Makambo aikimbia Yanga ajiunga Horoya ya Guinea

Makambo aikimbia Yanga ajiunga Horoya ya Guinea

Nachojua Makambo hapo Yanga alikua km mpita njia tu , yaani alikua anajitangaza ,Yanga wanamlipa mshahara tu, hakusajiriwa kwa hela , toka ametoka lupopo alikua huru ,mkataba wake unamruhusu kuondoka muda wowote

Km Yanga watapata hela basi ni kiasi kdg tu
 
Habari mpya ni kwamba leo Mshambuliaji tegemeo wa Yanga Heritier Makambo amejiunga na Horoya ya Guinea kwa mkataba wa miaka mitatu, habari zaidi zitafuata.
Horoya ndio timu gani. Hivi kwenye 8 bora africa walioingia simba walikuwepo? Sijawahi isikia hii timu
 
Dili la Makambo kujiunga na Horoya FC , Yanga kusubiri hisani tu ya mchezaji huyo na kocha wake kwakuwa alikuwa Yanga kwa mkopo akitokea DC Motema Pembe . Agent Mwinyi Zahera na klabu hiyo ndio wenye dhamana ya mwisho katika kumuuza mshambuliaji huyo mzee wa kuwajaza aliyegeuka kipenzi cha wanayanga kwa muda mfupi.

Samuel Samuel
Sawa Sawa Mkuu ,huyo DCMP walishindana Tabia , mtoto wa Kinshasa huyo ,hata Fc lupopo pia walishindwana hivyo hivyo , hapo Yanga watapata pesa kdg sana
 
Nachojua Makambo hapo Yanga alikua km mpita njia tu , yaani alikua anajitangaza ,Yanga wanamlipa mshahara tu, hakusajiriwa kwa hela , toka ametoka lupopo alikua huru ,mkataba wake unamruhusu kuondoka muda wowote

Km Yanga watapata hela basi ni kiasi kdg tu
Mkuu mbona unajichanganya unasema hakua na mkataba Mara unasema tena mkataba wake unamruhusu kuondoka sasa tukueleweje?
Mchezaji anaruhusiwaje kucheza ligi huku akiwa hana mkataba/ makubaliano maalumu na klabu?
 
Kwa ulaya hili jambo haliwezekani
Lakini kwa afrika bado hakuna
Yaani kocha anakuwa wakala wa mchezaji how comes? Kweli Bongo soka hakuna ladha kabisa Kocha anakuwa anawachezaji wake kwenye timu na Yanga mkakubali tu, anaaga anaenda Congo kumbe anakwenda kupiga dili na watu wanaachwa wamesinzia tu, tangu lini mchezaji anauzwa na timu iliyokopeshwa mchezaji yaani mmekopeshwa mchezaji halafu nyinyi mumuuze tena hiyo inakuja kweli?. Zahera anacheza na akili zenu kawaona kabisa ni vichwa maji halafu eti mmsubiri aje ndio muulize kuhusu hiyo ofa ya mchezaji na wakati tayari ameshatinga uzi wa HOROYA, Acha niweke nukta hapo.
Kwa ulaya hili haliwezekani ila kwa Afrika kocha anaweza kuwa wakala bila shida yoyote.
 
Sasa ka unajua kua hao mikia walikosea kwa kutokujua mauzo ya Okwi mbona mnafanya Yale Yale?.
Au wote ni mikia ila imetofautiana nyie wa kwenu wa mbuzi ila wao wa ng'ombe
👏👏👏👏👏
 
Mkuu mbona unajichanganya unasema hakua na mkataba Mara unasema tena mkataba wake unamruhusu kuondoka sasa tukueleweje?
Mchezaji anaruhusiwaje kucheza ligi huku akiwa hana mkataba/ makubaliano maalumu na klabu?
👏👏👏👍
 
Back
Top Bottom