Makamba futa tarif 4 na tarrif 6, ambapo Bei ya unit moja ni sh 100 na sh 12 ilihali TANESCO wanaonunua zaidi ya 200

Basai wote tuuziwe sh 12 kwa unit
Mkuu Nishati ni gharama hata kama gharama hio sio pesa (ndio maana kuna vifaa energy efficient na matangazo ya don't waste energy) kwahio mkuu hizi tariff ndogo wameweka kwa watu wenye matumizi madogo sasa wakiweka pesa ndogo sana huenda watu wakaanza kufuja yaani wanaacha taa zinawaka au hata kutumia AC wakati milango ipo wazi....

Issue sio free bali ni affordable, na kwa watu ambao wamepewa limit ya unit 75 kwa mwezi matumizi yao sio ya kufuja ni kweli ni madogo..., kwahio hata Bwawa la Nyerere likianza kumwaga Megawatt Huenda tukafika huko ila hata huko itabidi kuwe na limit sio mtu mmoja unatumia umeme kama vijiji kumi sababu tu eti ni bei rahisi
 
Hiyo ni point. Nakumbuka miaka ya 1980s na mwanzoni mwa 1990s tuliongea sana kuhusu mashirika ya nje kuwekeza katika umeme ili kuwe na ushindani lakini hatukufanikiwa, kwa kuwa hakuna ushindani TANESCO wanafanya wanavyotaka.
 
Na polisi wanapewa nini ( risasi
 
Tanesco, wafanye mapatio ya Tariffs za matumizi ya umeme.Kwa maana tariffs hizi zinatumika ziliwekwa wakati ule Shirika linanunua umeme kwa bei kubwa kutoka dowan s,songas,IPTL ambako waliingia mikataba ya kifisadi,yenye kuwekwa minimum fixed rate ya kulipwa,kila mwezi, Shirika liwe limepokea umeme au halikupokea umeme kutoka kwa supplier.
Kwa kuwa,kuanzia June 2022 mradi mkubwa wa umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere -Rufiji utakaozalisha Megawatt zaidi ya 2,000 kwa gharama nafuu ya shs50 kwa unit utaanza,basi mchakato wa kufanya mapitio ya Tariffs uanze,ili kuwapunguzia makali ya maisha wananchi.

Faida
(1) Watu wengi wataweka na kutumia umeme kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
(2) Utapunguza matumizi ya kuni na mkaa.(uhifadhi wa misitu).

Mapendekezo
(1). TANESCO iweke tariffs mbili tu, tariff namba moja umeme wa viwandani -Three Phase
(2). Tariffs two-Umeme wa majumbani single phase
(3) wafanyakazi wa TANESCO,waendelee kupewa bonus Kama ilivyo kwenye mkataba wa Hali Bora kati ya Mwajiri na wafanyakazi kupitia chama Chao cha wafanyakazi.
Kwa wafanyakazi ambao hawana nyumba,ninadhani Kuna utaratibu,unaotumika kuwapa motisha..
 
Nilidhan ungependekeza wananchi wote wapatiwe umeme kwa 100/unit ndo ingekua bizuri zaidi
 
Polisi wanapewa shilling laki tatu kila mwezi kama posho.
Kama polisi wanapewa laki 3 kama posho
Basi na wafanyakazi wa Tanesco wapewe pesa za posho lakini umeme walipe
Kupeana motisha vitu vya umma ni kulitia Taifa hasara....
 
Wabongo bwana!! Badala ya kulia umeme wa majumbani ushushwe bei nyie mna taka bei zirnde juu ati Tanesco wana pata hadara. Jema kwenu nyie ni lipi??
Hawa wapiga debe wa hivi karibuni Ni kundi limeanzishwa lituchanganye Kisha tukubafi Tanesco ibinafsishwe,hapo tayari bwawa la mwalimu nyerere litakuwa limekamilika ili tuupate umeme wa gharama ndogo,miundombinu ya umeme Hadi vijijini tayari kwa Kodi zetu halafu wanakuja na hadithi za kuua Tanesco ili watubamize!
 
Mmmh! Sasa kama watafuja si matumizi yao ndo watalipa, umeme uwe bei chini kwa dunia ya Leo teknolojia inatumia umeme kwa Kila kitu Sasa ukiwa bei chini hata hili swala la ajira litapunguza ukosefu wa ajira kwa wingi maana kwenye kutumia umeme Kuna kazi nyingi sana na pia vitu vingi vya kuokoa muda vinatumia umeme.
 
Pesa ya kuhudumia shirika mfu la ATCL ielekezwe TANESCO


full stop
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…