NCCR Mageuzi
Member
- Oct 3, 2007
- 23
- 63
Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha NCCR-Mageuzi ndugu James Francis Mbatia anasikitika kutangaza kifo cha makamu mwenyekiti mstaafu Tanzania Bara ndugu Rakia Abubakar Hassan kilichotokea siku ya Jumamosi Januari 30, 2021 Morogoro.
Marehemu alikuwa mmojawapo wa wanachama waanzilishi wa NCCR-Mageuzi tangu mwaka 1992 hadi umauti. Alikitumikia chama kwa mapenzi makubwa na kwa uadilifu mkubwa hadi kufanikiwa kupata nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi mbalimbali.
- Makamu mwenyekiti Tanzania Bara- (2009-2014)
- Mjumbe wa Halmashuri kuu ya Taifa wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa- (2014 hadi Umauti)
- Mjumbe wa Baraza la wadhamini- (2019 hadi Umauti)
- Mratibu wa Jumuiya ya wanawake mkoa wa Morogoro- (2003-2009)
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI. AMINA