CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Stephen Wasira amefika kutoa pole nyumbani kwa Waziri Wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa na kushiriki dua ya kisomo kufuatia kifo cha Baba yake mzazi, Alhaj Omary Mchengerwa.
Alhaj Omary Mchengerwa, amefariki dunia alfajiri ya leo Jumatatu, Februari 24, 2025 akiwa katika Ibada ya Umrah, Makkah.
Soma Pia: Waziri wa TAMISEMI Mohammedi Mchengerwa Amefiwa na Baba Yake Mzazi Akiwa Ibadani Makka Na Atazikwa hukohuko Makka
Leo Jumanne, kutafanyika dua ya kisomo jimboni Rufji, Mkoa wa Pwani na Jumatano itafanyika dua nyumbani kwa marehemu Alhaj Omary Mchengerwa Yombo, jijini Dar es Salaam.