is shyt business, huwezi kuwa kijna alafu unakuwa na biashara kama ile)
 
Vichekesho vya siasa hivi utaviona Tanzania pekee.
Yaani full vichekesho dah kweli wadanganyika tumelogwa na mchawi wetu kesha jifia siku mingi inabidi tumtafute mganga.
 
Hotuba ya Mbayuwayu wa the worst speech ever..

Sijawahi kuona hotuba nzuri ambayo imetoka magogoni kuanzia 2005,kama ipo naomba mnipe..
Ukisema ukweli, watu wataanza kusema ooh! kwa vile hamumjui tu! is very talented.........sawa, talented, sisi tutajuaje kama hatuoni product zake? kama hotuba zote anazotoa Mkwere ni shyt, maana yake muandikaji wake no bogus kabisa!!!
 
:argue:Hivi kwa Tanzania Ubunge ni ajira au? Why dont Tanzania take it as a prestige where one goes there for Publicity rather than income? Those who are fighting it for more income aspiration are weakening other social and economic sectors such as education, health etc.

My suggestion is that salaries and allowances for MPs should be made low like Religions leaders so that no one fight for it for income aspiration.
 
as per in red above, sehemu nzuri ya kuleta mabadiliko ya ukwei katika nchi yeyote hasa Tanzania ni Bungeni maana ndiyo watunga sera na sheria zinazoendesha nchi na kwingineko

Swafi sana Mkuu jibu lako ni vema tosha,

Sasa basi je kwa Tanzania hiii kunatatizo gani ambalo hao wabunge wetu waendapo bungeni wanashindwa tetea miswaada ya manufaaa ya nchi na kupitisha miswaada mibovu huko bungeni?

Vijana ambao wanao wanaia ubunge kwa ungwe hii wao wamejiandaa vipi ambao twawaita Taifa la Leo? Wameandalika vipi maana hao hao vijana wametokea UVCCM nandio hao katika mikutano yao huko kuanzia mkutano kuu wa Taifa UVCCM ni mizengwe na majungu hadi huko ngazi za mikoa,wilaya,mashina na matwi sasa hawa sioni mto yao ni nini wanataka uongozi ili watufanyie nini kama wao ndio wapiga kura ya kupitisha wajumbe kugombea ubunge na wanatuchagulia watu ilimradi mtu tu amempa gari ahakikishe ameshinda jimbo na kutandaza fitna na mizengwe?

Me ninge isifu sana UVCCM kila ilipo nchi nzima kuchagua viongozi inao waona ni swafi kwa maendeleo yao na si bora kiongozi ati umembiwa na M/kit wako kuwa fulani atatufaa sana wajua yule fulani ni mtu mzuri sana kuliko fulani hapo jua kuna chuki ndani yao hawatufai hao,

Sasa kwa J.Makamba sawa yuko huru kugombea lakini jeee yupo kwa maslahi ya Chama au Nchi? sio tu kijana anaingia bungeni kuendelea pongeza miswaada hoi kupitishwa si twatarajia kuona chachu ndani ya bunge ambalo lina vijana wakakamavu na sio wasaliti

 





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Nimewaiteni kwa mambo mawili. Kwanza, kuzindua kitabu nilichokiandika. Pili, kuzungumzia uvumi na minong'no kwamba natarajia kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bumbuli.

Nianze na jambo la pili. Baada ya kutafakari kwa kina, na kuzungumza na wana-Bumbuli wenzangu, nimeamua niombe fursa ya kuwa sauti yao, kuwawakilisha na kuwasemea Bungeni, kuwatumikia na kushirikiana nao kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jimboni kwetu.

Nimesukumwa na mambo gani?

1. Kwa muda mrefu, nimekuwa na hamu kubwa sana ya kushiriki mijadala ya msingi inayohusu mustakabali wa nchi yetu, nimekuwa na hamu ya kutoa mawazo yangu binafsi na kuyaweka hadharani, kuyaboresha kupitia mijadala na utafiti, na kuyatumia kubadilisha hali za maisha ya watu wa kwetu. Nimeonelea kwamba nafasi ya Ubunge itanipa fursa hii.

2. Naamini kwamba, baada ya kufanya kazi kwa karibu na Rais Kikwete, naweza kuchukua mfano wake kuitumia siasa vizuri zaidi kuitumikia nchi yangu kwa namna pana zaidi. Naamini naweza kushirikiana na vijana wenzangu, wa CCM na wasio wa CCM, kuifanya siasa iwavutie vijana wengi zaidi na ionekane kama ni sehemu ya utumishi wa umma.

3. Asilimia 72 ya Watanzania wana umri wa chini ya miaka 29. Mwaka huu, vijana waliozaliwa mwaka 1992 watapiga kura. Letu ni taifa la vijana. Inabidi ifike mahali vijana sasa wajitokeze kwenye nafasi za uongozi ili sura ya uongozi wa nchi ifanane na hali halisi ya nchi. Tutakapojitokeza wachache na tukafanikiwa, hata vijana wadogo zetu nao watakuwa na hamu ya kufuatilia siasa na tutakuwa hatujawapoteza katika kujihusisha masuala ya nchi na wengine wengi nao watajitokeza kwasababu wataona inawezekana. Hata hivyo ujana peke yake sio sifa ya uongozi.

4. Naamini uzoefu wangu kama Msaidizi wa Rais, kwa kuzunguka na Rais nchi nzima mara mbili, wakati anaomba kura na baada ya kuchaguliwa, ambapo nimelazimika kusoma ripoti za maendeleo za Wilaya karibu zote, ambapo, kama Msaidizi wa Rais, nimehudhuria vikao vya Baraza la Mawaziri na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, pamoja na mikutano mingine mingi ya kimataifa na ndani ya nchi, utanisaidia sana kuwa Mbunge mzuri. Naingia kwenye siasa nikiwa nimejifunza mengi kuhusu Serikali na jinsi inavyofanya kazi, nikiwa nimejifunza jinsi baadhi ya maeneo nchini yalivyopiga hatua za maendeleo na mbinu gani wametumia na wale ambao bado hawajapiga hatua ni mambo gani hawajafanya. Nitatumia elimu hii na uzoefu huu kushirikiana na watu wa kwetu Bumbuli kusukuma maendeleo mbele.

Sasa, kutamani Ubunge ni jambo moja, lakini kudhamiria kuwa Mbunge mzuri ni jambo jingine. Nimedhamiria kuwa mtumishi mzuri wa wananchi. Na nimeamua kuufanya mchakato huu wa kuwania Ubunge uwe tofauti kidogo.

Nimefanya utafiti wa kina kuhusu jimbo la Bumbuli. Nimezunguka na kuzungumza na watu wa makundi mbalimbali, vijana , wazee, kina-mama, viongizi, watendaji na wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya, walimu, viongozi wa vijiji na vitongoji. Nilitaka kujua matumaini yao, kero zao, karaha zao, na mambo yapi wanayatarajia kwa viongozi wao. Nilifanya semina ya siku mbili wa wana-Bumbuli karibu ishirini wanaowakilisha makundi mbalimbali, na tukazungumza kwa kina sana kuhusu masuala ya Bumbuli. Nilipata fursa ya kutazama kwa kina takwimu na taarifa mbalimbali zinazohusu maendeleo ya Jimbo. Nikafanya utafiti wa kina kuhusu dhana nzima ya maendeleo ya maeneo ya milimani. Matokeo ya yote haya ni hiki kitabu. Nimekiita Bumbuli: Jana, Leo na Kesho.

Nilidhani kwamba, kama mtu unaamua kugombea uongozi wa eneo fulani, na kama kweli una dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko kwenye eneo hilo, lazima ujiridhishe kama kweli unayajua mambo ya hapo mahali. Sio kuyajua tu juu juu kwa kuambiwa au kusikia. Uyajue kwa kina, kwa takwimu, na vielelezo na kwa kina. Huwezi kuzungumzia mabadiliko kama huna tarifa zote za kina kuhusu Jimbo lako. Hiki ndicho nilichofanya.

Kitabu nimekimegawanya katika sehemu tatu: Sehemu ya kwanza nimeiita Jana, ambapo tunaangalia historia ya Wasambaa na Usambara kwa ujumla. Historia na utamaduni vina nafasi kubwa kwenye mchakato wa maendeleo. Lazima tuyazingatie haya. Sehemu ya Pili, nimeiita Leo. Yaani Bumbuli ya leo ikoje? Changamoto ni zipi na fursa ni zipi. Na kwa kuzingatia hayo tunaanzaje. Sehemu ya tatu, nimeiita Kesho, ambapo sasa naelezea Bumbuli mpya inaweza kufananaje. Kitabu hiki kitakuwa na matoleo mawili: moja kwa lugha ya Kiswahili na jingine kwa lugha ya Kiingereza. Toleo la Kiswahili litatoka baada ya mwezi mmoja. Nimeamua kuandika kwa lugha ya Kiingereza pia kwasababu nadhani moja ya majukumu ya Mbunge ni kupanua wigo wa washirika wa maendeleo wa jimbo lako. Ningependa watu wengi muhimu na mashuhuri niliokutana nao wakati nasafiri na Rais nje ya nchi nao wapate kukisoma, na kutazama ni kwa namna gani wanaweza kusaidia.

Kwakuwa sasa sio wakati wa kampeni, sio vyema kutumia fursa hii kutoa ahadi ambazo zinaweza kutafsiriwa kama sehemu ya kampeni. Na kitabu hiki hakiongelei chochote kuhusu Ubunge wala Mbunge wala dhamira yangu ya kugombea. Kinatoa fursa kwa mtu yoyote - mwekezaji, mtalii, mtafiti na wengineo – kuifahamu vizuri Bumbuli.

Lakini kwa kuwa mimi nina dhamira ya kugombea Ubunge, nimetumia fursa ya kukiandika ili kujifunza, lakini pia nitakitumia kama mwongozo wangu.

Kwenye kitabu tunaona kwamba asilimia 90 ya wakati wa Bumbuli wanategemea kilimo. Hata hivyo, wakati Tanzania nzima wastani wa wakati kwa eneo ni watu 49 kwa kilomita moja ya mraba, Jimbo la Bumbuli wastani ni watu 309 kwa kilomita moja ya mraba, na wastani wa watu wanne wanalima katika hekta moja ya ardhi. Maana ya takwimu hizi ni kwamba watu wana vishamba vidogo sana, na uzalishaji ni mdogo na tija ni ndogo. Kwahiyo, ni muhimu kubadilisha hali hii. Nitashirikiana na wananchi kuhakikisha tunaongeza tija kwenye kilimo lakini vilevile tunajikita kwenye kuzalisha mazao yenye thamani kubwa zaidi, na kutafuta soko la maana la mazao ya wakulima.

Katika Wilaya ya Lushoto yenye majimbo matatu, zao la chai linalimwa kwenye Jimbo la Bumbuli pekee. Lakini ukiwatazama wakazi wa Bumbuli huwezi kujua kwamba wanalima zao lenye soko la dunia. Ukitazama kwenye kitabu nimejaribu kulinganisha kati ya mkulima wa chai Rungwe na yule wa Mponde, kule kwetu. Inasikitisha. Wastani wa bei ya majani mabichi ya chai kule Bumbuli ni shilingi 130 kwa kilo, wakati Rungwe ni karibu mara tano ya hiyo. Chai ni ile ile na mnada wa chai ni huo huo kule Mombasa. Wakulima wa chai Bumbuli wanatumia eneo kubwa zaidi kwa asilimia 40 kuliko wale wa Rungwe lakini tunazalisha kidogo zaidi – kwa tofauti ya kati ya kilo 200 hadi 330 za majani yaliyosindikwa kwa hekta. Utafiti wa mwaka 2008 unaonyesha kwamba asilimia karibu 20 ya mashamba ya chai yametelekezwa kwasababu wakulima hawaoni tena faida ya kulima chai. Nimeazimia kushirikiana na wananchi kupata ufumbuzi wa matatizo ya wakulima wa chai.

Tunaona kwamba huduma bado ni tatizo. Wakati wa mvua barabara nyingi hazipitiki na shughuli zinasimama. Watu wanashindwa kwenye kupekeka maiti kwa mazishi au kwenye kuhudhuria harusi au maulidi kwasababu barabara muhimu, kwa mfano ya Soni-Bumbuli, hazipitiki. Mbaya zaidi ni kwamba kule kwetu mvua ni karibu kila siku. Katika jimbo zima la Bumbuli hakuna hata tawi moja la Benki. Inawezekanaje mahali watu wanalima zao kubwa kama chai, wana biashara kubwa za mboga na matunda lakini hawana hata tawi moja la Benki. Matokeo yake ni kwamba hakuna mikopo, na hakuna huduma ya kuweka fedha. Hali hii lazima ibadilike. Lushoto nzima lipo tawi moja tu la Benki. Lakini ukiangalia mahesabu ya lile tawi, pesa zinazowekwa ni maradufu ya pesa zinazokopeshwa. Maana yake ni kwamba ile Benki iko pale kukomba pesa za eneo lile, eneo la watu ambao ni masikini, bila kutoa huduma za mikopo. Hili na lenyewe nitalitazama.

Kwenye elimu, bado ziko changamoto nyingi. Watoto wengi hawamalizi shule ya msingi. Mwaka huu, 2010, wanafunzi 1,286 hawakuingia darasa la saba kutokea darasa la sita, na kati hao, tofauti na sehemu nyingine nchini, wengi wao, karibu asilimia 71, ni wavulana. Lazima tumalize tatizo hili.

Serikali imejitajidi kujenga shule nyingi za Sekondari. Lakini bado mahitaji yapo. Hadi sasa, wanafunzi waliopo darasa la saba ni takriban 5,548. Kama wote wataingia kidato cha kwanza, yatatakiwa madarasa mapya karibu 160 na walimu wengi zaidi, jambo ambalo haliwezekani kwa muda uliopo. Lakini tukienda na mwenendo wa hali halisi, labda asilimia 8-10 ya wanafunzi hawa, yaani wanafunzi kati ya 450 hadi 550, ndio wataingia kidato cha kwanza, na nusu ya hawa ndio watamaliza sekondari. Je, hawa wengine wanaenda wapi? Nitakaa na wananchi wa Bumbuli na kuzungumza kwa kina kuhusu yote haya. Tunapaswa kuongeza shule za Sekondari na hata zile zilizopo zinapaswa kuimarishwa ili kuwa na hadhi na uwezo wa kutoa elimu bora. Katika Jimbo la Bumbuli hatuna shule hata moja ya kidato cha tano na sita. Hili tutalirekebisha.

Huduma ya afya na yenyewe bado haijawafikia wananchi wale kwa kiwango cha kuridhisha ingawa jitihada zimefanyika. Kwa kweli yapo mengi ambayo siwezi kuyamaliza kuyazungumzia yote. Lakini nimejiandaa vizuri. Nimefanya utafiti wa kina kuyajua matatizo ya Bumbuli, nimezungumza sana na watu wa Bumbuli, wazee kwa vijana, kina mama kwa watoto, wanyabiashara, viongozi wa dini, na viongozi wa vijiji na vitongoji, na wamenieleza mambo gani wanayatarajia, na mimi nimejiandaa kushirikiana nao kuyafanikisha.

Nawashukuru kwa kunisikiliza

January Makamba
5 Julai 2010
 
Time Has Arrived!




Nimesukumwa na mambo gani?
1. Kwa muda mrefu, nimekuwa na hamu kubwa sana ya kushiriki mijadala ya msingi inayohusu mustakabali wa nchi yetu, nimekuwa na hamu ya kutoa mawazo yangu binafsi na kuyaweka hadharani, kuyaboresha kupitia mijadala na utafiti, na kuyatumia kubadilisha hali za maisha ya watu wa kwetu. Nimeonelea kwamba nafasi ya Ubunge itanipa fursa hii.

Me nakupa hongera zangu na ninakutakia kila lakheri na ufanikiwa katika hili la kuwa mbunge na ninategemea Chachu yako bungeni itakuwa nzuri.

Ila kuna swala mmoja nilipenda liwekwe baya kwa watanzania wote,
Mustakabali wa nchi, Ndio nini au nini maana ya Mustakabari wa nchi najua fika ni wachache sana wanao jua hili.

Je Mustakabali wa nchi hujadiliwa tu pindi wagombea wanapo hitaji kura toka kwa wananchi au mustakabali watakiwa kuwepo kwanza na wagombea na wanachi wote twatakiwa kuufuata na kufanya utekelezaji au inakuwa ni vipi?

Na Tanzania inamustakabali upi? J.Makamba kwa kuwa wewe umefanya kazi kwa ukaribu sana na Rais wetu JK basi ni furusa kwako na ndio mwanya wako wa kujipatia ubunge tupe wewe uyajua yao ya mustakabali wa nchi yetu ni upi? twahitaji kuujua kwanza, then tutakuuliza maswali mengine

 
Nani anaweza kunipa namba ya January Makamba?hata e-mail yake..anahitaji kupewa ushauri..No wonder hata speech za mkuu zimekaa vibaya sana.

Hapa anasema siyo vizuri kutoa ahadi
Kwakuwa sasa sio wakati wa kampeni, sio vyema kutumia fursa hii kutoa ahadi ambazo zinaweza kutafsiriwa kama sehemu ya kampeni.
hapa anaelezea ahadi zake

Nitashirikiana na wananchi kuhakikisha tunaongeza tija kwenye kilimo lakini vilevile tunajikita kwenye kuzalisha mazao yenye thamani kubwa zaidi, na kutafuta soko la maana la mazao ya wakulima.
ahadi nyingine tena
Watu wanashindwa kwenye kupekeka maiti kwa mazishi au kwenye kuhudhuria harusi au maulidi kwasababu barabara muhimu,
hapa tena,ana lengo la kuhakikisha kuna benki..sijui ametumia vigezo gani?

Katika jimbo zima la Bumbuli hakuna hata tawi moja la Benki. Inawezekanaje mahali watu wanalima zao kubwa kama chai, wana biashara kubwa za mboga na matunda lakini hawana hata tawi moja la Benki.
hapa tena
Watoto wengi hawamalizi shule ya msingi.
Shule za kata pia
Tunapaswa kuongeza shule za Sekondari na hata zile zilizopo zinapaswa kuimarishwa ili kuwa na hadhi na uwezo wa kutoa elimu bora. Katika Jimbo la Bumbuli hatuna shule hata moja ya kidato cha tano na sita. Hili tutalirekebisha.
afya pia
Huduma ya afya na yenyewe bado haijawafikia wananchi wale kwa kiwango cha kuridhisha ingawa jitihada zimefanyika.
Yote aliyoyaongea hapo alishindwa kuyafanya kwa kipindi cha miaka mitano akiwa anahudhuria vikao vya NEC,Baraza la Mawaziri,Safari mbalimbali za nje ya nchi kama alivyosema hapa

Naamini uzoefu wangu kama Msaidizi wa Rais, kwa kuzunguka na Rais nchi nzima mara mbili, wakati anaomba kura na baada ya kuchaguliwa, ambapo nimelazimika kusoma ripoti za maendeleo za Wilaya karibu zote, ambapo, kama Msaidizi wa Rais, nimehudhuria vikao vya Baraza la Mawaziri na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, pamoja na mikutano mingine mingi ya kimataifa na ndani ya nchi
anyways Mpeni kura za ndiyo kwa kuwa ni kipenzi chenu na mna mpango wa kunufaika na uongozi wake ila bado hajajenga hoja!
 
kwa kishindo cha January ni wakati wa mzee shelukindo kuonyeshaa uwezo wake kwa kujiunga na upinzania ili apambane na kijana huyuu..

naamini nguvu ya UMMA ni kubwa kuliko wananchama wa CCM bumbuli kwani natumai kwa sasa kijana huyuu ana mvutoo zaidi plus MIZENGWEE YAO..

MZEE SHELUKINDO JIFUNZE KWA DR SLAA NA ONYESHAA NJIA THABITII..
 
kwa kishindo cha january ni wakati wa mzee shelukindo kuonyeshaa uwezo wake kwa kujiunga na upinzania ili apambane na kijana huyuu..

Naamini nguvu ya umma ni kubwa kuliko wananchama wa ccm bumbuli kwani natumai kwa sasa kijana huyuu ana mvutoo zaidi plus mizengwee yao..

Mzee shelukindo jifunze kwa dr slaa na onyeshaa njia thabitii..

Umemwita mzee meaning umri umesogea. Kwanini badala ya kutafuta ugonjwa wa shinikizo la damu wakati huu asitumie akiba yake aliyojiwekea kwa kipindi alichokuwa mbunge au hata kiinua mgongo chake kubuni mradi wake ambao utatoa ajira kwake, familia yake na wengine? Ni lazima afie bungeni?
 
Genge umenena. Huyu jamaa hajajenga hoja ila anapiga kampeni.......zaidi mi namtakia heri tu. Kama wana Bumbuli wanazani ndie wachague ila wasije anza kulia lia baada ya mwaka mmoja!
 
..he should have announced his candidacy in Bumbuli, not in Dar.

..sounds like a smart kid, sasa tunasubiri tuone kipaji chake ktk mijadala ya bunge.

Baada ya miaka mitano atasema nilikuwa napata uzoefu nipeni mitano mingine. Kama alivyosema bosi wake mind you Afadhali uraisi una kikomo.

Wakati anapata uzoefu watu wanaumia tu.
 
Back
Top Bottom