ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 2,424
- 4,954
.Hiyo ya wafanyakazi waondoe kabisa unit 750 kwa mwezi kweli huu unyonyaji, au wakistaafu huduma inasitishwa?
We hujamwelewa mtoa mada hata kidogo.Wabongo bwana!! Badala ya kulia umeme wa majumbani ushushwe bei nyie mna taka bei zirnde juu ati Tanesco wana pata hadara. Jema kwenu nyie ni lipi??
Bilion moja ya ofa kwa tanesco ni pesa ndogo sana mdau acha wawape wafanyakazi wao tu....Hii tarif 4 ambapo umeme unanunua unit 1 shilingi 100 ni hasara kwa shirika, kwani Bei ya umeme tanesco anauziwa 200 kwenda juu yeye anawapa watu kwa shilingi 100 kigezo ni umasikini na matumizi madogo. Matajiri na watu wenye uchumi juu ndo wanaongoza kwa kuwa tarrif hii, huku mikoa inayoongoza kwa wateja wanaonunua umeme kwa 100 , ikiwa ni Daresalaama,Arusha, Kilimanjaro, mbeya na mwanza, mikoa ambayo watu wanapesa kuliko, hii tarrif itaua shirika
Pia tarif 6 hii wanapewa wafanyakazi wa TANESCO , shirika linatumia zaidi ya Bilioni moja 1 kila Mwezi kuwapa wafanyakazi umeme wa ofa , shirika halitakaa likue
Haya ndio mawazo ya kizalendo.Bila shaka management mpya imesikia italifanyia Kazi.Hii tarif 4 ambapo umeme unanunua unit 1 shilingi 100 ni hasara kwa shirika, kwani Bei ya umeme tanesco anauziwa 200 kwenda juu yeye anawapa watu kwa shilingi 100 kigezo ni umasikini na matumizi madogo. Matajiri na watu wenye uchumi juu ndo wanaongoza kwa kuwa tarrif hii, huku mikoa inayoongoza kwa wateja wanaonunua umeme kwa 100 , ikiwa ni Daresalaama,Arusha, Kilimanjaro, mbeya na mwanza, mikoa ambayo watu wanapesa kuliko, hii tarrif itaua shirika
Pia tarif 6 hii wanapewa wafanyakazi wa TANESCO , shirika linatumia zaidi ya Bilioni moja 1 kila Mwezi kuwapa wafanyakazi umeme wa ofa , shirika halitakaa likue
Ukiangalia kwa undani utagundua mabeberu bado ndo wanatuuzia Gesi kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme kwahiyo kiufupi Bei ya umeme inapangwa na mabeberu ya Gesi songas na kinyerezi. Cc ni tuna kauli kwenye vubwawa tu hivoHaya ndio mawazo ya kizalendo.Bila shaka management mpya imesikia italifanyia Kazi.
Hao wanaoitwa wa tarrif 4 wengi wao hata sio watu maskini wa kushindwa kulipia umeme..
Kuwekwe vigezo vipya vya ku assess umaskini Ili wanaostahili wapewe nafuu na wasiostahili wasipewe.
By the way kwani vyanzo vya umeme vinamilokiwa na nani hadi useme Tanesco anauziwa umeme kwa 200 per single unit?
Kwani akina Mwigulu nao wananinua bando! Siwezi kuamini.Sheria na kanuni za kijinga ndizo zinazosababisha wizi,rushwa na hujuma kila kona ya nchi.
Hivi kuna tatizo gani kwa bei ya umeme kuwa sawa kwa watumiaji wote.
Kama mtu ana matumizi makubwa atatumia zaidi na atanunua zaidi.
Mwenye matumizi madogo atatumia kidogo sio kupunguziwa bei tena kwa kufanya dili.
Yaani kwa bei hizo zinawafanya watu ndani ya Tanesco kupiga rushwa toka kwa wenye pesa ili wawekewe tarifu za chini kabisa wanunue umeme kwa bei ndogo.
Lakini Pia wafanyakazi wa Tanesco wanawaibia watanzania umeme.
Wafanyakazi wa Tanesco wengi hawanunui umeme wanapewa umeme mwingi sana kama bonas.
Sasa kwa wingi wao nadhani shirika ni lazima lipate hasara.
Hiyo ipo pia kwenye Mafuta ya Petroli ,diseli na mafuta ya taa.
Serikali inapata hadara kubwa sana kwa ujinga tu wa watu wabinafsi wasiojali maslahi ya taifa zaidi ya maslahi binafsi na siasa za kijinga.
Mafuta ya taa yanachanganywa sana na mafuta mengine kwa kuchakachua kwa sababu yana ushuru mdogo ukilinganisha na petrol. Sasa unajiuliza kwa nini kodi ya Mafuta ya taa isiwe juu ili kuondoa suala zima la kuchakachua na kuingiza taifa kwenye hasara ya kuwalipa wapiga dili ndani ya Ewura?
Simple ilikua umeme bei moja na Petrol ,diseli na mafuta ya taa yote bei moja 2300/- kwa mfano.
Mbona bando kwenye simu kila mmoja anapiga kwa gaharama inayotokana na matumizi ya na sio uwezo wa mtu eti ,kundi la kipato Fulani wakipiga simu au wakiweka bando bei iwe chini na wengine bei iwe juu.
Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
Nadhani pia kama shirika kuna kitu wanakikimbia,maana wao ndiyo wanaojua namna ya kuiba na kuzuia wizi wa umeme so kitendo cha kuwabana wafanyakazi wao wasipewe ahueni wao wafanyakazi watafundishana mbinu za kuiba na still kitalilazimisha shirika kuajiri wataalamu kutoka nje ya shirika ili kuwabaini wezi wa umeme nazo ni gharama pia.Hiyo ya wafanyakazi waondoe kabisa unit 750 kwa mwezi kweli huu unyonyaji, au wakistaafu huduma inasitishwa?
Na sisi TRA tusamehewe KODI ya mapatoHiyo ya wafanyakazi waondoe kabisa unit 750 kwa mwezi kweli huu unyonyaji, au wakistaafu huduma inasitishwa?