Makamba, unatumia muda mwingi kujibrand kuliko kupambana na mgao umeme

Makamba, unatumia muda mwingi kujibrand kuliko kupambana na mgao umeme

Abuu Kauthar

Huku ninapoishi, Mburahati Barafu, katika wiki moja, umeme ulikatika siku sita kwa saa kuanzia sita hadi 14. Katika baadhi ya siku, umeme ulikatika mara kadhaa. Kukatika huko kwa umeme sio tu ni kero kubwa, lakini pia kumeongeza umaskini wa wananchi wanaotegemea nishati hiyo katika shughuli zao.

Baadhi yetu tunanunua vitoweo kwa wingi na kuwahifadhi katika jokofu. Wengi wetu imebidi tutupe samaki na kuku hao baada ya kuharibika kwa sababu tu ya mgao! Mamia ya kaya katika ambazo zinategemea umeme nazo zimejikuta zikisererekea katika umaskini kwa kukosa nishati wakiwemo wenye saluni, wauza juisi, watoa nakala za nyaraka.

Ukiwakuta mitaani mbele ya ofisi zao, utawakuta watu hao wamekaa nje wanapiga soga hawajui hatima yao.

Ulianza mgao wa mchana tu tukaambiwa ni matengenezo lakini sasa TANESCO wanakata hadi usiku! Hutokea baadhi ya siku umeme kuchelewa kurudi hadi saa tano usiku au zaidi. Isingekuwa Mwenyezi Mungu kutusitiri kwa mvua inayosaidia kupunguza joto, baadhi ya nyumba zisingelalika na huenda tungerejea zile zama za kulala vibarazani.

Nini kimebadilika katika kipindi kifupi tangu tulipobadili awamu ya utawala kutoka ya tano hadi ya sita. Tunaelewa kuwa kuna ukame, lakini wengi wetu hatuamini kama Rais John Magufuli angekuwa hai hali ingekuwa mbaya kiasi hiki. Kwa namna tunavyoona mwenendo wa viongozi wetu, ni vigumu kujua kama ni ukame tu au ni udhaifu wa viongozi na watendaji wa TANESCO?

Tuseme ukweli, kwa hali ilivyo sasa ni vigumu sana kupembua kati ya mchango wa ukame katika kupelekea tatizo la mgao na mchango wa uzembe. Walau kipindi kile Magufuli aliwakoromea na hata kuwatimua madarakani viongozi aliowapa majukumu ya kusimamia sekta hii nyeti ya nishati. Hivi sasa, tuna viongozi ‘baridi’ na ‘waelewa’ ambao wameamua kuwa wa kwanza kutoa nadharia, visingizio na kulaumu waliopita.[ badala ya kukabiliana na tatizo na kuliondoa.

Natamani wangejua kuwa wananchi wanataka umeme sasa, sio visingizio. Natamani wangejua kuwa haijalishi nani aliyekosea, sisi tunawatathmini kwa wanachofanya sasa kwani ukichambua utagundua kuwa kila awamu ilirithi matatizo ya awamu iliyopita, lakini na mazuri pia.

Nikiangalia ukurasa wa waziri wetu wa Nishati, bwana Januari Makamba, napata hisia kuwa huyu ni mtu aliye mbali na uhalisia wa maisha ya watu, anayefikiria mustkbali wake wa kisiasa kuliko shida ya mgao, akiposti picha kwenye kumbi na maofisi na watu wa hadhi, akionesha namna alivyo mweledi na mjuvi wa hali ya nishati duniani na nadharia ya namna Tanzania tutajikomboa.

Makamba ni bingwa wa kujibrand, ukimuona anavyopozi kwenye picha utadhani ni Obama mpya, shukran kwa timu ya timu yenye weledi imayohusika kumjenga na kumuandaa kwa nafsi ya juu kabisa! Lakini itasaidia nini kama kazi ya kutatua shida za wananchi katika nafasi hii uliyonayo sasa huitendei haki?

Nilipata hamu ya kutembelea tovuti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambako unakutana tena na sura ya Waziri Makamba akiahidi ‘kuzaliwa upya kwa TANESCO’ katika habari moja na akiahidi TANESCO litakuwa shirika bora la umeme Afrika ya Mashariki kwenye habari nyingine!

Ukiangalia vizuri hii tovuti, huwezi kujua kama nchi iko gizani! Wanazungumzia kila kitu lakini sio mgao! Hata ratiba ya mgao basi? Hata ushauri? Hata kutuomba radhi basi? Au ndio nyi haliwahusu bali ni makosa ya waleeee waliokuwepo kabla!? Hali ni hiyo hiyo katika tovuti ya Wizara ya Nishati. Kuna mgogoro wa mgao wa umeme lakini kuna habari nzuri tupu ni kama vile kila kitu kipo shwari mpaka unajiuliza hizi tovuti ni kwa ajili ya kusomwa na nani?

Hizi ndio siasa ambazo wananchi tumechoka nazo. Waziri Makamba anza na kutatua hili tatizo la mgao, kabla hujawaza makubwa na kabla hujamchafua Rais Samia na kuonekana hafai!
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Alitoa siku mbili atatoa suluhisho la kudumu kukatika kwa umeme mpaka Sasa hajaonekana.
Hamutaki matamuko tunataka meme usikatike.
Japo amemwaga wapambane jf wakumtetea,mtaangukua pua tu.
Jamaa anawaza 2030 mengine hayamhusu kabisa
 
Of course makamba anatumia nguvu nyingi kujidanganya na kelele za mitandaoni kuwa anatosha kuingia ikulu. Watanzania sio wajinga. Refer mwigulu nchemba na kampeni zake za mawe...lol
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
Sasa kama nyinyi ni TANESCO, mkisoma hiyo makala mtakuwa mmeona tatizo liko....It is too much, it is too frustrating.
 
2030 ni mbali sana.kama ni kweli anajihangaisha bure.na kama kuna back up nyuma yake basi wamemchagulia wrong ministry..lakini binafs sioni ubaya kwa mtu kuwa na ambition/ ndoto ya kuwa raisi.
 
Back
Top Bottom