Makamba mpiganaji! Mweh..

Makamba mpiganaji! Mweh..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Makamba ahimiza mapambano dhidi ya ufisadi

na Jacob Ruvilo, Kigoma

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba, amesema ufisadi unapaswa kupigwa vita na kila Mtanzania mzalendo, kwani umechangia kwa kiasi kikubwa kudidimia maendeleo ya nchi.

Makamba alisema hayo juzi kwenye semina ya viongozi wa CCM Jimbo la Kigoma Mjini iliyofanyika katika viwanja vya Lake Tanganyika.

Alisema suala la watu kujipatia mali kinyume cha utaratibu na kuhujumu nchi havina uhusiano wowote na CCM, kwani watuhumiwa wote hawakuagizwa na chama kufanya hivyo, bali ni hulka zao binafsi.

Makamba alifafanua kuwa suala la muumini wa dhehebu fulani kwenda kinyume na maadili au amri ya vitabu vya dini, hapaswi kulaumiwa sheikh au mchungaji, badala yake ni muumini husika ambaye mwisho wa siku ndiye atakayepata adhabu kwa Mungu.

Aidha, Makamba alisema suala la vyama vya upinzani kushika bango na kuidhihaki CCM kuwa ni mafisadi kutokana na viongozi wachache wasio waaminifu, halina maana, bali suala la umoja na mshikamano katika kupinga mafisadi hao ni jukumu la watu wote, ikiwamo CCM.

Mbali na hilo, Makamba alikemea baadhi ya viongozi wa chama hicho kutumia uwezo wao wa fedha kutoa rushwa ili kupita katika chaguzi mbalimbali kuwa ni moja ya upatikana wa viongozi mafisadi na wasiofaa kwa jamii.

Alisema Tanzania haikuandaliwa kutawaliwa na wenye nacho na kwamba hali hiyo inaweka tabaka la mwenye nacho na a asiyenacho, hali ambayo isipoangaliwa kwa umakini suala la rushwa litabaki kuwa ndoto.

My Take:
Nasubiri kina Rostam na wenyewe waunge mkono vita hii!!
 
Last edited by a moderator:
Hatimae "Yona" akubali kwenda Ninawi.
 
Hao ndio CCM, hivi mpaka leo hajui kua NCHI inaongozwa na CCM na kua CCM inatakiwa kudhibiti mafisadi wote kwa kutumia sheria za nchi.

Ohoo sorry, CCM inaendeshwa kwa imani, na ukivunja miiko ya imani za CCM utahukumiwa ahera.
 
Hizi zote ni Kampeni tu, maana wameona kuwa hakuna agenda nyingine zaidi ya ufisadi, tumechoka kusikia mambo ya ufisadi kila wakati huku hakuna kitu cha maana zaidi ya maneno tu
 
Ninawi ndo wapi mkuu, fafanua

kuna nabii/mtume alitumwa kwenda ninawi kutangaza injili akakataa na kuamua kwenda mji mwingine[tarshishi]baada ya dhoruba aliyoipata huko tarshishi akajirudi na kwenda ninawi kuhubiri injili,ni habari ipo kwenye biblia.
 
Ninawi ndo wapi mkuu, fafanua

Ukisoma kitabu cha Nabii Yona katika Biblia Takatifu, mji wa Ninawi haufafanuliwi kinagaubaga kwamba huko wapi bali ni mji mkubwa mno na ukubwa wake ni mwendo wa siku 3. Mungu alimwamuru Nabii Yona aende Ninawi kwa maana watu walizidi kutenda dhambi. Lakini Yona alikimbilia Tarshishi apate kujiepusha na uso wa BWANA. Mara ya pili BWANA alimwamuru tena Yona aende Ninawi na alipoingia mjini aliwatangazia watu wake kwamba baada ya siku 40 BWANA atauangamiza mji wa Ninawi. Watu wa Ninawi walimwamini BWANA na wakaanza kufunga, wakajivika magunia na kuketi katika majivu tangu mdogo mpaka Mfalme. Kuona hivyo BWANA alighairi na kuiacha hasira yake ya kuuangamiza mji wa Ninawi.
 
Mbona mwaka huu mtasikia mengi!!
 
Hii ni KAULI MBIU ya kampeni za uchaguzi mwaka huu na ule wa mwakani. Badala ya maisha bora kwa kila Mtanzania sasa ni piga vita ufisadi lakini waache wale waliokwisha jichotea wapumzike kwa amani!
 
Hii ni KAULI MBIU ya kampeni za uchaguzi mwaka huu na ule wa mwakani. Badala ya maisha bora kwa kila Mtanzania sasa ni piga vita ufisadi lakini waache wale waliokwisha jichotea wapumzike kwa amani!

labda ni baada ya kuona ile ya maisha bora kwa kila mtanzania imeshindikana au haitekelezeki tena
 
Makamba ahimiza mapambano dhidi ya ufisadi

na Jacob Ruvilo, Kigoma

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba, amesema ufisadi unapaswa kupigwa vita na kila Mtanzania mzalendo, kwani umechangia kwa kiasi kikubwa kudidimia maendeleo ya nchi.

Makamba alisema hayo juzi kwenye semina ya viongozi wa CCM Jimbo la Kigoma Mjini iliyofanyika katika viwanja vya Lake Tanganyika.

Alisema suala la watu kujipatia mali kinyume cha utaratibu na kuhujumu nchi havina uhusiano wowote na CCM, kwani watuhumiwa wote hawakuagizwa na chama kufanya hivyo, bali ni hulka zao binafsi.

Makamba alifafanua kuwa suala la muumini wa dhehebu fulani kwenda kinyume na maadili au amri ya vitabu vya dini, hapaswi kulaumiwa sheikh au mchungaji, badala yake ni muumini husika ambaye mwisho wa siku ndiye atakayepata adhabu kwa Mungu.

Aidha, Makamba alisema suala la vyama vya upinzani kushika bango na kuidhihaki CCM kuwa ni mafisadi kutokana na viongozi wachache wasio waaminifu, halina maana, bali suala la umoja na mshikamano katika kupinga mafisadi hao ni jukumu la watu wote, ikiwamo CCM.

Mbali na hilo, Makamba alikemea baadhi ya viongozi wa chama hicho kutumia uwezo wao wa fedha kutoa rushwa ili kupita katika chaguzi mbalimbali kuwa ni moja ya upatikana wa viongozi mafisadi na wasiofaa kwa jamii.

Alisema Tanzania haikuandaliwa kutawaliwa na wenye nacho na kwamba hali hiyo inaweka tabaka la mwenye nacho na a asiyenacho, hali ambayo isipoangaliwa kwa umakini suala la rushwa litabaki kuwa ndoto.

My Take:
Nasubiri kina Rostam na wenyewe waunge mkono vita hii!!
Mwkjj tunaikosea vita hii kwa kudeal na personality zaidi ya mfumo ndio maana akina makamba nao wanapata upenyo kuwa wahamasishaji kwa style hiyoo.

wamejipanga vema kuigeuzaa iwe ni vita ya wote ndani ya CCM.
Ufisadi sio tatizo la RA, EL, Mramba, Yona, Mkapa wala Chenge bali ni ukosefu wa Mfumo bora wa kuongoza na kutawala unaoratibiwa na CCM.

Natumai Makamba kwa sasa anapumua vema kwani amepanga kuungana na wabunge wote wa CCM waliojifanya ni wapiganaji wa vita dhidi ya ufisadi dhidi ya wenzao ndani ya chama chao.
 
lakini mbona sasa kila mtu anaelekeza macho yake kwenye ufisadi kuna nini???
 
kuna nabii/mtume alitumwa kwenda ninawi kutangaza injili akakataa na kuamua kwenda mji mwingine[tarshishi]baada ya dhoruba aliyoipata huko tarshishi akajirudi na kwenda ninawi kuhubiri injili,ni habari ipo kwenye biblia.

Sahisho kidogo. Yona alikuwa Nabii alyetumwa Ninawi mji mkuu wa Ashura (Assyria), himaya ambayo ilikuwa imeiteka Israel (North Israel) na kuwapeleka waisrael utumwani huko Ashuru mnamo karne ya nane kabla ya Kristu (BC). Yona hakuhubiri Injili maana unabii wake ulikuwa kabla ya kuzaliwa Yesu Kristu. Yona alipeleka ujumbe wa Mungu kwa watu wa Ninawi watubu la hasha Mungu atawaangamiza. Walitubu na wakapona kiama.

Hivi kweli Makamba anapeleka ujumbe wowote (huko aendako) wa maana wa kuifanya CCM na waumini wake watubu la sivyo nguvu ya umma atawaadhibu 2010? Tafakari.
 
Makamba wala sio mpiganaji mwaminifu. Kusema lolote usemalo mahali popote maadam kuna vyombo vya habari sio upiganaji. Kashfa aliyokuwa nayo pale Bungeni aliimaliza vipi? Paka anawezaje kuwadhibiti paka wasile panya?

Kama hakuna chombo cha habari au kama hajang'amua uwepo wa vyombo vya habari hasemi asemavyo. Kwa sababu hiyo ndio maana natamshi yake na maagizo yake daima yana utata mkubwa, kwani hatulii kupanga nini kukilenga. Anaongea kama vile mashabiki wanavyoongea bila muhtasari. Hivyo makosa ni mengi katika kauli zake. Ukitaka kushinda kampeni yako wala usimwalike atakuharibia.
 
hivi watu wanavyomjua huyu bwana alivyo kuwadi wa mafisadi anaweza kupambana na mafisadi kweli......hivi vichekesho na viini macho vya ukweli kabisa................huyu mzee mwehu kweli.............
 
Heading ya hii thread ni Makamba mpiganaji! Mweh.. au una maana Mwehu?
 
Not even bread and circuses, just a circus, a cheap bad circus at that.

Makamba wewe unapambana na ufisadi? Na wale wahindi waliokujengea nyumba utawaambia nini?

Na yule muajemi aliyempa mwanao kazi utamwambia nini?

Usifikiri nchi zima watoto wadogo wasiojua nyendo zako.
 
Back
Top Bottom