kwanza watueleze ilekampuni ya uwekezaji(NICOL) walioanzisha imefikia wapi mengi ni mtu mjanja ambaye amefanikiwa kwa kutumia propaganda ya vyombo vyake vya habari sasa hivi Azam anaanzisha tv nadhani tutaona mabadiliko makubwa kwenye tv zetu kwani kwa kutumia ushawishi wake alishinikiza wageni wasiruhusiwe kuendesha biashara ya tv kwa 100% ndio maana hata michezo kama kombe la mataifa ,ligi mbali mbali tumeshindwa kuziona bado kusahau kipindi kile alivyokuwa anatuweka usiku kusubiri ngumi za tyson kumbe zimeshapigwa zamani
Ndiye huyo huyo aliyelazimisha chanel ten wamruhusu kuonyesha kombe la dunia akijua kabisa hana haki
Ndiye miongoni mwa waliochangia NBC kuwa katika hali mbaya kutokana na kukaidi kulipa madeni alivyoandikwa kwenye vyombo vya habari akaja juu
kipindi cha Mwinyi aliwahi kulalamika juu ya wahindi kupewa viwanja katikati ya jiji alipopewa chake alikiuza nafikiri badala ya kusema wazawa wapewe angesema serikali iwe na hisa kubwa ili wananchi wote wanufaike
Aisee umeeleza kwa ufupi ila kwa ufasaha. Ifike wakati watu wafahamu kwa undani nia za ndani na rangi halisi za hawa matycoon ambao wanakuwa mstari wa mbele kutetea maslahi yao na ikibidi hata kukandamiza maslahi ya wengi ikiwa tu yataingiliana na maslahi yao.