Makampuni yanayotoa mikopo kwenye App yaige mbinu hii inayotumika Nigeria kuwaweza Watanzania watukutu; SMS za vitisho kwao ni sawa na wimbo

Makampuni yanayotoa mikopo kwenye App yaige mbinu hii inayotumika Nigeria kuwaweza Watanzania watukutu; SMS za vitisho kwao ni sawa na wimbo

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Ni nani ambae hakumbuki ule mtelezo wa app ya tala iliyokuwa ikitoa mkopo swafi kabisa wa elf 20 lakindi kwa mbongo ikawa ni kama zawadi.

Wabongo walichukulia kama zawadi hawakua na muda wa marejesho, haya meseji za vitisho zilivyoanza kutumwa ndio kwanza mtu anaweza pozi la 4 huku akishushia kinywaji na kucheka.

Kwa wenzetu huko wabishi Nigeria, haya matukio yaliwahi kutokea na watu walitumia fursa hizo kujipatia pesa za kula bata badala ya mikopo, mesej za vitisho tupa kule.

Sasa klichopo kwa sasa kuna dawa hii imesaidia kwa kiasi kikubwa (sio 100%) kufanya mtu alipe, unapewa mkopo hata laki 5 kupitia app lakini kwa namna wanayoijua watakusanya namba zako kuanzia wazazi, ndugu, ustadh / mchungaji, mme / mke wako, watoto wako, majirani, hadi ma ex, n.k.

Ukichelewa kurudisha mkopo wanatuma mesej kwa hao watu. Meseji wanaweza kutuma kama hii kwa mama yako

Habari yako, tunatoa onyo la mwisho kwa xxx arejeshe mkopo aliouchukua kwetu, jitihada za kumtafuta alipe zimeshindikana na ameonyesha wazi kabisa ni jeuri, hivi sasa ni mkimbizi anaekwepa mkono wa sheria kwa kukaidi ombi la kwenda kituo cha polisi kujisalimisha, tumeamua tukutumie meseji hii ili uweze kumsihi alipe deni lake ili tumalizane naye, meseji hii umeipokea kwasababu xxx aliweka namba yako wewe kama mtu wa alipokuwa anachukua mkopo"

Mesej hio kuna baadhi ya vitu ni uongo tu kama hapo kwenye kutafutwa na polisi, watu wako wataanza kukusihi ulipe na wanaweza kukusaidia kabisa lakini ni aibu, heshima yako itakuwa imeshuka mno, kuna kipindi hata mkikutana unaanza kuambiwa kama umekula maana wanadhani umefulia, mda mwengine unapigiwa simu na ndugu wakutaftie kibarua maana wanajua huna kazi labda, kwa ex wako ndio uakuwa kituko tu hasa pale walipoandika umeweka namba yake kama mtu wa karibu anakuona boya tu, mchungaji / ustadh nae atakwambia unahitaji maombi n.k. yaani hwahima yako inashuka watu wanakuona upo hoi kiuchumi.
 
Bado mtu anaweza kukopa kwa kutumia simu ambayo haina contacts. Hapo watafanyaje?
 
Bado mtu anaweza kukopa kwa kutumia simu ambayo haina contacts. Hapo watafanyaje?
Huko walishatupia jicho, wana njia zao za kuhakikisha mkopaji si janja janja, huenda wanashirikiana kabisa na mitandao ya simu
 
Unafikiri app ya Tala ilikuwa haikusanyi hizo taarifa?

Tena yenyewe ilifika mbali inaomba hadi permission ya ku-view gallery ya mkopaji
 
Unafikiri app ya Tala ilikuwa haikusanyi hizo taarifa?
Tena yenyewe ilifika mbali inaomba hadi permission ya ku-view gallery ya mkopaji
App ya tala tuliitumia wengi tu, haikuwa na mambo hayo, walikuwa wanakutumia mesej za vitisho mhusika wewe kama wewe
 
App ya tala tuliitumia wengi tu, haikuwa na mambo hayo, walikuwa wanakutumia mesej za vitisho mhusika wewe kama wewe
Chief usiwe mbishi tafuta nyuzi za tala humu kama utakosa maoni yangu nilifikisha hadi laki saba+ ndipo nilipo wadundia.

Ukipakua app yao wakati unai-launch kwenye device yako wanaomba kusoma yote hayo ni the same na wanavyofanya branch. Tofauti ni ilikuwa moja tu branch wanataka majina ya namba ya simu na ID utakayotumia na Facebook account yafanane kwa 100% Tala hawakuwa na hili
 
Gharama za kumfuatilia mtu mmoja n mara 1000 ya mkopo uliochukua hata watumie mbinu hizo ndio maana branch wamefeli,Tala wamefeli,imarisha,mpawa Keisha songesha kwisha,nivushe Tigo kwisha, timiza kwisha,imarisha wamepona
 
Back
Top Bottom