Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
View: https://www.youtube.com/watch?v=It3WB1-ceDw&ab_channel=JAMBOTV
Isihaka Mchinjita - Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ACT Bara
"Kama tulikuwa tunasubiri kuona maneno ya Rais Samia ni ya kweli au ni ya unafiki bsi uchaguzi wa Serikali za Mitaa basi ni ushahidi kuwa Rais Samia aliwanafikia Watanzania na bila iabu tukaenda kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa "
"CCM wanajua Uchaguzi wa mwaka 2019 ulikuwa umeharibiwa. Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wao Abdulrahman Kinana alikuja kwenye mkutano Mkuu wetu na akasema kinachowakatisha tamaa Watanzania ni uhribifu uliofanywa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019"
Katibu Mkuu wa sasa Emmanuel Nchimbi tumekutana nae TCD na mara zote kwenye kikao cha mwisho tukijadili mbovu zilizoletwa na TAMISEMI pale TCD watu wote walikuwa wanarejea uharibifu uliofanywa 2019. Aliposimama bila aibu akasema yale ya mwaka 2019 tunaomba tusiyataje taje sana, kwa sababu kulikuwa na mazingira maalum tunaomba tuyaache twende mbele"
Makamu wa kwanza Rais Zanzibar - Othman Masoud Othman
"Huko nyumba alishawahi kusema yule aliyetangulia, alisema atahakikisha vyama vya upinzani vitakufa. Lakini vyama vya upinzani vipo na vinaendelea kuwa imara"
"Chama chetu kilifanya siasa kwa mujibu wa siasa zilivyokuwa. Siasa tulizotoka ni za kuaminishwa kwamba tunakwenda kwenye siasa za maridhiano. Tulifanya engagement kwenye ngazi zote. Hakuna kiongozi wa CCM ambaye hatukumfika"
"Tuliamini kwenye siasa za maridhiano, tuliamini kwenye siasa za kistaarabu. Na tumeyafanya haya Tanzania bara na Zanzibar kwa kuingia kwenye maridhiano. Malipo yetu yalikuwa ni nini? Malipo yetu ilikuwa viongozi wetu ikiwemo Mwenyekiti wetu wa ngome ya vijana kukamatwa, kutekwa na kuteswa"
"Tume yetu ya Uchaguzi imekuwa kama yule mwigizaji Joti. Maana Joti akivaa nguo za kike anaitwa nani? Kiboga. Akivaa kaptula kwenda shule anakuwa andunje lakini si joti yuleyule"
"Baada ya kukutana tumeamua kuwa ni muda wa chama chetu kubadili namna ya kufanya siasa katika nchi yetu na sasa ni wakati wa kwenda na hali ya bahari yenyewe ilivyo. Chama chetu kimeamua kitoke kwenye siasa za maridhiano, sasa twende kwenye siasa zinazohitajika kwa wakati huu, siasa za mapambano"