Kenya 2022 Makamishina IEBC: Jumla ya kura zilizohakikiwa ni 100.1% ndio tunauliza hiyo ziada sawa na kura 143,000 imetoka wapi?

Kenya 2022 General Election
Cha kushangaza ni kuwa Odinga ana nakala ya matokeo ya urais ya vituo vyote vya uchaguzi na kura alizozipata anajua kuwa hazijatosha, ndiyo maana hana tuhuma ya kuibiwa kura, na hata akiulizwa kura zako ni ngapi hawezi kusema!
 
Halafu nilimtazama yule kamishina wa tume ya uchaguzi ya kenya ambaye ndiye makamu mwenyekiti akidai kuwa hiyo 0.01% inawasilisha kura 143,000. Na mzee Odinga akaamini kuwa kapigwa! Huyu mama hakustahili kuwa kamishina wa tume na ameiaibisha sana kenya iliyokuwa inafuatiliwa dunia nzima!
Raila si ni engineer, yule? Anashindwaje kujiridhisha mwenyewe before aje kulalamika? It means ndiyo watakuwa wakifanya hesabu za fedha ya miradi kwenye mikataba, siyo? Kama ndivyo, basi hafai kuwa president.
 
Haya mahesabu mnayakosea kwa kutokujua hesabu au ni malengo ya kupitosh?
Ukijumlisha asilimia za wagombea wanne unapata jumla ya asilimia 100.01% na siyo 100.1% kama unavyotaka kupotosha! Na hiyo inatokana na ku-round off figure kwa kutumia decimal points 2. Ukitaka kujumlisha asilimia zote hupaswi kutumia ambazo ziko rounded off, unatumia zikiwa na desimali zake zote na unapata 100%. Na hiyo 0.01% "inayoonekana kuzidi" kwa waliokimbia hesabu ina jumla ya kura.

1. Asilimia za ushindi za wagombea wanne zikijumlishwa zinafika 100.01%. Kimahesabu ilitakiwa zikijumlishwa ziwe 100%.

MAELEZO: Asilimia iliyotangazwa ni approximately (iliyokadiriwa kwa desimali 2). Hii inakubalika kimahesabu, ili mradi haibadilishi nafasi ya mgombea. Ngoja tuoneshe asilimia bila kukadiria:

* Williamu Ruto: 7,176,141/14,213,027 x 100 =50.489885089%. Ikakadiriwa kuwa 50.49%

* Raila Odinga: 6,942,930/14,213,027 x 100 = 48.849059388%. Ikakadiriwa kuwa 48.85%

* George Wajackoyah: 61,969/14,213,027 x 100 = 0.4360014232%. Ikakadiriwa kuwa 0.44%

* David Waihiga: 31,987/14,213,027 x 100 = 0.2250541%. Ikakadiriwa kuwa 0.23%

Ukijumlisha hizo asilimia bila kukadiria kwa desimali 2:
50.489885089%
48.849059388%
+ 0.4360014232%
0.2250541000%
JUMLA: 100%

Ukijumlisha kwa kukadiria desimali 2: 50.49% + 48.85% + 0.44% + 0.23% = 100.01%

Kwa mtu aliyeaminiwa kuwa kamishina wa tume huru ya uchaguzi, kutumia sababu ya kujumlisha asilimia kwa kutumia zilizokadiriwa na kufumbia macho asilimia halisi ili kujenga hoja NI AIBU YA MWAKA. Pia Raila kukubali hoja hiyo na kuifanya kama sababu ya kugomea matokeo na kwenda mahakamani ni AIBU YA MWAKA PIA. Ukitilia maanani kuwa wote Raila na Ruto wamekadiriwa kwa kiasi sawa! Ruto amekadiriwa kwa juu ikawa 50.49% na Raila amekadiriwa kwa juu ikawa 48.85%.

Hiyo sababu haiwezi kuwa sababu ya kubadilika kwa mshindi, achilia mbali kuwa makamishina hawakupaswa kujumlisha hivyo.

Lakini pia kwa makusudi kabisa hilo ongezeko la 0.01% wakadai ni ongezeko la kura zaidi ya laki moja. Wakati hata kama hilo ongezeko ni ongezeko halisi (wakati si ongezeko halisi) basi lingekuwa ni ongezeko la kura 1,421 tu. Hata kama hizo ukiamua kuzitoa kwa Ruto na kumpa Raila bado isingebadili mshindi wa uchaguzi huu.

Sasa hiyo hoja ndiyo hoja kubwa sana kwa mtazamo wa wale makamishina wanne waliosusa na wakaifanya hoja namba MOJA.

2. Makamishina wanadai hawakushirikishwa! Wanadai walioneshwa tu matokeo ambayo yameshaandikwa tayari, mwenyekiti hakutupa nafasi ya kuyahaskiki! Ikumbukwe kuwa kuna timu ya wataalamu wa tume waliokuwa wanahakiki matokeo pamoja na mawakala wa wagembea wote. Hivi inaingia akilini kazi kubwa ya kuhakiki matokeo ya kwa siku 6 iliyofanywa na watu wengi sasa iweze kuhakikiwa tena na makamishina 7 kwa masaa machache kabla ya matokeo kutangazwa!! Hicho ni kitu kisichowezekana na kililenga kutaka kukwamisha zoezi zima! Kwa hiyo namuunga mkono mwenyekiti kutumia mamlaka yake ya kikatiba kutangaza matokeo, asiyeridhika aende mahakamani!!

Ushauri wangu kwa Raila: Matokeo ya vituo vyote wanayo, na jumla ya kura aliyopata anaifahamu, aseme bayana amepata ngapi? Mawakala wake walishiriki uhakiki, ni vituo vipi ambavyo kura zake zimepunguzwa? Vinginevyo ANAJIAIBISHA!!
Kilikuwa na ulazima gani wa kukadiria kwa 2 decimal point?
 
Cha kushangaza ni kuwa Odinga ana nakala ya matokeo ya urais ya vituo vyote vya uchaguzi na kura alizozipata anajua kuwa hazijatosha, ndiyo maana hana tuhuma ya kuibiwa kura, na hata akiulizwa kura zako ni ngapi hawezi kusema!
Tatizo alishaaminishwa na kuamini 100% kwamba yeye ndiye the 5th! Unajua mshtuko wa ghafla si jambo la kitoto. Mara nyingi, katika hali hiyo, huwa akili zina-tendency ya kuhamia DRC (siyo Democratic Republic of Congo, bali Department of Retrogressive Cognition).
 
Haya mahesabu mnayakosea kwa kutokujua hesabu au ni malengo ya kupitosh?
Ukijumlisha asilimia za wagombea wanne unapata jumla ya asilimia 100.01% na siyo 100.1% kama unavyotaka kupotosha! Na hiyo inatokana na ku-round off figure kwa kutumia decimal points 2. Ukitaka kujumlisha asilimia zote hupaswi kutumia ambazo ziko rounded off, unatumia zikiwa na desimali zake zote na unapata 100%. Na hiyo 0.01% "inayoonekana kuzidi" kwa waliokimbia hesabu ina jumla ya kura.

1. Asilimia za ushindi za wagombea wanne zikijumlishwa zinafika 100.01%. Kimahesabu ilitakiwa zikijumlishwa ziwe 100%.

MAELEZO: Asilimia iliyotangazwa ni approximately (iliyokadiriwa kwa desimali 2). Hii inakubalika kimahesabu, ili mradi haibadilishi nafasi ya mgombea. Ngoja tuoneshe asilimia bila kukadiria:

* Williamu Ruto: 7,176,141/14,213,027 x 100 =50.489885089%. Ikakadiriwa kuwa 50.49%

* Raila Odinga: 6,942,930/14,213,027 x 100 = 48.849059388%. Ikakadiriwa kuwa 48.85%

* George Wajackoyah: 61,969/14,213,027 x 100 = 0.4360014232%. Ikakadiriwa kuwa 0.44%

* David Waihiga: 31,987/14,213,027 x 100 = 0.2250541%. Ikakadiriwa kuwa 0.23%

Ukijumlisha hizo asilimia bila kukadiria kwa desimali 2:
50.489885089%
48.849059388%
+ 0.4360014232%
0.2250541000%
JUMLA: 100%

Ukijumlisha kwa kukadiria desimali 2: 50.49% + 48.85% + 0.44% + 0.23% = 100.01%

Kwa mtu aliyeaminiwa kuwa kamishina wa tume huru ya uchaguzi, kutumia sababu ya kujumlisha asilimia kwa kutumia zilizokadiriwa na kufumbia macho asilimia halisi ili kujenga hoja NI AIBU YA MWAKA. Pia Raila kukubali hoja hiyo na kuifanya kama sababu ya kugomea matokeo na kwenda mahakamani ni AIBU YA MWAKA PIA. Ukitilia maanani kuwa wote Raila na Ruto wamekadiriwa kwa kiasi sawa! Ruto amekadiriwa kwa juu ikawa 50.49% na Raila amekadiriwa kwa juu ikawa 48.85%.

Hiyo sababu haiwezi kuwa sababu ya kubadilika kwa mshindi, achilia mbali kuwa makamishina hawakupaswa kujumlisha hivyo.

Lakini pia kwa makusudi kabisa hilo ongezeko la 0.01% wakadai ni ongezeko la kura zaidi ya laki moja. Wakati hata kama hilo ongezeko ni ongezeko halisi (wakati si ongezeko halisi) basi lingekuwa ni ongezeko la kura 1,421 tu. Hata kama hizo ukiamua kuzitoa kwa Ruto na kumpa Raila bado isingebadili mshindi wa uchaguzi huu.

Sasa hiyo hoja ndiyo hoja kubwa sana kwa mtazamo wa wale makamishina wanne waliosusa na wakaifanya hoja namba MOJA.

2. Makamishina wanadai hawakushirikishwa! Wanadai walioneshwa tu matokeo ambayo yameshaandikwa tayari, mwenyekiti hakutupa nafasi ya kuyahaskiki! Ikumbukwe kuwa kuna timu ya wataalamu wa tume waliokuwa wanahakiki matokeo pamoja na mawakala wa wagembea wote. Hivi inaingia akilini kazi kubwa ya kuhakiki matokeo ya kwa siku 6 iliyofanywa na watu wengi sasa iweze kuhakikiwa tena na makamishina 7 kwa masaa machache kabla ya matokeo kutangazwa!! Hicho ni kitu kisichowezekana na kililenga kutaka kukwamisha zoezi zima! Kwa hiyo namuunga mkono mwenyekiti kutumia mamlaka yake ya kikatiba kutangaza matokeo, asiyeridhika aende mahakamani!!

Ushauri wangu kwa Raila: Matokeo ya vituo vyote wanayo, na jumla ya kura aliyopata anaifahamu, aseme bayana amepata ngapi? Mawakala wake walishiriki uhakiki, ni vituo vipi ambavyo kura zake zimepunguzwa? Vinginevyo ANAJIAIBISHA!!
Kuna tofauti kubwa sana kati ya 0.01 na 0.01%.

0.01% = 0.0001 = 1/10,000

0.01% ya 14,000,000 = 1/10,000 = 1,400
Siyo 0.01% ni 0.1% ambayo kimsingi ni sawa na kura 14000
Soma hapo juu, mkuu
 
Hata ungekua ww ndo Chibukati uache hela ya bure kwa kumtangaza Baba ambae akiingia anaweza kukuletea figisu zaidi?
 
Mwalimu wako wa hesabu alikudandanya %1 ya 14M ni 140000
1660675199963.png

1% of 14M = 140,000

0.01% of 14M = 1,400
 
Kilikuwa na ulazima gani wa kukadiria kwa 2 decimal point?
Hiyo ni kawaida kwenye summary, vinginevyo asilimia za Ruto ni 50.489885989% na Odinga ni 48.849059388%. Wote walipandishiwa decimal point ya 2 kuwa 9 kwa Ruto, na kuwa 5 kwa Odinga. Hakuna mgombea kati ya Ruto na Odinga aliyeathirika kwa kutumia decimal point mbili!. Kama asilimia za kura za wagombea wote zikijumlishwa bila ku-round-off to two decimal points jumla inakuja 100%.

Nilitegemea Odinga aseme kuna kura zangu kadhaa nimeibiwa kitu ambacho hawezi kuthubutu!! Akubali tu kuwa mzee mzima kapigwa mweleka pamoja na mbeleko ya Uhuru Kenyatta! (ambaye kwa aibu pia yuko kimyaaaa!!)
 
Back
Top Bottom