Kenya 2022 Makamishina IEBC: Jumla ya kura zilizohakikiwa ni 100.1% ndio tunauliza hiyo ziada sawa na kura 143,000 imetoka wapi?

Kenya 2022 General Election
Kura zilizoharibika hakuna ..wasimamizi wa uchaguzi vituoni inaonekana wamesaidia watu kupiga kura vizuri..!!
Kwenye uchaguzi wa kuamua mshindi, kura zilizoharibika (Default cast votes) huwa haziwekwi kwenye takwimu, ni kura halali (valid cast votes) tu ndizo zinajumuishwa. Hivyo kwenye uchaguzi wa Kenya huwezi kuona kura iliyoharika ikitangazwa sambamba na kura halali.
 
10% ya 100 = 10
10% ya 1000= 100
10% ya 10,000= 1000
 
Hata mkipinga matokeo mahakamani hakuna mabadiliko ,subiri uone maigizo ya demokrasia. Hii ndo afrika
Mkuu sio kwa KENYA!!kama kweli kuna hilo tatizo, na mahakama ikaribaini ni kweli hakuna namna!!Kenya sio kama hizi nchi nyingine za kiafrika, huku hakuna mahakama.
 
Kama hayo malalamiko ni ya maafisa wale wa juu kabisa wa tume basi raila yeye ana uhalali wa kulalamika.
 
Duuu aibu 1% = 0.01.
Kwa hiyo 0.01 ya 14,000,000 = 140,000.
Kumbuka hapo 100 hatuzungumziii asilimia tena tunazungumzi kitu kizima.
Ni ngumu kuelewa sana hii.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya 0.01 na 0.01%.

0.01% = 0.0001 = 1/10,000

0.01% ya 14,000,000 = 1/10,000 = 1,400
 
Va

Valid point kivipi? U discuss matokeo wakati namba zinajieleza. Wapuuzi tu. Wafula kawanyoosha.
Kwamba Chebukati kawa-treat kama sie wapiga-kura wengine tu. Hajawashirikisha kwenye kujadili matokeo ya mwisho kama commissioners wa IEBC.
 
Makamishina wanne wa IEBC wanapingana matokeo ya Rais wa Kenya wanasema matokeo yalipikwa

Wanadai kuna kura zaidi ya 143,000 hazijulikani zimetoka wapi na Chebukati alishindwa kuwapa majibu

Wanapeleka ushahidi mahakamani

Source Citizen tv
Haya mahesabu mnayakosea kwa kutokujua hesabu au ni malengo ya kupitosh?
Ukijumlisha asilimia za wagombea wanne unapata jumla ya asilimia 100.01% na siyo 100.1% kama unavyotaka kupotosha! Na hiyo inatokana na ku-round off figure kwa kutumia decimal points 2. Ukitaka kujumlisha asilimia zote hupaswi kutumia ambazo ziko rounded off, unatumia zikiwa na desimali zake zote na unapata 100%. Na hiyo 0.01% "inayoonekana kuzidi" kwa waliokimbia hesabu ina jumla ya kura.

1. Asilimia za ushindi za wagombea wanne zikijumlishwa zinafika 100.01%. Kimahesabu ilitakiwa zikijumlishwa ziwe 100%.

MAELEZO: Asilimia iliyotangazwa ni approximately (iliyokadiriwa kwa desimali 2). Hii inakubalika kimahesabu, ili mradi haibadilishi nafasi ya mgombea. Ngoja tuoneshe asilimia bila kukadiria:

* Williamu Ruto: 7,176,141/14,213,027 x 100 =50.489885089%. Ikakadiriwa kuwa 50.49%

* Raila Odinga: 6,942,930/14,213,027 x 100 = 48.849059388%. Ikakadiriwa kuwa 48.85%

* George Wajackoyah: 61,969/14,213,027 x 100 = 0.4360014232%. Ikakadiriwa kuwa 0.44%

* David Waihiga: 31,987/14,213,027 x 100 = 0.2250541%. Ikakadiriwa kuwa 0.23%

Ukijumlisha hizo asilimia bila kukadiria kwa desimali 2:
50.489885089%
48.849059388%
+ 0.4360014232%
0.2250541000%
JUMLA: 100%

Ukijumlisha kwa kukadiria desimali 2: 50.49% + 48.85% + 0.44% + 0.23% = 100.01%

Kwa mtu aliyeaminiwa kuwa kamishina wa tume huru ya uchaguzi, kutumia sababu ya kujumlisha asilimia kwa kutumia zilizokadiriwa na kufumbia macho asilimia halisi ili kujenga hoja NI AIBU YA MWAKA. Pia Raila kukubali hoja hiyo na kuifanya kama sababu ya kugomea matokeo na kwenda mahakamani ni AIBU YA MWAKA PIA. Ukitilia maanani kuwa wote Raila na Ruto wamekadiriwa kwa kiasi sawa! Ruto amekadiriwa kwa juu ikawa 50.49% na Raila amekadiriwa kwa juu ikawa 48.85%.


Hiyo sababu haiwezi kuwa sababu ya kubadilika kwa mshindi, achilia mbali kuwa makamishina hawakupaswa kujumlisha hivyo.

Lakini pia kwa makusudi kabisa hilo ongezeko la 0.01% wakadai ni ongezeko la kura zaidi ya laki moja. Wakati hata kama hilo ongezeko ni ongezeko halisi (wakati si ongezeko halisi) basi lingekuwa ni ongezeko la kura 1,421 tu. Hata kama hizo ukiamua kuzitoa kwa Ruto na kumpa Raila bado isingebadili mshindi wa uchaguzi huu.

Sasa hiyo hoja ndiyo hoja kubwa sana kwa mtazamo wa wale makamishina wanne waliosusa na wakaifanya hoja namba MOJA.

2. Makamishina wanadai hawakushirikishwa! Wanadai walioneshwa tu matokeo ambayo yameshaandikwa tayari, mwenyekiti hakutupa nafasi ya kuyahaskiki! Ikumbukwe kuwa kuna timu ya wataalamu wa tume waliokuwa wanahakiki matokeo pamoja na mawakala wa wagembea wote. Hivi inaingia akilini kazi kubwa ya kuhakiki matokeo ya kwa siku 6 iliyofanywa na watu wengi sasa iweze kuhakikiwa tena na makamishina 7 kwa masaa machache kabla ya matokeo kutangazwa!! Hicho ni kitu kisichowezekana na kililenga kutaka kukwamisha zoezi zima! Kwa hiyo namuunga mkono mwenyekiti kutumia mamlaka yake ya kikatiba kutangaza matokeo, asiyeridhika aende mahakamani!!

Ushauri wangu kwa Raila: Matokeo ya vituo vyote wanayo, na jumla ya kura aliyopata anaifahamu, aseme bayana amepata ngapi? Mawakala wake walishiriki uhakiki, ni vituo vipi ambavyo kura zake zimepunguzwa? Vinginevyo ANAJIAIBISHA!!
 
Kama hayo malalamiko ni ya maafisa wale wa juu kabisa wa tume basi raila yeye ana uhalali wa kulalamika.
Sentensi yako imekaa kiutata na kibishi sana. The other way round: ^Kama hayo malalamiko ni ya maafisa wale wa CHINI KABISA wa tume, basi Raila HANA uhalali wa kulalamika.^

Nilidhani makosa ni makosa tu, ama?
 
Hesabu za wapi hizo? 0.01% ya 14M ni only 1400
Halafu nilimtazama yule kamishina wa tume ya uchaguzi ya kenya ambaye ndiye makamu mwenyekiti akidai kuwa hiyo 0.01% inawasilisha kura 143,000. Na mzee Odinga akaamini kuwa kapigwa! Huyu mama hakustahili kuwa kamishina wa tume na ameiaibisha sana kenya iliyokuwa inafuatiliwa dunia nzima!
 
Nice presentation.

Hata hiyo extra 0.1% kwenye 100.1% (if at all), bado haiji hiyo 143,000. Badala yake, 0.1% ya 14M = 14,000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…