sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,687
- 1,111
Uchumi wa nchi umekuwa Sana na kufikia uchumi wa kati kabla ya muda ulio kusudiwa, maanake tume break event.lakini Maisha ya Watanzania hayahakisi uhalisia wa mabadiliko hayo ya uchumi.
Makamu wa rais amesema kuwa Hali ya umaskini kwa Watanzania ni mbaya Sana,wananchi zaidi ya milioni 14 wanaishi chini ya mstari wa umaskini,hii ni kutokana na sera na mifumo kandamizi iliyo filisi na kuuwa sekta binafsi.
Athari zake ni mzunguko wa fedha kuwa dormant kunako sababisha wananchi wa kawaida kuishi Maisha duni na kujiingiza kwenye biashara ya fedha iliyobeba dhana ya Mikopo kwa wajasiliamali,ili kukidhi haja za matatizo yao.
Mikopo hii maarufu Kama suluhisho kwa wajasiliamali,imebeba dhima nzito ya kuwatwisha zigo la marejesho wananchi kwa vigezo vilivyo thibitishwa na serikali kwa kuwaongezea umaskini zaidi kuliko kutumika Kama fursa.
Makampuni haya yamesajiliwa kwa mujibu wa sheria,yamepewa vibali vyote toka taasisi za kifedha,yanalipa Kodi lakini uendeshaji wake wa utoaji Mikopo ni tatizo kwa jamii.
Nitatoa mfano halisi kwa Hali ilivyo. Mathalani unakopeshwa laki moja(100,000/-) kwa mwezi unatakiwa kulia laki na ishirini(120,000/-),maanake laki moja kwa mwezi riba yake ni shilingi 20,000/- . Utaratibu wa marejesho ni kila siku na kwa kiwango cha 100,000/- unatakiwa kulipa 4,000/- kila siku kwa siku 30 bila kukosa ili kumaliza mkopo wako. Haijalishi public holiday Wala weekend.
Hoja yangu hapa nini!!!
Utaratibu unaotumika hauna tofauti na utakatishaji fedha(money laundering),mbaya zaidi ukiwa umebeba baraka zote za serikali.
Pili mfumo huu wa Mikopo unawaumiza Sana wananchi kwa kuwa hauzingati mwongozo wa ukopeshaji fedha kwa mujibu wa sheria na taratibu za upatikanaji riba. Hii inatoa picha jinsi gani wenye dhamana na mamlaka ya utoaji vibali hawatumi muda wao kukagua taasisi hizi ambazo zilikufa wakati wa Magufuli sasa zimerudi kwa kasi.
Ikiwa mkopo huo utaachiwa uendelee kuwaumiza wananchi kwa sababu ya umaskini wao,tutegemee kuutokomeza umaskini ni msamiati uliokosa maana halisi.
Nihisi serikali kulitazama jambo hili kwa umakini mkubwa,kwa kuwa wanaoumia ni wananchi, makampuni yamejazana wilayani kwa kujua uelewa wa wananchi ni mdogo katika mambo ya ukopeshaji na riba zake.