Makampuni Binafsi Tanzania Yananyima haki ya ongezeko la mishahara kwa mwaka na wanaondoa motisha ya mwaka kwa wafanyakazi!!!

Makampuni Binafsi Tanzania Yananyima haki ya ongezeko la mishahara kwa mwaka na wanaondoa motisha ya mwaka kwa wafanyakazi!!!

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2020
Posts
3,443
Reaction score
4,006
Wakuu,

Hili ni bandiko la mshangao na masikitiko kwa sauti za wafanyakazi kutoka sekta binafsi zimeiga seriklali kutoongeza mishahara kwa asilimia 6%-10% kwa zaidi ya miaka mitano sasa, lakini hata motisha ya jumla kwa mwaka kwa wafanyakazi imeondolewa bila maadalizi ya kisaikolojia kwa watenda kazi za uzalishaji kitendo ambacho kimeondoa hamasa na utendaji bora kazini.

Makampuni husika hayajawahi kufunga shughuli za kiuchumi kwa sababu zozote na miradi mingi wanapata na kulipwa mamilioni ya fedha lakini wafanyakazi ambao ndio wanaostahili kupewa motisha hawathaminiwi tena ila wanajali marejesho ya mitaji yao oambapo wanapata faida kubwa bila kuathiri gharama za uendeshaji.

Je, Serikali kupitia wizara ya kazi, ajira na maendeleo ya vijana, ulemavu na watoto pamoja na shirikisho la waajiri Tanzania (ATE) wamebariki unyonyaji huu unaofanywa na wawekezaji kutoka nje ya nchi? Wafanyakazi kodi wanakatwa kubwa tu ambazo haijulikani kama huwa zinakilishwa serikalini kwa majina yao au hapana

Je, sheria za kazi ziko kimya kiasi kinachofanya wafanyakazi kudhalilika kiasi hicho?

Mamlaka husika tafadhali mulikeni kurunzi yenu kwenye kichaka hiki maana wanasingizia ugonjwa korona wakati wakijua sio kweli

UJUMBE Umewekwa mezani karibuni wadau maana wafanyakazi wana kilio chenye hasira za mkisi!!!
 
Kama biashara hakuna wafanyeje?
Mkuu,

Umesoma ukaumaliza uzi lakini au unakurupuka unawezekana ni mmoja wa wanufaika mnakandamiza wafanyakazi wa chini kwa visingizio visivyokuwepo. Mada imetaja bayana kwamba makampuni hayo bado yanaendelea kupata miradi na biashara zaidi lakini kisingizio ni korona wakati hawajawahi kufunga shughuli zao na wala hakuna mfanyakazi ambaye alishawahi kupunguzwa halafu wewe unadakia kana kwamba haupo Tanzania. Justice is impartial my friend so do not fuel angers to the productive human capital resources. So refrain politicking the serious matter of peoples affairs, it is not a constructive approach at all and the repercussion shall be of no remedial modality.
 
Wakuu,

Hili ni bandiko la mshangao na masikitiko kwa sauti za wafanyakazi kutoka sekta binafsi zimeiga seriklali kutoongeza mishahara kwa asilimia 6%-10% kwa zaidi ya miaka mitano sasa, lakini hata motisha ya jumla kwa mwaka kwa wafanyakazi imeondolewa bila maadalizi ya kisaikolojia
Maandalizi ya kisaikolojia? Mkuu, katika maisha tegemea lolote kutokea muda wowote. Kwa kiingereza wanaita "Contingency" kama sijakosea
 
Kampuni zinapo funga biashara wengine wanachekelea wengine wanaaumiaaa

moja ya mikakati ya kuweza kuendelea na wafanyakazi ulioko nao ni kuondoa marupurupu/bonus/ etc lengo ni kutomwachisha kazi, aendeleee na basic salary huku akiamua kuondoka aondoke na isiwe kampuni imemfukuza

kwa miaka hii nategemea kampuni nyingi kufanya mabadiliko katika uendeshaji, sio kwa nia mbaya bali kulingana na uhalisia wa biashara

mlowekeza kwenye kilimo mtupe gats nasi wengine tujee

Karudi baba mmoja toka safari ya mbali ...kavimba mapaja na mwili kutetemekaaa... watoto kuuliza mali ... akawajibu MALI MTAIPATA shambani /aridhini (madini)
 
Serikali yenyewe haijaongeza mishahara miaka sita sasa.
 
Sekta binafsi hawawezi kulipa mishahara mikubwa kuliko kima cha chini kilichopangwa na serikali.

Sasa wewe upo upo tu hujui tatizo ni ni nani ???
 
Hata hayo makampuni binafsi,ni ya watu wa kawaida Kama wewe,uongezwe mshahara kwa tija ipi?wewe umeongeza kitu gani kwenye kampuni?
Shukuru unachopata,kuongezewa mshahara,au kupewa bonsai,sio lazima,mwajiri akipenda sawa.
Miaka ya 2000,makampuni ya simu,yalikuwa yanatoa marupurupu Mengi sana kwa wafanyakazi,magari ya kutumia,hata ukiwa likizo,posho nono,mikopo,bonasi,
Sasa hv uchumi umebadirika,ukilazimisha makampuni yatoe nyongeza kila mwaka,utafunga makampuni Mengi,
Makampuni Mengi hata Kima Cha chini hawalipi,sembuse nyongeza,Kama unafikiri kufungua na kuendesha kampuni ni rahisi,acha kazi kaanzishe ya kwako.
Na kwa watumishi wa serikali wanapenda kulialia kila wakati,wakitaka kupandishwa vyeo,nyongeza za mishahara,posho za kila wakati,wasifikiri kwamba serikali inawategemea sana,au wao kuwepo kazini,wanaifsnyia hisani serikali,wao ndio wanaihitajj serikali kuriko serikali inavyowahitaji wao,
Wakishindwana waache ngazi tu,waende "wakajiajiri"Kuna watu wengi kitaa,wenye ujuzi,na nia ya kufanya kazi zao kwa malipo hata nusu.
Kama mshahara haukutoshi,acha kazj,kaanzishe kampuni yako ujilipe mamilioni.
 
Mbona serikali haiongezi mishahara pamoja na kujinasbu ongezeko la makusanyo ya kodi!
 
Ndo maana tunasisitiza Sekta binafsi izikwe kabisa
 
Back
Top Bottom