Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Naibu Mkurugenzi wa Siasa na Matukio wa Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, Ali Makame Issa amebainisha kuwa kuingia ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni maamuzi ya kikatiba ya Wazanzibari wenyewe, na si jambo linalopaswa kuamuliwa nje ya misingi hiyo ya kisheria.
Chama hicho kimeeleza wasiwasi wake juu ya jinsi baadhi ya viongozi wanavyopigania maslahi yao binafsi huku wakivunja haki za kikatiba ambazo Wazanzibari wenyewe waliziridhia kupitia kura. Imeelezwa kuwa katiba inatamka wazi taratibu za kufuata baada ya uchaguzi, ikiwemo uwasilishaji wa majina ya nafasi za makamu wa rais, lakini inashangaza kuona baadhi ya washirika wanachagua kutia saini za viongozi binafsi badala ya kuheshimu katiba ya nchi.
Soma: Rais Mwinyi: Tumeanza mazungumzo na ACT Wazalendo ya malalamiko yao kuhusu Serikali ya umoja ya Kitaifa
Pamoja na changamoto hizo, CUF imepongeza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikitambua kuwa ni hotuba ya kiongozi wa kweli wa kitaifa. Chama hicho kimeshiriki mtazamo wa Rais kwamba kukubali kukaa pamoja na kujadili masuala kwa maridhiano si ishara ya udhaifu kwa upande wowote.