Changamoto kubwa, nionavyo mimi, ya nafasi ya uraisi ni kusita kufanya maamuzi kutokana na labda kuogopa lawama na kelele kutoka kwa wananchi na wadau wengine.
Makamba, Mwigulu na Nape;
Hawa matusi yameshamalizika ya kuwatukana kabla ya kufanya lolote, sijui kama kuna tusi la kuwatukana limebaki.
Hawa wameshapewa kila aina ya uzushi na kashfa kiasi sijui kama kuna uzushi mwingine umebaki. Hawa wameshaonyeshwa chuki na wawachukiao za kiwango cha mwisho, sijui kama kuna kipande cha chuki hawajaonyeshwa hawa jamaa. Kama Makamba mpaka mtu aliandaliwa kipindi fulani na kulipwa mamilioni kwa ajili ya kudeal na yeye tu.
Pamoja na hayo yote, hawa jamaa bado wapo wanakomaa na kupambana kivyao!
Hayo yote naona yamewakomaza sana na kuwapa ujasiri hawa jamaa kiasi kwamba ikitokea mmojawapo atapata nafasi ya juu na kuwa Rais hawawezi kusita kufanya maamuzi kwa wakati na stahiki maana hatokuwa na cha kuhofia kwa kuwa lawama zilishamtangulia tayari kabla ya yeye kufika hivyo ameshazizoea.
Nawasilisha.