Mujuni2
Senior Member
- Jun 11, 2008
- 142
- 3
Kwa wasiomjua Makamba, wanaweza kumshangaa! Makamba hakuwa chaguo la Kikwete ila aliletwa na mtandao chini ya makamanda EL na RA, kama walivyo wengine kina Sitta, Chenge na wengineo. Na huyu Makamba aliletwa kama stooge wa mtandao, ili afanye yale anayoambiwa na waliomliomuweka, na sifa kubwa ni kutenda bila kuuliza maswali, kama ilivyo asili ya wajeshi kupokea amri kutoka kwa waliowazidi vyeo. Sasa anachowakilisha Makamba ni sauti za wakubwa zake, kwa maana nyingine anatumika kama amplifier, na ndio maana katu hawezi kujadili swal la Ufisadi na Makundi ndani ya chama chake. Hivi karibuni wamempa zawadi ya kijana wake(January) kuwa mbunge, naye akiandaliwa kupokea amri za wakubwa wa baba yake (makamanda wa uliokuwa mtandao), baada ya kuonekana Makamba kachoka kimwili na akili pia, so he has to be replaced. Wengi mtasema ni Consipiracy theory but that's a fact. Kwa kumalizia atakachosema mzee huyu, si yeye bali analipa fadhila ya waliompa unga, kwa ku-amplify interest zao bila kujali his own intergrity, anahitaji kuhurumiwa. Pole Mzee.