Shy,
nimesubiria muda mwingi sana uende mahakamani lakini naona kimya. Nilichosema kuwa wewe unahusishwa kwenye ile skendo ya kuwakamata wana JF bado nastand by that na sifuti statement yangu so you can go ahead and do what you want!
haya mambo ya kutisha watu umeyatoa wapi tena? bado nakuuliza swali kama ulifaidika na nini wana JF walipokamatwa?
Makamba masikini,
mambo yanaenda south kwa kila anachogusa!
Inawezekana kabisa kuwa kuna mpango wa makusudi wa kuwalisha sumu hao waliobomolewa nyumba ili wapotee kabisa - Unadhani kuwa Makamba hakujua kuwa kuna haja ya kuchunguza hicho chakula au aliyekitoa?
Nahakika makamba hajui lolote kuhusu huo mchele mbovu,alichofanya yeye alimpigia tu simu huyo muhindi na kuomba msaada wa huo mchele ndio maana amekuwa mpole ktk hili kasheshe.CCM ndio zao tokalini wakawa na uhuruma na maisha ya watanzania zaidi ya kuwadenda wawape kura wakati wa uchaguzi.Zakaria ni milionea tanzania ktk matajiri wa bongo basi kama hamjui yeye yupo kwenye tatu bora.
Kama kweli Makamba hakujua kuwa huo mchele haufai (bado naamini kuwa alijua au alizembea tu ili asijue), kwanini hamchukulii hatua huyo mhindi? hawa wafanyabiashara kwa kiasia na ccm sijui wamefunga ndoa lini ambayo haiwezi kuvunjwa na wanadamu! grrrr
...Mi namshangaa Makamba..amenunua chakula bila kuangalia kina expire lini na kukitoa kama msaada hii inaingia akilini kweli..??.Hivi kweli kingekuwa chakula anachonunua kwa ajili ya familia yake kweli asingeangalia kina expire lini??? .. Hii mi natafsiri kama ni dharau na kejeli kwamba hawa wananchi wa tabata si binadamu na hawafai kupewa chochote kilicho bora..
Hapa Makamba amenakiliwa akimtaja Zakaria kama ndiye aliyemuuzia mchele mbovu, jee akipatiwa taarifa rasmi anaweza kumchukulia hatua kama mhalifu anayewalisha WTZ chakula kibovu?. au ndio basi lilopita limpita ataomba abadilishie na kadhia imekwisha.
"Nilinunua chakula kwa Zakaria nikawapelekea baada ya kuniambia wana matatizo yakiwamo ya masufuria na pamoja na mchele huo niliwapa pia magunia 10 ya maharage...inaonekana sasa suala hili linataka kugeuzwa la kisiasa," alisema Bw. Makamba.