- Source #1
- View Source #1
Siyo umbea sikiliza mwenywe
NCHI HII TUMELOGWA. NA HII NI KWA VILE ANAJUA ATAIBA KURA ATASHINDA! TUME IKO UPANDE WAKE ATAIBA KURA ATASHINDA
NCHI HII TUMELOGWA. NA HII NI KWA VILE ANAJUA ATAIBA KURA ATASHINDA! TUME IKO UPANDE WAKE ATAIBA KURA ATASHINDA
- Tunachokijua
- Stephen Wasira ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyeteuliwa mnamo tarehe 18 Januari 2025 akimrithi mtangulizi wake katika nafasi hiyo Abdulrahman Kinana. Pia amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Bunda mwaka 2005 hadi 2015.
Wasira ni mwanasiasa mkongwe ndani ya CCM ambaye amewahi kutimkia NCCR mageuzi mwaka 1995, baada ya kushindwa kwenye kura za maoni za ndani ya CCM, dhidi ya Jaji Joseph Warioba (Waziri Mkuu na Makamu wa Rais Mstaafu). Wasira hakuridhishwa na ushindi wa Warioba na aliamua kukihama chama hicho na kwenda NCCR Mageuzi wakati huo ikiwika na akachaguliwa kuwa mbunge kupitia NCCR lakini 1996 mahakama ilitengua ubunge wa Wasira baada ya Warioba kukata rufaa Mahakama Kuu.
Kumekuwapo na video inayomuonesha Wasira akisema atagombea ubunge jimbo la Bunda ikidaiwa kuwa ni ya mwaka 2025.
Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search umebaini kuwa video ilichapishwa mtandaoni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020
Katika video hiyo Wasira aliweka bayana nia yake ya kutaka kugombea ubunge mwaka 2020 katika jimbo la Bunda huku akionesha kutoridhishwa na uchaguzi wa mwaka 2015 ambao alishindwa kutetea kiti hicho dhidi ya Ester Bulaya akidai uchaguzi huo uligubikwa na hujuma.
Baadaye tarehe 15 Julai, 2020 Wassira alichukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara hata hivyo hakufanikiwa kuapata nafasi hiyo baada ya kuteuliwa Robert Chacha Maboto kupeperusha tiketi ya ubunge kupitia chama hicho.