PreGE2025 Makamu Mwenyekiti CCM Stephen Wasira: CCM imeanza kuwabaini wanaotumia pesa ili wachaguliwe

PreGE2025 Makamu Mwenyekiti CCM Stephen Wasira: CCM imeanza kuwabaini wanaotumia pesa ili wachaguliwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Steve Wasira amewaagiza Wenyeviti wa CCM ngazi za mkoa na wilaya nchini kusimamia maadili wakati huu wa kuelekea kwenye Uchaguzi mkuu ili kuwapata wagombea wanaokubalika kwa watu badala ya wale wanaotegemea pesa kama mtaji wao wa kuwafanya wateuliwe kwenye kura za maoni ambao amesema tayari Chama kimekwisha baini wapo ambao wameanza kujitokeza kutoa pesa ili wateuliwe kwenye mchakato wa kura za maoni.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Wasira ametoa agizo hilo leo mjini Tabora akianza ziara mkoani humo ambapo amekutana na Wajumbe wa halmashauri kuu zilizoboreshwa katika wilaya za Tabora mjini,Uyui,Nzega na Igunga akihamasisha kupata wagombea wenye sifa zinazostahili na sio wale ambao wameanza kutoa fedha ili kupata nafasi za kugombea Ubunge na Udiwani

 
Yeye ataacha lini kusema uongo au kuruka kwa kutumia ndege yake ya asili??
 
Back
Top Bottom