Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
Makamba akiri kuwepo kwa makundi ndani ya chama tawala
Hemed Kivuyo, Arusha
10/19/2009
SIKU chache baada ya kudaiwa kuingia katika baadhi ya majimbo na kuendesha kampeni za kuwang'oa wabunge waliopo na kuwawekea mazingira ya ushindi watoto wake; Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amekerwa na makundi yaliyomo ndani ya chama hicho katika mikoa mbalimbali, ukiwamo wa Arusha.
Pamoja na hayo, Makamba pia aliwafananisha na watoto wadogo wanachama na viongozi wa chama hicho ambao wamehamia katika vyama vya upinzani kwa madai kuwa mtu mzima mwenye akili timamu hawezi kuhama CCM.
Alisema kuwa pamoja na chama hicho kuonyesha dalili nzuri ya kushinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa, bado kuna tatizo la baadhi ya wagombea wanaoshindwa katika kura za maoni ambao huhamia katika kambi ya upinzani na kundi la wanachama.
"Mimi naona kuwaita wazee wale waliohamia kambi ya upinzani siyo sahihi, bali ni kama watoto wadogo," alisema .
Aliwataka viongozi wa chama hicho mkoani Arusha kuhakikisha wanamfukuza mwanachama yeyote anayeonyesha dalili za kukiasi chama hicho kwa kumnyangâanya kadi ya uwanachama mapema.
"Kama kuna mtu mnaomuona ana dalili za kwenda upinzani na kutoa siri za chama, chukueni kadi mapema na aende huko anakotaka," alisema Makamba.
Katika hatua nyingine, Makamba alisema kuwa chama hicho kitawalipa 'posho' mawakala wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu pamoja na kuwepo kwa mawakala wengi wa kusimamia kura kwa upande wa chama hicho.
Makamba aliyasema hayo mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa wilaya, Jubilate Kileo wakati akimkaribisha kuzungumza na wanachama waliohudhuria katika mkutano huo.
Ziara ya Makamba mkoani Arusha ambayo ina nia ya kukiongezea nguvu chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa, umeikuta CCM ikiwa katika hali mbaya baada ya wanachama kadhaa na viongozi kuhamia kambi ya upinzani.
Pamoja na hayo pia chama hicho mkoani hapa kimegawanyika katika makundi mbalimbali ambayo huwaunga mkono baadhi ya viongozi na wengine wakiwapinga.
Wakati huo huo, jana Makamba aliwatoa nje waandishi wa habari katika mkutano wake kwa madai kwamba wataandika 'madudu'.
Hali hiyo ilitokea katika Ukumbi wa chama hicho mkoani hapa majira ya saa 5:55 asubuhi. Kabla ya hapo alitoa risala kwa waandishi hao kwa muda wa dakika 10 mbele ya viongozi na wanachama wa CCM huku akishangiliwa kwa nguvu wakisema: "Kidumu Chama Cha Mapinduzi".
Makamba alifika katika ukumbi huo saa 4:22 asubuhi akiongozwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Batilda Buriani na mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Mkoa wa Arusha, Elishilia Kaaya na viongozi wengine wa mkoani hapa.
Baada ya hapo Makamba ambaye wakati fulani alionekana kutabasamu, aliangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili vilivyopangwa kumpokea na kisha kuwagawiya wachezaji zawadi za fedha ambazo kiasi chake hakikufahamika. Makamba aliingia katika ukumbi huo saa 4:34 na viongozi kadhaa wa chama hicho walianza kusoma risala mbele yake na yeye aliitikia kwa kuwalaani waliokihama chama hicho.