Makampuni gani yaliyoshinda tenda ya kuagiza sukari

Makampuni gani yaliyoshinda tenda ya kuagiza sukari

ERoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
48,052
Reaction score
104,677
Salam,
Hivi karibuni serikali kupitia body ya sukari Tanzania, Sugar Body of Tanzania ilitoa ruhusa kwa makampuni ya kitanzania kuagiza tani 5,000 za sukari toka nchi za nje.

Sababu za kutoa zabuni kwa makampuni ya kitanzania kuagiza sukari, licha ya kuwa viwanda vingi vinapinga zoezi hilo ni kuwa viwanda vinazalisha sukari takribani tani 400,000 kwa mwaka. Wakati huo huo matumizi ya sukari nchini kwa mwaka ni kama tani 500,000.

Sababu nyingine ni kuwa, mwezi wa tatu na wa nne viwanda vyetu huwa vinafungwa kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho na matengenezo, hivyo miezi hiyo miwili hakuna uzalishaji wa sukari.
Kwa maana hiyo basi, serikali ikatoa zabuni kwa makampuni na ndani ya miezi miwili wawe wameshaingiza tani zisizozidi 5,000 kwa kila kampuni ( hayo ni yale makampuni yaliyoshinda zabuni). Tatizo hayo makampuni yaliyopata hizo tender yamewekwa kama siri, na sisi tunaotaka kuwa third party katika hili dili tunakosa nafasi ya kufanya makubaliano nao.

Je, kuna mtu anafahamu kampuni gani zimepata hizo tender? Kama wapo humu tafadhali tuwasiliane ili tuongee vizuri.
 
Wa Kwanza ambae nina uhakika nae ni METL huyu ukifika KIUTA pale lazima ukute magari yake yakipeleka sukari kwenye godown zake.
 
Wa Kwanza ambae nina uhakika nae ni METL huyu ukifika KIUTA pale lazima ukute magari yake yakipeleka sukari kwenye godown zake.


Unamaanisha Mohammed Enterprises sio?
 
Back
Top Bottom