Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mangula, Halmashauri ya Mji wa Makambako, Sunday Chungwa, kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ameahidi kushirikiana kwa karibu na wananchi wa mtaa wake ili kuhakikisha maendeleo ya pamoja.
Chungwa alisisitiza kuwa ushirikiano kati ya viongozi na wananchi ni muhimu kwa maendeleo endelevu, akiahidi kuwa sauti za wananchi zitazingatiwa katika mipango na maamuzi ya mtaa huo.