Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Steve Wasira amewaagiza Wenyeviti wa CCM ngazi za mkoa na wilaya nchini kusimamia maadili wakati huu wa kuelekea kwenye Uchaguzi mkuu ili kuwapata wagombea wanaokubalika kwa watu badala ya wale wanaotegemea pesa kama mtaji wao wa kuwafanya wateuliwe kwenye kura za maoni ambao amesema tayari Chama kimekwisha baini wapo ambao wameanza kujitokeza kutoa pesa ili wateuliwe kwenye mchakato wa kura za maoni.
Wasira ametoa agizo hilo leo mjini Tabora akianza ziara mkoani humo ambapo amekutana na Wajumbe wa halmashauri kuu zilizoboreshwa katika wilaya za Tabora mjini,Uyui,Nzega na Igunga akihamasisha kupata wagombea wenye sifa zinazostahili na sio wale ambao wameanza kutoa fedha ili kupata nafasi za kugombea Ubunge na Udiwani