Pre GE2025 Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar: ACT kimeamua kitoke kwenye siasa za maridhiano, tunaanza kufanya siasa za mapambano

Pre GE2025 Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar: ACT kimeamua kitoke kwenye siasa za maridhiano, tunaanza kufanya siasa za mapambano

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hiki chama zito kabwe yumo? Kama yupo atawavuruga kweli kweli! Jamaa huyu siku hizi ni msaliti na mlamba miguu ya mama
 
WAnasiasa wajanja sana.
Katulia kwanza kala mema ya nchi miaka 4, anaona uchaguzi umekaribia ndipo anajifanya anaanza mapambano...
Je uchaguzi ni haki ili akosen sababu ya siasa za mapambano? Amesema kilichokuwa kinaendelea ni siasa za ulaghai, ila uchaguzi wa SM za umeonyesha ni ulaghai tu.
 
No reform No election
shikilieni hapo hapo Msije kubadilika!
 
Ila dalali zito na wenzako mnavituko sana mmekula mema ya nchi miaka 4 unakaribia uchaguzi mnataka kuhadaa wananchi

Baada ya uchaguzi unarudisha tena mpira kwa kipa
 

View: https://www.youtube.com/watch?v=It3WB1-ceDw&ab_channel=JAMBOTV

Isihaka Mchinjita - Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ACT Bara

"Kama tulikuwa tunasubiri kuona maneno ya Rais Samia ni ya kweli au ni ya unafiki bsi uchaguzi wa Serikali za Mitaa basi ni ushahidi kuwa Rais Samia aliwanafikia Watanzania na bila iabu tukaenda kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa "

"CCM wanajua Uchaguzi wa mwaka 2019 ulikuwa umeharibiwa. Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wao Abdulrahman Kinana alikuja kwenye mkutano Mkuu wetu na akasema kinachowakatisha tamaa Watanzania ni uhribifu uliofanywa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019"

Katibu Mkuu wa sasa Emmanuel Nchimbi tumekutana nae TCD na mara zote kwenye kikao cha mwisho tukijadili mbovu zilizoletwa na TAMISEMI pale TCD watu wote walikuwa wanarejea uharibifu uliofanywa 2019. Aliposimama bila aibu akasema yale ya mwaka 2019 tunaomba tusiyataje taje sana, kwa sababu kulikuwa na mazingira maalum tunaomba tuyaache twende mbele"

Makamu wa kwanza Rais Zanzibar - Othman Masoud Othman

"Huko nyumba alishawahi kusema yule aliyetangulia, alisema atahakikisha vyama vya upinzani vitakufa. Lakini vyama vya upinzani vipo na vinaendelea kuwa imara"

"Chama chetu kilifanya siasa kwa mujibu wa siasa zilivyokuwa. Siasa tulizotoka ni za kuaminishwa kwamba tunakwenda kwenye siasa za maridhiano. Tulifanya engagement kwenye ngazi zote. Hakuna kiongozi wa CCM ambaye hatukumfika"

"Tuliamini kwenye siasa za maridhiano, tuliamini kwenye siasa za kistaarabu. Na tumeyafanya haya Tanzania bara na Zanzibar kwa kuingia kwenye maridhiano. Malipo yetu yalikuwa ni nini? Malipo yetu ilikuwa viongozi wetu ikiwemo Mwenyekiti wetu wa ngome ya vijana kukamatwa, kutekwa na kuteswa"

"Tume yetu ya Uchaguzi imekuwa kama yule mwigizaji Joti. Maana Joti akivaa nguo za kike anaitwa nani? Kiboga. Akivaa kaptula kwenda shule anakuwa andunje lakini si joti yuleyule"

"Baada ya kukutana tumeamua kuwa ni muda wa chama chetu kubadili namna ya kufanya siasa katika nchi yetu na sasa ni wakati wa kwenda na hali ya bahari yenyewe ilivyo. Chama chetu kimeamua kitoke kwenye siasa za maridhiano, sasa twende kwenye siasa zinazohitajika kwa wakati huu, siasa za mapambano"

Hawa wajinga wameanzisha Tena kampeni ndogo katikati ya kampeni kubwa.

Wakati wenzao wakiwa kwenye kampeni ya kupigania katiba mpya wao walianzisha yao ya Time huru ya Uchaguzi kuelekea katiba mpya lengo ilikuwa ni kuwapa gate way CCM ya kukwepa katiba mpya na
Sasa No reforms No election imewaibua tena mafichoni.

Same people same script
 
Hongereni sana ACT,kwa kuutambua ukweli na kuwa tayari kufanya siasa kwa kuzingatia mazingira na ubaramia wa aliyeshikilia mpini.

Kwasasanguvu zote za vyama vya upinzani, na watanzania wote wazalendo na qenye mapenzi mema kwa Taifa, tuelekeze nguvu zote katika kuondoa mazingira shetani kwenye uchaguzi.

NO REFORM NO ELECTION ihame kutoka kuwa ya CHADEMA, na kuwa ndiyo msimamo wa vyama vyote vya upinzani, na uwe ndio msimamo wa wananchi wote walio wazalendo wa kweli kwa Taifa letu.

Viongozi wa vyama vya upinzani, wanaharakati, watetezi wa haki, viongozi wa dini, na asasi mbalimbali, andaeni mkutano mkubwa wa pamoja utakaowahusisha wananchi na viongozi wote, ili kutoa tamko la pamoja.
Lakini kumbuka ACT wanaendelea na zoezi la kuandaa wagombea wa ubunge. Uwakilishi na nadiwani, nyinyi CHADEMA endeleeni kuingizwa mkenge; Oktoba 2025 mtawaona wenzenu bungeni, baraza la wawakilishi na katika serikali ya umoja wa kitaifa Januari 2926.

Mtakumbuka shaka kumekucha.

Hawa wanaokesha kujadili mechi ya Simba na yanga kutofanyika ndio waingie barabarani?
 
Uamuzi sahihi kabisa bado Mzee Hashim Rungwe ulaghai wa Samia umeshtukiwa thank you God.
 
Back
Top Bottom